Local News

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA AFYA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYOKWENYE HATARI KUAMBUKIZWA VVU
Local News

SERIKALI imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoa elimu kwa makundi ya watu wanaotumia dawa za kulevya na wale wanaojihusisha na biashara ya ngono katika maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.Akizungumza kwa Niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta MOHAMED ALLY MOHAMED wakati wa kutambulisha matokeo ya tafiti za watu walio katika...

Like
235
0
Tuesday, 24 February 2015
ASILIMIA 11.7 HAWANA AJIRA TANZANIA
Local News

NAIBU Waziri wa kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, amesema kuwa hali ya ukosefu wa ajira nchini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi uliofanyika mwaka 2006, jumla ya watu waliokuwa hawana kazi hapa nchini ni asilimia 11.7. Ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa Semina ya vijana Mkoa wa Lindi, na kusema kuwa utafiti huo umeonyesha kuwa takribani asilimia 13.4 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 wa Tanzania hawana kazi kabisa. Mheshimiwa Makongoro Mahanga, ameeleeza...

Like
330
0
Tuesday, 24 February 2015
MECK SADIQ AMTAKA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI KUSIMAMIA KATIBA YA NCHI
Local News

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam SAID MECK SADIQ amemtaka mkuu wa wilaya ya Kinondoni PAUL MAKONDA kusimamia vyema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Mheshimiwa SADIKI ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati akimuapisha rasmi mkuu wa wilaya hiyo ambapo amesema kuwa kusimamia ipasavyo katiba ya nchi ni suala muhimu katika kuhakikisha usawa unapatikana kwa kila mtu. Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa...

Like
292
0
Monday, 23 February 2015
WATANO MBARONI KWA UCHOCHEZI WA VURUGU SAKATA LA JKT
Local News

JESHI la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata vijana wapatao wa tano wanao jiita viongozi wa umoja wa kikundi cha wahitimu wa mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa JKT kwa makosa ya uchochezi na mikusanyiko isiyo ya halali. Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishna wa polisi kanda hiyo suleman kova ambapo amesema kuwa lengo la kikundi cha wahitimu hao kufanya mikusanyiko hiyo nikutaka kuandamana kwenda Ikulu kuonana na Rais Dkta JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa madai...

Like
273
0
Monday, 23 February 2015
TANZANIA INAUNGA MKONO KWA DHATI UMOJA WA AFRIKA NA USHIRIKIANO WA EAC
Local News

Tanzania inaunga  mkono kwa dhati Ushirikiano  wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki -EAC. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita Rais  Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti...

Like
331
0
Monday, 23 February 2015
WAZIRI WA MAMBO YA KIGENI WA UJERUMANI AMEIONYA URUSI DHIDI YA UCHOCHEZI MGOGORO WA UKRAINE
Local News

WAZIRI wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameionya Urusi dhidi ya kuchochea zaidi mgogoro wa Ukraine, akisema mashambulizi ya waasi kwenye mji wa Mariupol yatakuwa ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya amani yalioungwa mkono na jamii ya kimataifa. Katika mahojiano na gazeti linalosomwa na watu wengi zaidi nchini Ujerumani la Bild, toleo la leo Jumatatu, Steinmeier ambaye yuko nchini Kenya akikamilisha ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika, amesema hatua yoyote ya kusonga mbele kwenye mji huo itakuwa...

Like
250
0
Monday, 23 February 2015
WAKULIMA MBEYA WAKABIDHIWA MASHINE ZA KUPANDIA MPUNGA KUKUZA KILIMO
Local News

WAKULIMA Wilayani Ileje Mkoani Mbeya wamepokea Mashine Sita za kupandia Mpunga zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 60 kwa ajili ya kuwezesha Kulima kwa kutumia Teknolojia bora ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Akikabidhi Mashine hizo kwa baadhi ya Vikundi vya wakulima katibu tawala FRANSIS MBEGILE amewataka wakulima hao kuzitumia vizuri na kuzitunza kwani watapata maelekezo ya namna ya kuzitumia Kwa upande wake Kaimu afisa Kilimo mkoani humo HERMAN NJEJE amesema hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni utekelezaji wa mpango...

Like
790
0
Monday, 23 February 2015
ESCROW: BARAZA LA MAADILI KUWAHOJI VIGOGO LEO
Local News

VIGOGO wanaodaiwa kuhusika katika Akaunti ya Tegeta ESCROW leo waananza kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma. Habari za kuaminika zimeeleza kuwa vikao vya Baraza hilo ambavyo vitawahoji viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Mameya vitaanza leo na vitadumu kwa wiki tatu. Hata hivyo macho na Masikio ya Watanzania wengi yapo kwa Vigogo wanaotajwa kupata mgawo wa fedha za ESCROW kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd, JAMES...

Like
309
0
Monday, 23 February 2015
WAZIRI WA MAMBO YA NCHI ZA NJE WA UJERUMANI AWASILI DRC
Local News

WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani FRANK-WALTER STEINMEIER amewasili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku nne barani Afrika. Kabla ya ziara hiyo kuanza,Mwanasiasa huyo kutoka Chama Cha Social Democratic amesema, uhusiano wa siku za mbele pamoja na Bara la Afrika amesema utatuwama katika juhudi za kuepusha Mizozo,Ushirikiano katika masuala jumla na Ushirikiano wa kiuchumi. Mbali na Jamhuri Kidemokrasia ya Kongo,Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amepanga kuzitembelea pia...

Like
209
0
Thursday, 19 February 2015
HALI YA SOKO LA BUGURUNI NI TETE
Local News

HALI ya Miundombinu katika Soko la Buguruni jijini Dar es salaam imeendelea kuwa mbaya kutokana na mahitaji ya Wananchi kuongezeka pasipo Soko kupanuliwa. EFM imefika katika soko hilo na kujionea mrundikano wa bidhaa na msongamano wa watu katika soko hilo na kulifanya lionekane kuelemewa kutokana na wafanyabiashara wengine kuuza bidhaa...

Like
219
0
Thursday, 19 February 2015
SERIKALI IMETAKIWA KUTOA RATIBA SAHIHI YA MFUMO WA UANDIKISHAJI WA BVR
Local News

 MTANDAO wa Asasi za Kiraia wa kuangalia Chaguzi Tanzania -TACCEO unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa ratiba sahihi ya jinsi zoezi la Uandikishaji wa wapiga Kura kwa Mfumo wa BVR litakaloendeshwa nchi nzima linatarajiwa kukamilika lini ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Mtandao huo MARTINA KABISAMA amesema kuwa mtandao huo ambao unatarajia kutuma waangalizi Zaidi ya 100 nchi nzima kwa...

Like
328
0
Thursday, 19 February 2015