Local News

JESHI LA POLISI LIMESHAURIWA KUZISOMA NA KUZIELEWA SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI
Local News

JESHI la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza ili kuliepushia lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani.   Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini katika Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar....

Like
198
0
Thursday, 30 July 2015
LOWASSA KUOMBA RIDHAA YA KUWANIA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA LEO
Local News

MWANACHAMA mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, Edward Lowasa  asubuhi hii anachukua fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa kiongozi huyo kuchukua fomu kwa ajili ya kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1995 kisha Juni mwaka huu akiwa ndani ya chama cha Mapinduzi-CCM, kabla jina lake halijakatwa na vikao vya juu vya chama hivho Julai 12 mwaka...

Like
315
0
Thursday, 30 July 2015
WATANZANIA WAMETAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA
Local News

WATANZANIA wametakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vitawafikisha pabaya na kurudisha maendeleo yao nyuma hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi  mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini-Takukuru, Dokta Edward Hosea katika mafunzo ya maafisa wa Taasisi hiyo juu ya  utakatishaji fedha na kupata taarifa na mlolongo wa uhalifu kwa kutumia sheria za Tanzania. Dokta Hosea amesema mafunzo hayo yatawasaidia maafisa hao kupata na kuelewa vithibitisho vya uhalifu vinavyogusa fedha na mali...

Like
208
0
Wednesday, 29 July 2015
JUMA SIMBA: CCM HAITISHWI WALA KUZUIA MTU KUHAMA
Local News

CHAMA cha Mapinduzi –CCM, kimesema kwamba ni chama kikubwa na hakitishwi wala kuzuia mtu yeyote kukihama huku kikizungumzia uwepo wa wanachama ambao waliwahi kukihama na kurejea.   Taarifa hizo zimetolewa leo na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam Juma Simba, ambaye amezungumzia pia kuhusu tetesi kuwa wafuasi wa Lowassa ambao ni wengi ndani ya chama hicho wanasemekana kuwa wapo mbioni kumfuata kada huyo, amesisitiza wao hawazuii mtu yeyote kuhama chama hicho....

Like
251
0
Wednesday, 29 July 2015
WATANZANIA MILIONI 10 HUTUMIA MTANDAO KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI
Local News

IMEELEZWA kuwa watanzania takribani milion kumi wanatumia huduma za mtandao katika shughuli zao mbalimbali. Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa mkongo wa taifa  naibu Katibu mkuu kutoka Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia CELINA LYIMO amesema kuwa mbali na kuwa idadi  hiyo wizara hiyo inakusudia kupunguza gharama  za watumiaji  wa mitandao ili watanzania wengi waweze kutumia  huduma...

Like
195
0
Wednesday, 29 July 2015
WANANCHI WATOA MAONI TOFAUTI KUFUATIA MAAMUZI YA LOWASSA
Local News

BAADA  ya jana kutangaza rasmi kuachana na chama cha Mapinduzi –CCM kwa aliyekuwa kada na mwanachama wa muda mrefu wa chama hicho, Edward Lowasa, na kuunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, baadhi ya Wananchi Jijini Dar es salaam wamekuwa na maoni mbalimbali kufuatia uamuzi huo.   Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema uamuzi aliochukua Lowasa ni mzuri na wanauunga mkono kwa kuwa maamuzi hayo yatasaidia kukuza siasa ya vyama vingi na hivyo kukuza demokrasia.  ...

Like
189
0
Wednesday, 29 July 2015
WIZARA YA NISHATI NA MADINI IMEANDAA MUFUNZO KUEPUSHA MIGONGANO KANDA YA KASKAZINI
Local News

IMEELEZWA kuwa ili kuondokana na migongano kwenye usimamizi wa sekta ya madini Kanda ya Kaskazini, Wizara ya Nishati na Madini imeandaa mafunzo kuhusu sekta ya madini yatakayoshirikisha viongozi mbalimbali katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro yatakayofanyika Agosti 12 mwaka huu. Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Arusha Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro Fatuma Kyando amesema kuwa mafunzo hayo yatashirikisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, maafisa tawala wa wilaya, watendaji na wawakilishi kutoka Mamlaka ya...

Like
276
0
Tuesday, 28 July 2015
TAASISI ZA KIFEDHA ZIMESHAURIWA KUTUMIA NAFASI ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA NISHATI
Local News

TAASISI za Kifedha, Binafsi na Washirika wa  Maendeleo nchini wameshauriwa kuzitumia nafasi zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kwa kushirikiana na  serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini –REA–  ili kujiletea maendeleo.   Hayo yamebainishwa  na washirika wa Maendeleo katika tasnia ya nishati, kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujadili namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuhakikisha vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme.   Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu...

Like
334
0
Tuesday, 28 July 2015
VYAMA 21 VYA SIASA VIMESAINI MAADILI YA UCHAGUZI MKUU 2015
Local News

VYAMA vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo. Maadili hayo yanayohusisha Serikali,Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC- na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu dokta Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam,...

Like
247
0
Tuesday, 28 July 2015
WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA AMPONGEZA RAIS KIKWETE
Local News

WAZIRI Mkuu wa Australia Tony Abbot amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba ya Tanzania. Waziri Mkuu Abbot ametoa pongezi hizo mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Kikwete namna nchi hizo mbili zinavyoweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii. Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa...

Like
439
0
Tuesday, 28 July 2015
UNITED KUMNUNUA KIPA WA ARGENTINA
Local News

Manchester United mnamo Jumapili walithibitisha kumnunua kipa wa Argentina Sergio Romero kwa mkataba wa miaka mitatu. Mlindalango huyo wa miaka 28 atajaza pengo lililoachwa na Victor Valdes, aliyetimuliwa Old Trafford baad aya kudaiwa kukataa kucheza na timu ya akiba ya United. “Kuchezea timu kubwa zaidi duniani kwangu ni kutimia kwa ndoto,” alisema Romero kupitia taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo. “Louis van Gaal ni meneja mzuri sana na nasubiri sana kuanza kibarua hiki mpya na cha kusisimua kwenye maisha yangu...

Like
303
0
Tuesday, 28 July 2015