Local News

erikali yaagiza waliolipia ving’amuzi Azam, Dstv, Zuku warejeshewe fedha
Local News

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema kampuni zinazotoa huduma za ving’amuzi zinapaswa kuwarejeshea fedha wateja wanaotumia ving’amuzi hivyo kutokana na kukiuka masharti ya leseni. Kamwelwe amezitaja kampuni hizo kuwa Azam, Dstv na Zuku na kwamba zimekiuka masharti ya leseni zao. Kampuni hizo ziliondoa chaneli za ndani zisizolipiwa baada ya tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), lililokusudia kusimamisha leseni kwa maelezo ya ukiukwaji wa masharti. Tangazo hilo la TCRA lilieleza kuwa kampuni hizo...

Like
512
0
Sunday, 12 August 2018
Mtatiro Ajiondoa CUF, Ajiunga CCM
Local News

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF Julius Mtatiro amejivua uanachama wa chama hicho nakujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM huku akisema kuwa huu ni wakati wake wakwenda kutumia vipaji vyake kikamilifu pia kuwa balozi mkubwa wa Rais Magufuli Ndani na nje ya Nchi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyie nchi yake maendeleo. Katika hatua nyingine baada ya...

Like
416
0
Saturday, 11 August 2018
Uingereza yaipatia Tanzania Sh307 bilioni
Local News

Serikali ya Uingereza imetoa msaada wa Sh 307.5 bilioni kwa Tanzania ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais John Magufuli katika elimu, mapambano dhidi ya rushwa na uboreshaji huduma za afya. Msaada huo umetangazwa leo Ijumaa Agosti 10, 2018 na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Penny Mordaunt alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, inasema kuwa Mordaunt amesema fedha hizo zimetolewa...

Like
393
0
Friday, 10 August 2018
Mwanasiasa wa Zimbabwe Tendai Biti anyimwa hifadhi Zambia
Local News

Mwanasiasa wa cheo cha juu kwenye muungano wa upinzani nchini Zimbabwe MDC Tendai Biti amenyimwa hifadhi kwenye taifa jirani la Zambia. Polisi wa Zimbabwe wanamlaumu Bw Biti kwa kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Zambia Joe Malanji aliiambia BBC kuwa vigezo vya vyake kuomba hifadhi vilikuwa dhaifu. Alizuiwa eneo salama hadi pale aliporejeshwa Zimabwe, waziri alisema. Mapema wakili wake alisema mteja wake alikuwa amezuiwa kwenye mpaka na Zambia na mamlaka za...

Like
458
0
Thursday, 09 August 2018
Serikali Yaondoa zuio la Kuuza Mazao Nje ya Nchi
Local News

Serikali imeondoa zuio la kuuza mazao nje ya nchi ili kutoa fursa soko na mapato kwa wakulima. Hata hivyo, wanaotaka kuuza mazao nje ya nchi watalazimika kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Uamuzi huo umetangazwa leo Agosti 8 na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa akiyafunga rasmi maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. “Hata hivyo, lazima kila mwananchi kuanzia ngazi ya kaya kuhakikisha uwepo wa akiba na usalama wa chakula,” amesema Mkapa Amewataka...

Like
613
0
Wednesday, 08 August 2018
Tanzia: King Majuto Afariki Dunia
Local News

Muigizaji Mkongwe wa sanaa za vichekesho, Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki pamoja na wadau wa filamu nchini. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi...

Like
664
0
Wednesday, 08 August 2018
Ethiopia yatia saini mkataba wa kumaliza uhasama na waasi wa Oromo Liberation Front – OLF
Local News

Serikali ya Ethiopia imetia saini muafaka wa amani na kundi moja kuu la waasi nchini humo Oromo Liberation Front- OLF, ili kukomesha uhasama nchini humo. Awali utawala huko Addis Ababa ulitangaza kuwa sasa kundi hilo halitaitwa la kigaidi kama ilivyokuwa ikijulikana hapo awali. Hayo yametangazwa muda mfupi uliopita na Runinga ya taifa nchini Ethiopia ambapo mkataba huo umesainiwa katika mji mkuu wa Eritrea ambapo ndio makao makuu ya OLF. Waziri wa habari wa Eritrea Yemane Gebremeskel amesema kwa sasa OLF...

Like
358
0
Wednesday, 08 August 2018
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto.
Local News

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto. Amesema elimu hiyo itawawezesha kinamama kupata kizazi chenye afya bora na kushiriki vyema masuala ya uchumi na kijamii kwa siku zijazo. Ameyasema hayo leo Agosti 7 muda mfupi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji watoto duniani yaliyofanyika mjini humo kwa ngazi ya wilaya ya Kisarawe. Hii ni kazi ya kwanza kwa Jokate tangu ateuliwe na kuapishwa...

Like
743
0
Tuesday, 07 August 2018
JASINTA MBONEKO ALA KIAPO CHA UKUU WA WILAYA YA SHINYANGA
Local News

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack amemuapisha Jasinta Venant Mboneko kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Agosti 6,2018. Hafla fupi ya kuapishwa kwa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Shinyanga imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,vyama vya siasa,taasisi na wadau mbalimbali. Akizungumza baada kula kiapo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mheshimiwa Jasinta Venant Mboneko alisema amekuja wilayani humo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kusimamia...

Like
701
0
Monday, 06 August 2018
Kangi Lugola Atoa Onyo Makampuni ya Ulinzi Yanayoajiri Vikongwe
Local News

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Alphaxard Lugola, ametoa mwezi mmoja kwa makapuni binafsi ya ulinzi nchini kuhakikisha yanarekebisha mfumo wao wa kuajiri pamoja na utoaji wa mishahara kabla ya Wizara yake haijaanza kuyahakiki makampuni hayo. Lugola amesema baadhi ya Makampuni hayo yameajiri wazee wasiojiweza ambao muda wote wanalala na wanasabaisha uhalifu kuendelea kwa kasi, wakati vijana wapo wengi wenye nguvu zao wanaweza wakazifanya kazi hizo kwa umakini zaidi, na pia tatizo lingine wanalipwa mishahara midogo hali hiyo...

Like
617
0
Monday, 06 August 2018
BAD NEWS: Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla limepata ajali
Local News

BAD NEWS: Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla limepata ajali Magugu, Manyara na Ofisa wa habari, Hamza Temba amefariki dunia. RPC, Augustino Senga Manyara...

Like
804
0
Saturday, 04 August 2018