Mahakama Kuu ya Tanzania, imetoa wito kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kufika mahakamani hapo leo, kesi ya Kikatiba kuhusu madaraka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itakapotajwa. Zitto akishirikiana na mwanasheria wake, Fatma Karume alifungua kesi hiyo iliyosajiliwa kwa namba 01/2019, akiiomba Mahakama kutoa tafsiri ya Ibara ya 143(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alifungua kesi hiyo akipinga hatua...
Serikali ya imeahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto mkoani Njombe. Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wamepatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo. Akizungumza Bungeni leo, Waziri wa Mambo ya Ndani nchi, Kangi Lugola amesema tayari wameshabaini baadhi ya wale waliohusika na mauaji hayo na hatua kali zitachukuliwa. “Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina…n tayari...
Wananchi Mjini Njombe wameiomba Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usalama kudhibiti vitendo vya mauaji ya watoto wenye umri kati ya miaka 4-9 ambavyo vinatajwa kuongezeka tangu mwezi disemba mwaka jana na kuendelea kutishia hali ya usalama mjini humo. Wananchi hao wametoa rai hiyo baada ya mwili wa mtoto mwingine wa jinsia ya kiume kuokotwa kando ya msitu wa asili wa Nundu ulioko nje kidogo ya mji wa Njombe. “Ni kweli kuna mtoto mwingine amekutwa amefariki pale msituni, tulipofika pale...
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati kupitia programu ya ‘Peoples Empowerment Foundation’ chini ya Kampuni ya Camal Group amefanikisha kuwakabidhi viungo bandia walemavu 10 wa miguu kutoka wilaya tofauti za mkoa huo ambao walikosa msaada na kulazimika kuishi wakiwa na upungufu wa viungo vya mwili. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ofisi ya Mbunge huyo ambapo amesema kuwa Mh. Ritta Kabati alifanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Iringa na kubaini uwepo wa walemavu zaidi ya 110...
Vijana wengi wamekuwa na tamaa ya kupata fedha nyingi na kwa haraka zaidi hali ambayo inawapelekea kufanya matendo yanayohatarisha maisha ya watu wengine ikiwemo kujichukulia hatua mkononi kupoteza maisha ya watu wengine. Vijana wengi wamekuwa wakipita njia za mkato kusaka pesa hali ambayo inawagharimu sana, kufuatia tabia hiyo kijana mmoja ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani ‘House boy’ inasemekana ameyachukua maisha ya mwajiri wake ambaye alikuwa ni mstaafu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Tunsume Sakajinga ambaye ameuawa vibaya...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayojali wananchi wake hivyo kuanzia sasa amesitisha zoezi zima la kubomoa makazi ya watu yaliyojengwa bila kufuata mpango mji. Rais ameelekeza kuwa nyumba hizo zisibomolewe kwa kuwa hayakuwa makosa yao kujenga katika maeneo hayo na kuelekeza kuwa watu wote wasio na hati miliki za ardhi kufanyiwa urasimishaji wa makazi yao. ”Serikali ya awamu ya tano kuanzia sasa haitabomoa tena nyumba...
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameruhusu kuanza mchakato wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Ruhuji mkoani Njombe utakaozalisha megawati 358, kwa lengo la kuwa na hazina kubwa ya nishati ya umeme ambao utauzwa katika nchi jirani ikiwemo Zambia, Kenya na Uganda. Ameyasema wakati akiwasha umeme katika vijiji vinne vinavyopitiwa na ujenzi wa mradi wa umeme wa Makambako -Songea ikiwa na pamoja...
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amejivunia kujiandikisha kwenye Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP), ambao amedai umemuongezea thamani kama msanii. Akizungumza na Dar24 katika mahojiano maalum, Mngereza ameeleza kuwa akiwa kama msanii wa sanaa ya ufundi pamoja na muziki, mbali na kuwa Katibu Mtendaji, ameamua kuchangamkia fursa ya TACIP kwani inaongeza thamani ya msanii na kumfanya aheshimike kwa kumtambulisha. “Mimi ninazungumza kama Katibu Mtendaji, lakini nikiuvua ukatibu...
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba kupitia tiketi ya CUF, Katani S Katani amelalamikia hatua ya serikali kulipa kiasi kidogo cha fedha kwenye vyama ushirika ambavyo viko kwenye jimbo lake linalokadiriwa kuwa zaidi ya vyama 128. Kwa mujibu wa Mbunge Katani, mpaka sasa hakuna mkulima ambaye anamiliki magunia zaidi ya 16 ambaye ameshalipwa kutokana na utaratibu wa serikali, kulipa wenye idadi ya magunia 15. “Kwa mfano mimi kwangu, kumefanyika uhakiki lakini fedha iliyolipwa haizidi bilioni 6, na hii fedha imelipwa kwa...
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amezitahadharisha Kaya ambazo bado hazijaweza kurudi katika makazi yao kutokana na nyumba zao kuezuliwa na upepo na mvua kali na kuwafanya kuishi kwa mikusanyiko katika majengo ya serikali juu ya usafi wa mazingira ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchache wa vyoo katika maeneo hayo. Amesema hayo baada ya kuwatembelea waathirika wa mvua na upepo mkali waliohifadhiwa katika kituo cha kilimo kilichopo katika kijiji cha Kipeta, Kata ya Kipeta Wilayani Sumbawanga...
Polisi wanawake mkoa wa Arusha kupitia Mtandao wao (TPF NET) wamepongezwa kutokana na utendaji bora wa kazi zao za kila siku hasa katika suala zima la kudumisha nidhamu na kufanya kazi kwa uaminifu. Pongezi hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati wa kuhitimisha maazimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili yaliyoanza rasmi Novemba, 25 mwaka huu. Amesem kuwa askari wa kike wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi lakini...