Local News

JWTZ YAKABIDHIWA JENGO LA KUFUNDISHIA WATAALAMU WA SAYANSI YA TIBA
Local News

JESHI la Wananchi wa Tanzania-JWTZ- leo limekabidhiwa Jengo litakalotumika kwa ajili ya Chuo cha Kijeshi cha kufundishia wataalamu wa Sayansi ya Tiba kwa kiwango cha Shahada lililojengwa kwa msaada na Serikali ya Ujerumani ili kuongeza idadi ya Madaktari Nchini. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Ulinzi Dokta Hussen Mwinyi amesema awali Jeshi hilo lilikuwa na chuo kinachofundisha matabibu kwa kiwango cha Cheti na Stashahada hivyo chuo hicho kitaweza kutoa elimu hiyo kwa kiwango cha kinachotakiwa. Kwa upande wake Balozi...

Like
332
0
Tuesday, 29 September 2015
VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUJIKITA KATIKA SHUGHULI ZA UJASILIAMALI
Local News

VIJANA  nchini wametakiwa kutojihusisha na makundi hatari bila kuwa na kazi yoyote  na badala yake wahakikishe wanajikita zaidi katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali ili waondokane na umasikini. Kauli hiyo imetolewa na Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi-CCM-Silvestry Koka  alipokuwa akizungumza na vijana wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa tawi jipya la CCM jimboni hapo. Koka amesema kuwa baadhi ya vijana wanalalamika kutokuwa na ajira tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa husababishwa na wao kwa kutotaka...

Like
218
0
Tuesday, 29 September 2015
VIPIMO VYA MARADHI YA MOYO KUFANYIKA BURE MUHIMBILI LEO
Local News

LEO ni Siku ya Afya ya Moyo Duniani ambapo kila ifikapo September 29  ya kila mwaka Dunia nzima huadhimisha siku hiyo inayolenga kuijulisha jamii baadhi ya masuala mbalimbali yanayo husu afya ya Moyo. Katika mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es salaam daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini, TULIZO SHEMU SANGA amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi leo katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kupima afya hiyo bure. Aidha DKT TULIZO ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti...

Like
370
0
Tuesday, 29 September 2015
WAMILIKI WA VITALU VYA MBOGAMBOGA WAMETAKIWA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA KIAFYA
Local News

WAMILIKI wa vitalu vya mbogamboga wametakiwa kufuata kanuni na taratibu za kiafya zilizowekwa na serikali pindi wanapolima kilimo hicho ili kulinda afya za watumiaji.   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Ubungo NHC, AMANI SIZYA ameiambia efm radio kuwa asilimia kubwa ya wakulima wa mbogamboga wanatumia maji yanayopita kwenye mitaro ya maji taka kumwagilia mboga hizo, na kusababisha kutokuwa salama kiafya kwa...

Like
253
0
Monday, 28 September 2015
DK BILAL AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Muhammed Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani aliyefariki Septemba 24 katika hospitali ya Andraprash Apolo Nchini India kutokana na ugonjwa wa Saratani ya Kongosho.   Tukio hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali kutoka Tanzania bara na visiwani...

Like
268
0
Monday, 28 September 2015
TANZANIA YAAHIDI KUCHUKUA HATUA 5 ZA KUTETEA NA KUENDELEZA HAKI ZA WANAWAKE
Local News

TANZANIA imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, kwa kufuta sheria kandamizi kwa wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia.   Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kufuta na kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni vinavyoendeleza ubaguzi kwa wanawake ikiwemo Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.   Msimamo huo umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano...

Like
233
0
Monday, 28 September 2015
WITO UMETOLEWA KWA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA TAASISI KUSAIDIA JAMII
Local News

WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga utamaduni  wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Wito huo umetolewa mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Profesa Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Amesema chuo cha CBE mwaka huu kimetimiza miaka 50 tangu kuanzishwa...

Like
444
0
Monday, 28 September 2015
TANZANIA YAUNGA MKONO MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO
Local News

TANZANIA imeunga mkono Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDG’s), ikisisitiza kuwa malengo hayo ni silaha ya kutosha ya kufuta umasikini duniani katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030. Aidha imesema kuwa endapo dunia itafanikiwa kutekeleza malengo hayo ya SDG’s katika miaka 15 ijayo kama ilivyopangwa ni dhahiri kuwa ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa mahali pazuri zaidi. Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipohutubia Baraza Kuu...

Like
268
0
Monday, 28 September 2015
MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI WAAGWA LEO
Local News

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na mgombea Ubunge wa jimbo la Ulanga mashariki kupitia-CCM– marehemu Celina Kombani  kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Bunge kupitia kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano zinaeleza kuwa baada ya Zoezi hilo kukamilika mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu mkoani Morogoro ambapo utapokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa na maafisa kutoka serikalini....

Like
336
0
Monday, 28 September 2015
EFM MUZIKI MNENE BAR KWA BAR KIBAHA 2015
Entertanment

93.7 EFM yajinyakulia ushindi baada ya kuwafunga kibaha veterans mabao mawili kwa moja, katika mchezo uliochezwa jumamosi ya juzi katika uwanja wa Tamco kibaha. Mechi hiyo ni baadhi ya mechi zinazoendelea baina ya EFM na timu mbalimbali za wasikilizaji wake, Kupitia kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar .   Burudani haikuishia hapo, baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani ya kibaha kontena. Ilikuwa ni bandika bandua ya ngoma kali kutoka kwa Rdj’s wa 93.7 EFM na shamra shamra kutoka...

Like
761
0
Monday, 28 September 2015
PROGRAMU ENDELEVU YAANZISHWA KUTATUA MATATIZO YA UZAZI
Local News

KATIKA Kuhakikisha suala zima la uzazi salama linazingatiwa nchini ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto ,Muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania umeanzisha programu endelevu ya  kushirikisha wananchi katika kupaza sauti zao kuhusu matatizo mbalimbali ya afya  yanayowakumba kipindi cha uzazi na jinsi gani serikali na Asasi mbalimbali zisizo za Kiserikali zinaweza kutatua changamoto hizo. Mratibu Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania ROSE MLAY  amewaambia wandishi wa habari leo,  kuwa Taasisi imekuwa...

Like
259
0
Friday, 25 September 2015