MTANDAO wa Kijinsia Tanzania-TGNP umeitaka jamii kuishi kwa kufuata mbinu za kiraghibishi yaani utafiti ili kumuwezesha mtu kutambua nafasi yake na uwezo wa kubadilisha mazingira ili kuleta maendeleo nchini. Akizungumza katika semina ya Uraghibishi,mtafiti Mkuu kutoka TGNP AGNESS LUKANGA amesema kuwa endapo jamii itaweza kuishi kwa kufuata njia za Uraghibishi itaweza kujitegemea ikiwa ni pamojua na kuhamasisha mtu kufanya kitu ambacho kitaleta maendeleo katika jamii. Ameeleza kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kutoa maamuzi ya mambo...
KAMPUNI ya Simu ya Push Mobile imetiliana saini na Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa -UN ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu Ugonjwa hatari wa Ebola. Kwa mujibu wa Taarifa ya Umoja wa Mataifa, Kampuni hiyo ya Simu imesema kupitia ushirikiano huo Kampuni hiyo itaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa Elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola. Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, Serikali na...
SIKU moja baada ya kuibuka kwa vurugu kubwa kati ya Askari Polisi na Wananchi wa Kijiji cha Ilula Kilolo Mkoani Iringa watu 18 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na tukio hilo. Vurugu hizo zimeibuka February 24 mwaka huu baada ya mwanamke mmoja kudaiwa kuuawa na askari Mkoani Iringa wakiwa doria kwa lengo la kuwakamata watu wanaokunywa pombe kabla ya muda huo kufika. Wakati Askari watano wakiwa wamejeruhiwa kwenye tukio hilo wananchi wawili pia wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali...
SERIKALI imesema inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya Tume Maalum iliyoundwa na Bunge kushughulikia mgogoro kati ya Wakulima na wafugaji. Aidha, imewataka Wafugaji kuacha Mila na Desturi zilizopitwa na wakati za kufuga mifugo mingi pasipokuwa na tija, wakati maisha yao yakiendelea kuwa duni. Akizungumza Mkoani Mbeya Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA amesema kutoelewa kwa makundi hayo mawili kumesababisha uvunjifu wa amani mara kwa...
MBUNGE wa Bariadi Magharibi kupitia chama cha Mapinduzi -CCM, Andrew Chenge amepandishwa kizimbani kwa madai ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi, jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo. Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungu hivyo vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni pamoja na alipokuwa Mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo kuelekea Lusaka Zambia kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Edgar Chagwa Lungu wa Nchi hiyo. Viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi ikiwemo suala la reli ya Tanzania na Zambia Railway Authority (TAZARA), inayounganisha Tanzania na Zambia. Hivi karibuni Reli ya TAZARA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitajika kujadiliwa kwa kina na viongozi...
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya amesema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja. Amesema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi, zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na...
KAMISHINA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SULEIMAN KOVA ametoa agizo kuchunguza tuhuma za askari wake wanaodaiwa kugawana fedha shilingi milioni Nane ambazo zilikuwa Mali za Akina Mama Wajasiriamali waliojiunga kwenye vikoba. KOVA ameeleza hayo jijini Dar es salaam na kusema kuwa tuhuma hizo amezesikia lakini hawezi kumhukumu mtu hivyo ametoa agizo kuwa uchunguzi ufanyike. Amebainisha kuwa endapo uchunguzi utafanyika na kubaini kuwa askari au mtu yoyote amehusika kuchukua fedha hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni...
MTU mmoja Mkazi wa Dar e salaam, ambaye hujishughulisha na uokotaji wa makopo ya plastiki amenusurika kifo kutokana na kipigo cha wananchi baada ya kuvunja vioo vya nyuma vya magari mawili ya wafanyakazi wa bima ya AAR yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ofisi hizo. Kijana huyo aliyekuwa na jeraha upande wa nyuma wa kichwa chake kikivuja Damu nyingi amejitambulisha kwa jina Amir Ismail na kuiambia EFM kuwa kuna vijana sita wamemvamia na kumpora fedha zake shilingi elf 60 alizokuwa nazo. Ismail...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE amewaasa wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini kusoma kwa bidii masomo yote hususani ya sayansi ili kuinua kiwango cha elimu na kuliletea Taifa maendeleo. Rais KIKWETE ametoa wito huo leo wakati akipokea rasmi vitabu milioni mbili na laki tano vya sayansi na hisabati katika shule ya sekondari ya MTAKUJA BEACH Kunduchi jijini Dar es salaam kutoka kwa serikali ya marekani kupitia shirika la msaada la-USAID- kwa lengo la...
KUNA taarifa kuwa mtu mmoja amefariki dunia baada ya kile kinachosemekana kuwa ameuawa na Askari Polisi katika kata ya Ilula, Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo lililotokea tukio hilo, polisi walikuwa kwenye msako wa vilabu vya pombe za kienyeji ambako mtu huyo ambaye jina lake bado halijajulikana inasemekana alikuwa anakunywa pombe hizo. Hata hivyo bado Efm inaendelea kulifuatilia tukio hilo, ili kujua chanzo cha tukio, na juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi mkoani Iringa zinaendelea...