Rapa Lil Wayne anakabiliwa na kesi ya kujibu baada ya kushtakiwa na aliekuwa dereva wa gari la msafara wa show yake ya mwaka 2014 summer concert tour. Mark Jones amemtuhumu Lil Wayne kwakutaka kufanya jaribio la kumuua wakati anaendesha msafara wa msanii huyo na kikosi chake ambapo dereva huyo amedai kuwa Wayne alikuwa akitumia lugha za vitisho anapotoa maelekezo ya msafara huo mfano alipotaka kwenda hotelini alimfuata na bunduki na kuiweka sawa kisha akamuamuru afuatishe matakwa yake la sivyo...
Mama mzazi wa Beyonce mwenye umri wa miaka 61, Tina Knowles amefunga ndoa na muigizaji Richard Lawson mapema mwishoni mwa wiki kwenye boti maalum katika ufukwe wa Newport huko marekani. Hii ni harusi ya pili kwa Tina Knowles ambae alifungua kesi ya madai ya taraka mwaka 2009 kutoka kwa baba mzazi wa Beyonce ambae pia alikuwa meneja miaka ya nyuma bwana Mathew Knowles Mwezi Octoba Tina ambae pia ni mbunifu wa mavazi aliweka wazi mahusiano hayo na muigizaji huyu Richard...
Mwanasheria wa mkali wa ngoma zilizowahi kufanya vizuri ikiwemo Just a dream na Dilema ameanza kufanya harakati za utetezi kwa msanii huyo kwakudai dawa za kulevya alizokamatwa nazo hazikuwa zake. Nelly alitiwa nguvuni na vyombo vya usimamizi wa sheria baada ya gari lake la msafara wa kikazi kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na silaha ndani yake. Mwanasheria huyo wa Nelly Scott Rosenblum kwenye mahojiano yake na mtandao wa Tmz amedai kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 15...
Rapa Meek Mill anakabiliwa na kesi ya kujibu baada ya kupuuza onyo ama katazo lililotolewa na mmiliki wa eneo la moja ya mabangaloo maarufu nchini marekani glass mansion linalopatikana Beverly Hills. Katika onyo hilo lilitolewa na mmiliki huyo lilimtaka Meek kutofanya party ya aina yoyote itakayoleta mkusanyiko wa watu kwenye eneo hilo Katika mkataba waliowekeana na Meek Mill mmiliki huyo ameelezea kipengere kilichosainiwa na Meek kwamba asifanye party eneo hilo ambapo uongozi wa kampuni ulionya kutofanyika kwa Grammy...
Mkali kutoka code ya 254 kwa Uhuru Kenyata Wahu ni miongoni mwa wasanii wachache Afrika Mashariki walioweza kudumu kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya muongo mmoja. Kumekuwa na kimya kirefu kwa msanii huyu toka afanye vizuri na wimbo wake wa still a liar kwenye vituo tofauti vya redio na tv. Kufuatia ukimya huo maswali yamekuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii kwa mashabiki wake kutaka kufahamu iwapo kama ameachana kabisa na muziki na haya ni majibu yake. ‘’j_doctor did you...
Tom Cruise amesema hakupata nafasi ya kukutana na mtoto wake kwa takribani mwezi sasa kufuatia kubanwa na ratiba kikazi ambapo kwa maelezo aliyoyatoa star huyo amedai hali hiyo imetokana na kuwa busy na kushoot filamu ya “Mission Impossible 5” huko London. Hivyo yalibaki masaa kadhaa aweze kukutana na binti yake Suri. Ila chanzo kinadai kuwa muigizaji huyo alikuwa mapumzikoni kwa takribani wiki mbili mara baada ya ratiba ya kushoot kufungwa lakini hakwenda kumtazama mwanae. Chanzo cha karibu na Katie...
Katika kuonyesha mapenzi na ukaribu walionao na kituo hiki kampuni ya uandaaji wa Filamu nchini 5 effects ni moja kati ya kampuni zilikuwa pamoja nasi na kututakia heri kwenye kumbukumbu ya kunzishwa kwa kituo hiki hapo...
Huu ni wimbo uliyotayarishwa katika studio za Vipaji Tz chini ya Producer Abba Artist : Muzdy ft Rich Mavoko Song: Mboni yangu unaweza kuusikiliza na kudonwload hapa ...
Mastar wakubwa duniani katika tasnia ya muziki wameunganisha nguvu pamoja na katika uzinduzi wa kampuni ya muziki ya Tidal. Katika uzinduzi huo wa kampuni ya kwanza kubwa ya muziki duniani kumilikiwa na msanii Jay z uliofanyika siku ya jumatatu katika jiji la New York ulishuhudiwa na mastar ambao pia wametajwa kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo Miongoni mwa mastar hao ni Rihanna, Madonna, Beyonce, Usher, Daft Punk, Arcade Fire, Jack White na Kanye West. Akizungumzia matarajio yake juu ya...
Mkali wa muziki wa pop duniani Akon amewasili nchini Kenya siku ya ijumaa tayari kuhudhuria kwenye kilele cha tamasha la kutafuta vipaji vya muziki la Airtel Trace Music. Msafara wa Akon unaundwa na timu ya watu mashughuli duniani akiwemo Devyne Stephens pamoja na mkongwe aliegundua wakali kama Jay Z, P Diddy, Alicia Keys, Usher, Mariah Carey, Akon n.k Tanzania inawakilishwa na Mayunga ambae alishinda kwenye mashindano ya hapa nyumbani nakupata nafasi ya kusonga...
Mbali na director mkali wa filamu pamoja na muziki Marekani Brett Ratner kuukana ukweli kuhusu yeye kuwa na mahusiano na Mariah Carey na kuziita taarifa hizo ni utoto kwa sasa ameshindwa kuficha kikohozi chake kufuatia kuonekana kwa picha tofauti zikiwaonyesha wawili hao wakiwa pamoja katika muonekano wa wakimapenzi. Mariah Carey na Brett Ratner wanatofauti ya mwaka mmoja wakati Ratner akisherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya ijumaa huku ya Mariah Carey ikifuata siku ya jumamosi. Moja kati ya picha hizo inawaonyesha wawili hawa...