Iker Casillas ateuliwa kuwania tuzo ya golikipa bora katika kikosi cha shirikisho la soka duniani (FIFA) cha mwaka 2014.
Casillas ambaye ni golikipa wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania amejumuishwa katika kiny’ang’anyiro hicho pamoja na Manuel Neuer (Bayern Munich, Germany), Gigi Buffon (Juventus, Italy), Thibaut Courtois (Chelsea, Ubelgiji) na Claudio Bravo (FC Barcelona, Chile).
Kujumuishwa kwa nahodha huyo wa Hispania kumewashangaza watu wengi kwani Casilllas alicheza mechi mbili tu katika msimu wa 2013/2014 ndani ya La Liga huku akifanya vibaya katika michuano ya kombe la Dunia huko nchini Brazil huku timu ya taifa ya Hispania ikitupwa nje katika hatua ya makundi.
Mshindi wa nafasi hiyo ya golikipa ambaye hupigiwa kura na wachezaji wapatao ishirini elfu kutoka duniani kote atatangazwa mnamo tarehe kumi na mbili mwezi wa kwanza mwaka 2015 kwenye ugawaji wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (Ballon d’Or).