Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na kelele serikali imewaelekeza wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama inavyoelekezwa kwenye masharti ya leseni zao. Hili ni kwa sababu ya kulinda afya za wananchi kutokana na athari za kelele na mitetemo. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Seleman Jaffo wakati akiongea na vyombo vya habari Juni 29 kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na...
“Watoto waelekezwe kuhusu matumizi ya barakoa, wajue namna ya kuzivaa, waelekezwe na mahali pa kuzitupa” Dkt Ama. Alikuwa anajibu maswali ya Dina Marious kuhusu madhaara ya Corona kwa watoto. Japo hawako kwenye hatari kubwa kama wazee, lakini mi muhimi walindwe. . Swebe alisema watoto kwa kutokuelezwa vizuri kuhusu Barakoa, wawapo shuleni wanaweza kuchangia, au kuokota na kuzivaa. . Hivyo wazazi wanasisitizwa kuwalinda watoto, lakini pia Wizara ya Afta kwa kushirikiana mamlaka nyingine na walimu wanahakikisha watoto wanaelezwa vyema na...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambao wanataka akamatwe ili wajitoe udhamini. Mahakama imetoa siku 7 kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na maombi ya wadhamini, Ibrahim Ahmed na Robart Katula Julai 14, mwaka huu ambapo Wadhamini hao wamefungua maombi wakiiomba itoe hati ya kumkamata kwa kuwa wameshindwa kumpata na kumfikisha Mahakamani hapo. Maombi hayo namba 2/2020 yalipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi...
Rais Magufuli ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kuhakikisha wafanyabiashara ndogondogo (Machinga), mama lishe pamoja na magari ya mizunguko mifupi jijini, (Daladala) kutengewa maeneo ya kufanya kazi katika stendi mpya ya kisasa Dodoma. Ametoa agizo hilo Jun 18 kwa njia ya simu, baada ya Mkurugenzi kuwatembelea wafanyabiashara katika stendi hiyo na kusikiliza kero zao. Ameongeza kuwa Mama lishe lazima wawepo, ikiwa stendi hiyo imejengwa kwaajiri ya watanzania wote wakiwepo maskin ambapo Hakuna sababu ya kuwa na...
Rais Magufuli amesema amemsamehe aliyekuwa Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye baada ya kumuomba msamaha kwa zaidi ya mara tatu na viongozi wengine katika jeshi hilo ambao ilitakiwa awafukuze. Amesema kwa upande wa Andengenye, hawezi kumrudisha katika Jeshi hilo ila ataonekana katika kazi nyingine kwani mtu akiomba msamaha na kuonesha kutubu inabidi asamehewe Rais Magufuli ametangaza msamaha huo huku akitoa onyo kwa askari wa Jeshi la Zimamoto juu ya uchukuaji wa rushwa na kuingia mikataba...
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango ametoa shukurani kwa shirika la fedha duniani, (IMF) kwa kusamehe deni ambalo walikuwa wanaidai Tanzania la takriban Bilioni 33. Ametoa shukurani hiyo leo Juni 11, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa anawasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 na kusisitiza kuwa wanaendelea kuomba mashirika mengine yatoe msamaha wa madeni. Hii baada ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) jana, kutangaza limeisamehe Tanzania deni lenye thamani ya Dola Milioni 14.3 (takriban Tsh. Bilioni 33) ambalo...
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2020/2021 utazinduliwa tarehe 15 Juni 2020, ambapo serikali imejiweka kando kutopanga bei elekezi katika zao hilo pamoja na mazao mengine badala yake bei za mazao zitatokana na soko. Ameyasema hayo, wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza. Ameongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inasimamia uzalishaji bora wa mazao kadhalika...
Daraja la Wami, ajali mbili tofauti zimetokea kwa kufuatana mara baada ya malori hayo kufeli breki na kusababisha vifo ambapo Lori la kwanza limesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wawili, huku lori la pili likiwa limesababisha vifo vya watu wawili mama pamoja na mtoto mdogo. Katika ajali ya Lori la kwanza lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Arusha limepoteza mtu mmoja ambae alikuwa dereva aliyeshindikana kuokolewa kufuatia kushindwa kufungua mkanda wa gari hivyo amezama katika mto wami wenye kina...
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameagiza vyuo vyote nchini kuhakikisha hadi kufikia ijumaa Juni 5, mwaka huu viwe vimeshawalipa wanafunzi wote fedha zao za kujikimu na ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua. Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo leo Juni 3, jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi magari manne kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho ni miongoni mwa vyuo vinne vitakavyonufaika na mkopo wa Benki ya Dunia kupitia mradi wao wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi...
Vijana nchini wametakiwa kuachana na biashara ambazo zimekuwa zikiwapotezea muda na badala yake wajikite katika ubunifu wa kazi wanazozifanya, ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayobadilisha maisha yao. Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, katika uzinduzi wa shughuli za kiubunifu Kitaifa zilizofanyika jijini Dodoma, zilizoandaliwa na Tanzania Innovation Explore Gala. “Epukeni biashara zinazowapotezea muda, haiwezekani miaka mitano unafanya biashara isiyokupa faida,...
Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles ‘Jaguar’ Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa. Hatua hiyo inajiri huku Mbunge huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi usiku kucha ambapo anasubiri kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi. Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya, licha ya wabunge wengi kushutumu jinsi ambavyo bwana Jaguar alitoa hoja yake , baadhi yao walikubaliana kwamba kuna swala tata kuhusiana na raia wa...