Local News

WATU MILIONI TISA HUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UGONJWA WA SARATANI KILA MWAKA
Local News

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema takribani watu Milioni Tisa wanakufa kila mwaka kutokana na kuugua ugonjwa wa Saratani. Kauli hiyo imetolewa na Waziri huyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa February 04 kila mwaka Duniani kote. Ametaja kauli Mbiu ya mwaka huu kuwa ni UDHIBITI WA SARATANI UPO NDANI YA UWEZO WETU. Amebainisha kuwa pamoja na idadi ya watu wanaokufa na ugonjwa...

Like
324
0
Wednesday, 04 February 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUANZISHWA KWA MFUKO WA KUJITEGEMEA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuweka mikakati bora itakayowezesha kuanzishwa kwa mfuko wa kujitegemea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kuboresha tume ya kupambana na kudhibiti Ukimwi –TACAIDS- ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo na kuliletea Taifa maendeleo.   Akitoa taarifa za utekelezaji wa kamati ya masuala ya Ukimwi leo Bungeni mjini Dodoma mwenyekiti wa Kamati hiyo LEDIANA MNG’ONG’O amesema kuwa endapo mfuko huo utaanzishwa utaisaidia nchi kwa kiasi kikubwa katika kupambana na ugonjwa huo pasipo...

Like
233
0
Tuesday, 03 February 2015
AU YATOA HESHIMA ZA PEKEE KWA BABA WA TAIFA MWL. JK NYERERE
Local News

UMOJA wa Nchi Huru za Afrika –AU, umetoa heshima pekee kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kumuenzi kwa kuamua kuwa moja ya majengo yake muhimu katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, litapewa jina la Mwalimu Julius Nyerere. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anapewa heshima hiyo kubwa kwa mchango wake katika ukombozi wa Bara la Afrika na kuliondoa Bara hilo katika ukoloni. Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama (Peace and Security Council)...

Like
380
0
Tuesday, 03 February 2015
CHAMA CHA ACT KIMETANGAZA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA
Local News

BAADA ya hivi karibuni kujitokeza kwa  migogoro baina ya viongozi wa Chama cha Alliance for Change –ACT,  Chama hicho kimeamua kufanya marekebisho ya katiba ya chama  ili kukinusuru na migogoro ya namna hiyo. Akizungumza na EFM Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama SAMSONI MWIGAMBA amesema kuwa Marekebisho hayo yatasaidia kusuruhisha  migogoro inayojitokeza kwa baadhi ya viongozi wanaotumiwa kukivuruga  chama. Amebainisha kuwa katiba mpya imerekebisha mapungufu ya katiba ya awali ambayo ilikuwa haina kamati ya nidhamu na maadili...

Like
383
0
Tuesday, 03 February 2015
RAIS WA UJERUMANI AWASILI NCHINI
Local News

RAIS wa Ujerumani JOACHIM GAUCK na msafara wake amewasili nchini . Mara baada ya kuwasili akiwa ameambatana na mkewe Bibi SCHADT  amelakiwa na Makamu wa Rais Dokta  MOHAMED GHARIB BILALI pamoja  na burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea. Rais huyo  ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia  mwaliko kutoka kwa Rais JAKAYA KIKWETE leo amepokelewa katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo Rais huyo akiwa na mwenyeji wake, JAKAYA KIKWETE...

Like
266
0
Tuesday, 03 February 2015
TRA YAWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA BIASHARA ZA MAGENDO
Local News

MAMLAKA ya mapato Tanzania –TRA, imewataka wananchi kujiepusha na biashara za magendo kwani adhabu zinazotolewa kwa wahusika wanaokamatwa na na biashara hizo ni kali na zinarudisha nyuma maendeleo yao Taifa. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano wa TRA Richard Kayombo na kuongeza kuwa ni wakati sasa wananchi wanapaswa kuinua uchumi wa nchi yao kwa kulipa kodi. Kayombo ameongeza kuwa TRA imejipanga kikamilifu kwani kipo kikosi kinachoitwa fast Team ambacho kipo mahususi kwa ajili...

Like
279
0
Monday, 02 February 2015
AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI ITAKAYOGHARIMU SHILINGI MILIONI MIA TISA
Local News

KAMPUNI ya simu za Airtel, leo imezindua promosheni kabambe itakayogharimu shilingi milioni mia tisa ijulikanayo kama airtel yatosha zaidi ,itakayomuwezesha mteja wake kijishindia gari aina ya Toyota IST. Akiongea wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa masoko ya airtel, Levi Nyakundi amesema promosheni hiyo ni nafasi ya pekee kwa wateja wao wanaojiunga na vifurushi vya airtel yatosha zaidi vya siku,wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana na pesa wanazozitumia, lengo likiwa ni kuhakikisha wanatoa huduma na...

Like
601
0
Monday, 02 February 2015
KAMATI YA TANZANIA KWANZA NJE YA BUNGE MAALUM LA KATIBA IMEWATAKA WANANCHI WAISOME NA KUILEWA KATIBA
Local News

KAMATI ya Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum la Katiba imewataka Watanzania kutokubali kutafasiriwa katiba pendekezwa na Wanasiasa au kikundi chocchote na badala yake waisome na kuijua ikiwa ni pamoja na kufuatilia matangazo ambayo Serikali inayatangaza. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Kwanza AGUSTINO MATEFU amesema kuwa kuna baadhi ya kikundi cha watu wachache ambacho kimevaa uhusika kwa ajili ya kuwataka waislam wasipigie kura katiba pendekezwa kwa kuwa hakuna kipengele cha Mahakama...

Like
270
0
Monday, 02 February 2015
ZITTO AMTAKA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KUJIUZULU
Local News

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE amemtaka waziri wa maliasili na Utalii ambaye pia ni mbunge wa Singida mheshimiwa LAZARO NYALANDU kujiuzuru endapo atashindwa kutekeleza agizo la utoaji wa tangazo katika gazeti la serikali juu ya tozo na mapato yatokanayo na wageni wanaolala katika hoteli za kitalii zinazozunguka hifadhi za Taifa hadi ifikapo leo jioni. Mheshimiwa ZITTO ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa mikakati mbalimbali zilizotolewa na kamati ya Ardhi, maliasili na...

Like
273
0
Monday, 02 February 2015
WAKAZI WA LINDI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KIJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Local News

WAKAZI  wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Jerry Silaa  wakati akiongea kwenye kilele cha sherehe za kutimiza miaka 38 ya chama hicho  mkoani Lindi zilizofanyika katika tawi la  Mnazi Mmoja lililopo kata ya Mingoyo wilaya ya  Lindi mjini. Silaa mbaye pia ni Mstahiki...

Like
366
0
Monday, 02 February 2015
KISWAHILI KUTUMIKA KULETA HAKI NA USAWA KATIKA NGAZI ZOTE ZA SERIKALI
Local News

SERIKALI imesema imedhamiria kuweka mikakati madhubuti itakayowezesha lugha ya Kiswahili kutumika katika ngazi zote nchini ikiwemo utoaji wa hukumu katika mahakama zote  ili kuleta haki na usawa kwa wananchi kupitia lugha hiyo. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria mheshimiwa UMMY MWALIMU C wakati akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na mbunge wa viti maalumu mheshimiwa SABRINA SUNGURA ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali ya kuhakikisha lugha ya Kiswahili inatumika na kuleta manufaa kwa watu wote....

Like
301
0
Monday, 02 February 2015