Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege na kumwamuru kurejesha Dola za Marekani 42,543 (Sh68,068,800). Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando alimtia hatiani Ekelege baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa utetezi uliotolewa na mshtakiwa. Hakimu Mmbando alisema katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulithibitisha mashtaka yote yanayomkabili Ekelege...
Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu. Wanawake zaidi ya 30...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia ameridhishwa na tathimini ya mkutano wa mashauriaono wa awamu ya kwanza wa Mradi wa Mabasi yaendeyo Haraka (DART) uliofanyika hivi karibuni ukiwemo pia na wa kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na wamiliki wa usafirishaji jijini Dar es...
Timu Ya Arsenal ya nchini Uingereza jana usiku iliweza kufuzu kucheza mashindano ya kombe la UEFA kwa msimu wa 17 mfululizo kwa timu za Ulaya baada ya kuichapa timu ya Besiktas ya Uturuki kwa bao 1-0. Katika mchezo wa awali wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana na hivyo kusubiri uamuzi wa nani atavuka katika mechi ya pili ya marudiano ambayo ilichezwa jana usiku. Alikuwa ni mchezaji mpya wa timu ya Arsenal aliyejiunga msumu huu akitokea timu...
Kundi la muziki la Mapacha wawili wa Ki Nigeria P Square kuanzia Alhamisi ya leo na ndani ya masaa 48 wanategemewa kuachia nyimbo tatu mfululizo moja kati ya hizo ikiwa collabo kali ya kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa meneja wa wasanii hao Jude Okoye ambaye pia ni kaka yao wasanii hao wataachia nyimbo hizo kupitia record lebo yao ya Square Music. Wasanii hao ambao wamejijengea sifa kubwa ulimwenguni kote kwa sasa wanatamba na kibao cha “Taste The Money”....
Baada ya kipigo cha magoli 4-0 dhidi ya timu yake, Meneja wa klabu ya Man Utd Van Gaal amelia na kikosi chake ambacho jana usiku kiliendelea kupata matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu mpya wa soka huko nchini Uingereza Agosti 16. Kocha Van Gaal amesema kikosi chake hakikucheza vizuri wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Milton Keynes Dons ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuwatupa nje ya michuano hiyo...
Israel na wapiganaji wa Ki Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda mrefu katika ukanda wa Gaza. Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza kutekelezwa jana kuanzia majira ya saa moja usiku. Hamas wamesema mpango huo unawakilisha “ushindi wa upinzani wao”.Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza....
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kukutana na viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ili kuzungumzia mchakato wa Katiba wakati wowote wiki hii. Katika mkutano huo, ambao unasubiriwa kwa hamu, Rais Kikwete atakutaka na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF. Aprili 16, mwaka huu wajumbe wa Ukawa na baadhi kutoka Kundi la 201, walisusia vikao vya Bunge hilo wakitaka msingi wa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba...
Kitendo cha Bunge Maalumu la Katiba kukusanya maoni ya makundi na wananchi mbalimbali, kimepokewa kwa hisia tofauti, baadhi ya wasomi wakisema ni kinyume cha sheria na kuonyesha kutapatapa huku Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akisema linafanya kazi ambayo tayari tume yake ilishaifanya. Hata hivyo, Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad amesema litaendelea kupokea mapendekezo kutoka kwa watu na makundi mbalimbali hadi hapo litakapohitimisha kazi yake. Kwa muda sasa, wawakilishi wa taasisi mbalimbali...
Rais JAKAYA KIKWETE ametoa wiki moja kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, kuwapatia viwanja vya kujenga nyumba wahanga wa mafuriko ya kiasi cha miaka minne iliyopita mjini Kilosa.Rais KIKWETE ametoa agizo hilo mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kilosa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kilosa baada ya kutembelea Wilaya hiyo kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.Agizo hilo limekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wahanga hao kwa njia ya maneno na mabango baada ya kuwa wameahidiwa...
Haya ni maeneo ya Mikocheni Tanesco ambapo huwaga hivi kama siku itanyesha mvua kubwa…husababisha foleni kubwa ya magari kwa wafanyakazi waendao makazini nyakati za...