Local News

NJIA KUU YA RELI INAYOUNGANISHA TANZANIA NA ZAMBIA YAFUNGWA
Local News

Njia kuu ya reli inayoiunganisha Zambia na Tanzania imefungwa, baada ya wafanyakazi wake kugoma wakidai malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano ya nyuma. Kampuni inayosimamia njia TAZARA, ambayo anamilikiwa na Serikali ya Tanzania na Zambia, na imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kwa zaidi ya Muongo mmoja, treni zote zimesimamishwa kwa muda usiojulikana kuanzia January 12 mwaka huu....

Like
344
0
Wednesday, 14 January 2015
CCM YAFANYA KIKAO ZANZIBAR LEO
Local News

JANUARY 13 MWAKA huu Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa  Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE imefanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar. Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na, Sakata la Akaunti ya tegeta Escrow, Waliopewa  adhabu kwa kukiuka maadili ya chama, Soko la Mahindi na Ratiba ya vikao vya...

Like
300
0
Wednesday, 14 January 2015
SERIKALI IMEOMBWA KUONDOA CHANGAMOTO KATIKA SHULE MAALUM ZA WATOTO WENYE ULEMAVU
Local News

SERIKALI imeombwa kuhakikisha kuwa shule Maalum za watoto wenye Ulemavu zinapatiwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuondoa changamoto zinazozikabili shule hizo.  Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko shule ambayo ina wanafunzi wenye Ulemavu na wasio na Ulemavu ....

Like
258
0
Wednesday, 14 January 2015
KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA YABAINI UFISADI HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
Local News

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa-LAAC imebaini kuwepo kwa Ufisadi na uzembe katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.  Hali hiyo imesababisha wajumbe kuwaomba Watendaji akiwemo Meya wa jiji hilo DIDAS MASABURI kupisha Kamati hiyo kwa muda ili kujadili taarifa zao.  Hatua hiyo imetokana na baadhi Wajumbe wa Kamatihiyo kuhoji ni kwa nini jiji wamekataa kumpatia Simon Group Akaunt kwa ajili ya kufanya malipo ya Hisa zilizokuwa zikiuzwa na jiji la Dar es salaam....

Like
336
0
Wednesday, 14 January 2015
VIJANA KILIMANJARO WAZIOMBA HALMASHAURI KUHAMASISHA VIJANA KUANZISHA SACCOSS
Local News

VIJANA WA MKOANI Kilimanjaro wameziomba Halmashauri zao kuhamasisha vijana kuanzisha SACCOSS za Wilaya zitakazowawezesha vijana kuwekeza na kuwasaidia kuomba mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana utakaopitishiwa katika SACCOSS hizo ili waweze kujiajiri. Hayo yamesemwa na Vijana wakati wa kufunga Semina ya Uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuiomba Wizara yenye dhamana na vijana kujitolea kutoa Elimu kwa vijana mara kwa mara itakayowawezesha vijana kujitambaua na kuwajengea...

Like
410
0
Tuesday, 13 January 2015
WIMBI LA VIJANA WASIOKUWA NA AJIRA NI TATIZO LA DUNIA NZIMA
Local News

WIMBI la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo duniani kote na Serikali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na kulitatua. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa –UNDP, ALVARO...

Like
327
0
Tuesday, 13 January 2015
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA AFARIKI BAADA YA KUNYWESHWA POMBE
Local News

MTOTO mwenye umri wa mwaka Mmoja JAPHET MTUI mkazi wa Kijiji cha Msule Wilayani Ikungi amekufa kutokana kunyweshwa Pombe. Kamanda wa Polisi Mkoani Singida THOBIASI SEDOYEKA amethibitisha kutokea kwa kifo hicho baada ya Mtoto huyo kupewa Pombe ya Kienyeji aina ya Mtukuru akiwa na Mama yake MAGDALENA...

Like
457
0
Tuesday, 13 January 2015
MKUU WA WILAYA YA MANYALA ATOA MIEZI MINNE KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Local News

 MKUU WA MKOA wa Manyara JOEL BENDERA  ametoa miezi Minne kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondary. BENDERA ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya siku moja kukagua Ujenzi wa Maabara katika Wilaya za Simanjiro na Kiteto na kuzungumza na Wenyeviti wa Vijiji,Madiwani na Watumishi wa Wilaya hizo....

Like
403
0
Tuesday, 13 January 2015
KOVA: ONGEZEKO LA AJALI DAR ZINASABABISHWA NA PIKIPIKI
Local News

ongezeko la ajali za barabarani jiji la Dar es salaam  zinasababishwa na madereva wa Pikipiki kwa kutozingatia Sheria na taratibu za usalama barabarani. Kamanda KOVA amesema ongezeko hilo la ajali ni kithibitisho kuwa madereva hao hawana mafunzo ya uendeshaji wa vyombo...

Like
252
0
Monday, 12 January 2015
DK. SHEIN AONGOZA MAELFU YA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI
Local News

 RAIS WA ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta ALLY MOHAMMED SHEIN leo amewaongoza maelfu ya Watanzania na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE katika Maadhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katika Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar Dokta SHEIN amezungumzia mafanikio yaliyopatikana nchini humo katika kipindi cha miaka minne ikiwa ni pamoja na Ukuaji wa Uchumi, Ongezeko la Wataalamu wa Afya na kukua kwa kiwango...

Like
251
0
Monday, 12 January 2015
MKUU WA WILAYA YA MASASI ATOA ONYO KWA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU
Local News

MKUU wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara FARIDA MGOMI, ametoa onyo kwa viongozi wa vijiji vya Mwongozo, Mdenga na Nangoo vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi, ambao wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu miundombinu katika mradi wa maji wa mamlaka ya maji safi na Mazingira Masasi-Nachingwea -MANAWASA. MGOMI ametoa onyo hilo baada ya Mamlaka hiyo kutangaza kusudio la kusitisha huduma ya Maji kwenye Vijiji hivyo vitatu kutokana na wananchi wake kuhujumu Miundombinu ya maji na kusababisha huduma...

Like
483
0
Monday, 12 January 2015