Local News

WATU 9 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA NYUMBA KUTEKETEA KWA MOTO
Local News

WATU tisa wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi iliyoko maeneo ya Buguruni Malapa kuteketea  kwa moto na kusababisha vifo vyao papo hapo Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa mtaa wa Malapa KARIMU MAHMUDU amesema kuwa moto huo ulianza majira ya saa tisa ndani ya nyumba hiyo na kusababisha vifo vya watu tisa ikiwemo watoto wanne ambao walijulikana kwa majina ya AHMEDI, ABDULLAH, AISHA, ASHRAFU, Mama wa watoto hao aliyejulikana kwa jina...

Like
520
0
Thursday, 27 August 2015
MASHEKHE NA WALIMU WA MADRASA WAMETAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPENDA AMANI
Local News

MASHEKHE na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwahamasisha Wananchi kupenda Amani ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.   Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifungua mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.   Katika mkutano huo Sheikh Omary amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu wa Amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini na hata ndani ya Nyumba...

Like
425
0
Thursday, 27 August 2015
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MAKUZI NA MALEZI YA WATOTO
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza makuzi na malezi ya watoto katika familia ili kujenga Taifa lenye watu wenye maadili. Akifungua kongamano la wadau wa haki za watoto Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dokta Pindi Chana amesema Serikali inashughulikia marekebisho ya kisera na mipango zilizopo ili kukuza upatikanaji wa haki za watoto nchini.  Kongamano la wadau wa malezi na makuzi ya familia limefanyika muda ambao mpango wa utekelezaji wa malengo ya milenia unafikia ukingoni,...

Like
284
0
Thursday, 27 August 2015
UMABWILA: VYAMA VYA BODABODA HAVIFUNGAMANI NA SIASA
Local News

UMOJA wa madereva wa bodaboda wilaya ya IIala (UMABWILA) wamesema kuwa vyama vya bodaboda havifungamani na siasa na kila mwanachama anahaki ya kupenda na kushabikia chama chochote cha siasa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Makamu mwenyekiti  wa Umoja huo, BASHIRU KASHAIJA amesema kuwa watashirikiana na chama ambacho kimesaidia kuwezesha bodaboda kuwa chombo rasmi cha...

Like
253
0
Wednesday, 26 August 2015
BAWACHA KUFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA WANAWAKE KESHO
Local News

BARAZA la Wanawake la chama cha Demokrasia na Maendeleo-BAWACHA- linatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni ya Wanawake wa chama hicho kupitia kongamano linanalotarajia kufanyika  kesho Agosti 27 jijini Dar es salaam.   Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza hilo Halima Mdee amesema kongamano hilo linalengo la kuwaunganisha wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 na hatimae kufikia lengo la la idadi ya asilimia hamsini kwa hamsini hasa ikizingatiwa kua wanawake ndio...

Like
243
0
Wednesday, 26 August 2015
WADAU WAKUTANA KUTAHMINI NA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA YA AFYA
Local News

KATIKA kuboresha huduma za afya nchini Wadau mbali mbali wa maswala ya afya wamekutana kutathmini  utoaji huduma na kutazama namna ya kuboresha utoaji huduma za afya kwa Watanzania.   Wadau hao wamekutana katika kongamano la tano la kitaifa la kuboresha huduma za afya  lililoanza leo jijini Dar es salaam linalotarajia kuchukua siku mbili likiwa limeaambatana na maonyesho ya vifaa na huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi za serikali na zile za binafsi zinazojishughulisha na maswala ya afya...

Like
209
0
Wednesday, 26 August 2015
MUZIKI MNENE BAR KWA BAR 2015 BANGO
Local News

Bwana E Mr Jimmy Jiam wa EFM akipozi na mshindi wa EFM Muziki Mnene Bango eneo la Sinza, jijini Dar Es Salaam. Mshindi huyo alionekana akiwa anasikiliza 93.7 EFM na pia alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya kazi. Mshindi mwingine wa EFM Muziki Mnene Bango akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa zawadi na bwana E wa EFM. Dada huyo alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya biashara eneo la Magomeni, jijini Dar Es Salaam. Bwana...

Like
370
0
Wednesday, 26 August 2015
UVUVI HARAMU KWA NJIA YA SUMU HATARI KWA MAISHA YA WATU UKEREWE
Local News

IMEELEZWA kuwa uvuvi haramu kwa njia ya sumu wilayani Ukerewe unahatarisha maisha ya watu kwa kuugua ugonjwa wa ini na figo huku wengine wakipoteza maisha kwa ugonjwa huo.   Wakiongea na Efm baadhi ya wakazi  wa ukerewe   walioathirika na ulaji wa  samaki waliovuliwa kwa sumu wamesema uvuvi haramu ndio chanzo cha wao kuugua ugonjwa wa ini na figo na kufanya familia zao kuishi kwa taabu.   Kwa upande wake daktari kutoka katika hospitari ya rufaa Bugando jijini mwanza  Mathayo James...

Like
256
0
Wednesday, 26 August 2015
MARUFUKU KWA WAGOMBEA WA URAIS KUFANYA KAMPENI KWENYE MIKUSANYIKO ISIYO RASMI – NEC
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imevitaka vyama vya siasa kuzingatia ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais kwa kufanya mikutano kwa tarehe, sehemu na mahala kwa mujibu wa ratiba. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na NEC, vyama vyote vya siasa vinatakiwa vizingatie ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais na viache kufanya mikusanyiko ya aina yoyote ambayo haipo katika ratiba ya kampeni hizo. Chama kitakachokiuka maelekezo hayo kitakuwa kimekiuka kipengele cha maadili ambacho kinaelekeza kuwa ni wajibu wa vyama vya...

Like
229
0
Wednesday, 26 August 2015
LOWASSA ATEMBELEA KARIAKOO, POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAFUASI WA UKAWA
Local News

JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Ilala limelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi-UKAWA– kutokana na mgombea wa nafasi ya Urais kupitia umoja huo Edward Lowasa kufika eneo la kariakoo kwa lengo la kutaka kuwaona wafanyabiashara wa soko hilo. Lowasa amefanya ziara leo ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo Tandale, Tandika na Kariakoo ili kutathimini hali ya maisha ya wananchi. Kamanda wa polisi Ilala Lucas...

Like
301
0
Tuesday, 25 August 2015
RAIS KIKWETE ASISITIZA WAJIBU WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA CHANGAMOTO NA MAPUNGUFU KATIKA UJENZI WA BARABARA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mikoa na Serikali za Mitaa kusimamia changamoto na mapungufu katika usimamizi wa ujenzi wa barabara nchini ili kuleta manufaa kwa wananchi. Ameongeza kuwa ni wajibu wa ngazi hizo za uongozi kuhakikisha kuwa kazi za barabara hazifanyiki kwa viwango duni na kukomesha uwepo wa upendeleo katika uteuzi wa wakandarasi wa kazi za ujenzi wa barabara kinyume cha Sheria ya Manunuzi. Rais Kikwete ameyasema hayo wakati...

Like
213
0
Tuesday, 25 August 2015