Local News

WATUMAIJI WA TEKNOLOJIA YA INTERNET WATAKIWA KUITUMIA HUDUMA HIYO KUONGEZA MAARIFA
Local News

WATUMIAJI wa teknolojia ya interneti nchini wametakiwa kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa mbalimbali za maarifa na zenye  mwelekeo wa kuleta maendeleo badala ya kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa zisizo na faida na zenye mwelekeo wa kupotosha kizazi cha sasa kimaadili. Wito huu umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, katika siku ya matumizi ya interneti duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote ambako amesema kuwa Vodacom kama kampuni ya mawasiliano siku zote itakuwa mstari wa...

Like
237
0
Tuesday, 10 February 2015
GHOROFA LATEKETEA KWA MOTO DAR
Local News

WATANZANIA wametakiwa kutii sheria na kukaa pembeni ya Barabara pindi wasikiapo ving’ola vya hatari ili kurahisisha shughuli za uokoaji wa maisha ya watu na mali. Hayo yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha zima moto kanda maalum ya Dar es salaam Esward Ikonko alipokuwa Katika ajali ya moto iliyotokea leo eneo la Kariakoo na mnazi mmoja katika mtaa Jamhuri jijini Dar es salaam ambapo amesema moja ya changamoto inayosababisha magari ya zima moto kuchelewa katika eneo latukio ni msongamano wa watu....

Like
341
0
Tuesday, 10 February 2015
HOFU YA KUPIMA AFYA YAONGEZA IDADI YA VIFO VITOKANAVYO NA SARATANI
Local News

IMEELEZWA kuwa wanawake wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa ugonjwa wa Saratani kutokana na uoga wa kupima afya zao mara kwa mara. Akizindua upimaji wa Saratani Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma FATMA ALY amesema Wanawake wamekuwa wakiishi kwa hofu kuogopa kupima afya zao wakihofia kupokea majibu ambayo si mazuri. Amesema Saratani inatibika kama watawahi kabla haijazidi hivyo amewataka wajijengee tabia ya kupima afya mara kwa mara.  ...

Like
267
0
Tuesday, 10 February 2015
MIILI YA WATU SITA WALIOPOTEZA MAISHA KUZIKWA LEO DAR
Local News

MIILI ya watu Sita wa Familia moja walioteketea kwa moto inatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Airwing jijini Dar es salaam. Hata hivyo bado chanzo cha moto huo hakijajulikana huku baadhi ya watu wakidai huenda moto huo umesababishwa na Petrol. Moto huo umetokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika Mtaa wa Kipunguni A Kipawa jijini Dar es salaam....

Like
361
0
Tuesday, 10 February 2015
TGNP YAFANYA MAFUNZO KUELIMISHA WAZEE WA KIMILA
Local News

MTANDAO wa kijinsia Tanzania TGNP umefanya mafunzo ya kuelimisha Wazee wa kimila katika Mikoa ya Mara, Shinyanga, Pwani, Dar es salaam, Mbeya na Morogoro lengo likiwa ni kuwapa Ujuzi wazee hao ili waweze kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. Akizungumza na EFM Afisa mawasiliano kutoka Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP MERKIZEDECK KAROLI amesema kuwa kupitia Semina hiyo itawawezesha wazee hao kujua endapo katika maeneo wanayoishi kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutoa...

Like
237
0
Monday, 09 February 2015
SERIKALI KUWEKA SERA MOJA YA MALEZI, MAENDELEO NA MAKUZI YA MTOTO
Local News

SERIKALI inatarajia kuweka sera ya aina moja inayounganisha sera zote nchini zinazomuhusu mtoto ijulikanayo kama Sera ya malezi, maendeleo na makuzi ya mtoto. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa utafiti wa elimu ya awali kwa watoto uliofanywa na chuo kikuu cha Aga Khan, Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo na malezi ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto BENEDICT MISSANA amesema kuwa mpaka sasa serikali imeshafungua vyuo 6 vya kufundishia elimu...

Like
353
0
Monday, 09 February 2015
WANANCHI WAISHAURI SERIKALI KUFANYIA KAZI RIPOTI YA KAMATI TEULE YA YA BUNGE KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI
Local News

KUFATIA Kamati Teule ya Bunge Kuwasilisha Ripoti ya Uchunguzi juu ya namna ya kushughulikia migogoro ya ardhi iliopo baina ya Wakulima,Wafugaji na Wawekezaji iliyofatiwa na hoja mbali mbali za Wabunge, baadhi ya Wananchi wameitaka Serikali kuharakisha kuifanyia kazi ripoti hiyo huku wakishauri kutafuta maeneo maalumu katika mapori kwa ajili ya wafugaji ili kunusuru maisha. Wakizungumza na EFM jijini Dar es salaam kwa nyakati tofauti Wananchi hao  wamesema ripoti imepitia changamoto nyingi zilizopo baina ya wakulima,Wafugaji na Wawekezaji...

Like
360
0
Monday, 09 February 2015
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA DARESALAAM KUFUATIA VIFO VYA WATU SITA KWA AJALI YA MOTO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa moto usiku wa kuamkia Jumamosi, Januari 7, mwaka huu, katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. Katika salamu zake, Rais Kikwete amevielezea vifo hivyo kuwa ni vya kusikitisha na kuhuzunisha sana. KATIKA hatua nyingine, Rais...

Like
532
0
Monday, 09 February 2015
KAMATI TEULE YA BUNGE YAITAKA SERIAKALI KUBORESHA NA KUIMALISHA MABARAZA YA ARDHI
Local News

KATIKA kupambana na migogoro ya Ardhi kati ya Wakulima,Wafugaji na Wawekezaji Kamati teule ya Bunge imeitaka serikali kufanya maboresho na kuimarisha  Mabaraza ya Ardhi ili kuwe na wataalam wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya usuluhishi wa migogoro hiyo. Mapendekezo hayo yametolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Mjumbe wa Kamati teule ya bunge alipokuwa akisoma ripoti ya kamati hiyo iliyoundwa kuchunguza na kutafuta njia  za kutatua migogoro hiyo CHRISTOPHER OLE SENDEKA ambapo ameitaka serikali iimarishe mabaraza hayo katika ngazi ya vijiji,...

Like
275
0
Friday, 06 February 2015
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA WILAYA YA TEMEKE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Sophia Mjema kufuatia vifo vya wanafunzi wawili wa Darasa la Nne waliofariki dunia asubuhi ya tarehe 3Mwezi huu,  katika Shule ya Msingi Unity iliyoko Mbagala, Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya gari aina ya RAV 4 kugonga ukuta wa darasa walilokuwemo wanafunzi hao ambapo wanafunzi wengine watatu walijeruhiwa. Rais Kikwete amewataka...

Like
301
0
Friday, 06 February 2015
SERIKALI IMEKIFUNGIA KIWANJA CHA TWIGA CEMENT KILICHOPO WAZO HILL
Local News

SERIKALI imekifungia Kiwanda cha TWIGA Cement kilichopo Wazo hill jijini dare s salaam baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wanaoishi eneo hilo kuvuta hewa chafu inayotoka katika kiwanda hicho na kukitaka kulipa faini ya shilingi milioni 50. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare s salaam Mwanasheria wa mazingira wa NEMC amesema kuwa kumekuwa na malamiko ya muda mrefu na hivyo Serikali wameutaka uongozi wa kiwanda hicho cha Twiga Cement kukifunga ili kuweza kurekebisha mazingira ya watu...

Like
430
0
Friday, 06 February 2015