VIJANA HUSUSANI Waendesha Bodaboda wametakiwa kushiriki katika masuala ya kupiga vita uhalifu nchini ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa Amani pamoja na kuendeleza jitihada za kuliletea Taifa maendeleo. Ushauri huo umetolewa na SIMBA MOHAMED SIMBA ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania BONIVENTURE MWALONGO wakati akifungua Maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Chama cha Waendesha boda oda wa Magomeni-Kagera jijini Dar es...
MAMA WAJAWAZITO Wilayani Kahama Shinyanga wameaswa kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani na kutumia dawa za kienyeji wakati wa kujifungua. Badala yake wamehimizwa kujifungulia hospitali ili kupata msaada wa Madaktari kuhakikisha Usalama wao. Ushauri huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kahama Dokta JOSEPH NGOWI wakati wa uzinduzi wa filamu iitwayo FESTULA inayoelezea athari za ugonjwa...
WATANZANIA wameshauriwa kupiga vita matumizi ya bidhaa Feki na badala yake watumie bidhaa zenye ubora ili kudhibiti wasambazaji wa bidhaa hizo nchini. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Afisa mawasiliano wa Shirika la viwango Tanzania –TBS ROIDA ANDUSAMILE wakati akizungumza na EFM kuhusu mikakati ya kuhakikisha masoko yote nchini yanakuwa na bidhaa bora....
TUME YA TAIFA ya Uchaguzi imetangaza Matokeo ya Zoezi la Uandikishaji wa Wapigakura katika Daftari la Kudumu kwa mfumo wa BIOMETRIC VOTERS REGISTRATION-BVR katika majimbo matatu ya Bunju,Katavi na Kilombelo ambapo zoezi limeonyesha Mafanikio makubwa. Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji DAMIAN LUBUVA amesema zoezi hilo limefanikiwa kufikia malengo ambapo katika jimbo la Bunju wameandikishwa watu 21,323 kati ya 35,486, Jimbo la Katavi ni 11,210 kati ya 11394 na Kilombero ni...
MWENYEKITI wa Mtaa wa Kimara Baruti Jijini Dar es salaam kupitia Tiketi ya Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo- CHADEMA FLOMENCE KINYONGA amewataka wananchi wa Mtaa huo kuwa na Utaratibu wa kusafisha Mitaa kila ifikapo mwisho wa Mwezi. Akizungumza na EFM amesema kuwa ili kutimiza ahadi walizojiwekea katika kujiletea Maendeleo wananchi hao hawana budi kushirikiana na Viongozi wa Mtaa huo katika kusafisha mitaa ikiwa ni pamoja na kuzibua mitaro ambayo imejaa Michanga na Maji hasa katika kipindi cha...
LICHA ya Serikali kufanya juhudi mbalimbali kukabiliana na Unyanyasaji wa Watu wenye Ulemavu wa ngozi-ALBINO nchini tatizo hilo limeendelea kujitokeza na kutishia amani yao. Hali hiyo imejitokeza jijini Mwanza baada ya mtoto mwenye Ulemavu wa Ngozi PENDO SHIBINDE kutekwa nyumbani kwao katika kijiji cha Ndabi Wilaya ya Kwimba jijini Mwanza. Akithibitisha kupotea kwa mtoto huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza VALENTINO MLOWOLA amesema kila mtu anajukumu la kumlinda mtoto na kuachana na imani potofu ambazo zinapelekea watoto hao kudhuriwa,...
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam SAID MECKY SADIQ amesema mwaka jana ulikuwa na mafanikio yaliyotekelezwa kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Maabara. Amesema katika mwaka huo mkoa umejipanga kutoa Elimu na hamasa kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga...
NAIBU Waziri wa Maendelea ya Jamii,Jinsia na Watoto Dokta PINDI CHANA ameitaka Jamii kutunza Mazingira ili kulinda Afya ya Mtoto. Akizungumza na Waandishi wa Habari Dokta PINDI ameeleza kuwa mtoto anatakiwa kupata haki za Msingi ikiwemo ya kulindwa,kutunzwa,kuendelezwa,kuishi,kushirikishwa pamoja na kutobaguliwa. Amebainisha kuwa Ulinzi wa Mtoto unahitajika dhidi ya Ukatili kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya Sheria ili kumsaidia kupata mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na Mavazi,Malazi na...
JESHI POLISI Kanda Maalum jijini Dar es Slaam limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 95 wanaotuhumiwa kwa Makosa mbalimbali yakiwamo ya Uhalifu wa kutumia silaha. Kamshina wa Polisi Kanda hiyo SULEIMAN KOVA amesema watuhumiwa wote wamekamatwa katika kipindi cha Sikukuu ya Krismas kufuatia Oparesheni iliyofanywa na jeshi hilo. Amebainisha kuwa mwaka 2014 unaisha vizuri kwa wakazi wa jiji kusherekea vyema Sikukuu za mwisho wa mwaka bila uvunjifu wa...
LEO USIKU Watanzania wataungana na wenzao katika baadhi ya maeneo Ulimwenguni kuukaribisha mwaka mpya 2015. Ni dhahiri kwamba litakuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwani kuuona mwaka mpya si jambo dogo bali ni kwa kudra za Mwezi Mungu. Katika kuukaribisha mwaka mpya ambapo kawaida shughuli katika maeneo mbalimbali huanza muda wa Saa 6 usiku watu hukusanyika na kufanya sherehe. Wapo wanaokwenda kwenye nyumba za Ibada,wanaokwenda katika Viwanja mbalimbali ukiwamo uwanja wa Taifa kufanya Ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka...
WENYEVITI wa Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuwatendea Haki Wananchi ambao wamewachagua na kuwaepuka baadhi ya Watendaji ambao wamekuwa wakiwarubuni na kushindwa kuwatendea Haki Wananchi. Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa Kata ya Sandali Wilayani Temeke jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDALLAH BULEMBO amesema imebainika kuwa watendaji wengi wamekuwa ni kikwazo kwa Wenyeviti hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi kwa...