Mahakama nchini Misri imewahukumu kwenda jela watu sita kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua raia wa Ufaransa katika kituo cha Polisi walikokuwa wamewekwa kizuizini. Eric Lang mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa mwalimu wa lugha aliwekwa kizuizini nchini Misri miaka mitatu iliyopita. Kwa mjibu wa upande wa mashitaka ni kwamba Lang aligombana na wenzake wakiwa rumande ambapo walianza kumshambulia hadi kumsababishia kifo chake. Hata hivyo Polisi wa Misri wamekuwa wakituhumiwa kuhusiaka na mauaji ya mwanafunzi raia wa Italia Giulio Regeni...
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi ikiwemo ya Dadaab nchini humo. Awali siku ya Ijumaa iliyopita Serikali ya Kenya ilisema kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha. Aidha imetoa tangazo kama hilo mapema, lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga kambi zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi Laki...
MEYA wa jimbo aliyeongoza kampeni kali ya urais nchini Ufilipino, Rodrigo “Digong” Duterte ameshinda uchaguzi huo kufuatia kujitoa kwa wapinzani wake. Licha ya kwamba matokeo rasmi hayajatangazwa, mpinani wake mkuu Mar Roxas amekiri kushindwa baada ya kura zinazohesabiwa kudhihirisha Duterte anaongoza kwa kura nyingi. Mgombea huyo aliye na umri wa miaka 71 alizusha mzozo wakati wa kampeni kwa matamshi yake makali....
Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania. Alifikishwa mahakamani Jumatatu asubuhi mjini Dar es Salaam. Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia. Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa...
Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu. Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo. Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi...
SPIKA wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani Paul Ryan amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho. Mfanyabiashara huyo bilionea anaonekana dhahiri kushinda katika mbio za uteuzi kukiwakilisha chama hicho lakini Ryan amesema kuwa kabla hakuweza kuidhinisha suala hilo Trump alipaswa kuwaonyesha watu kuwa anaheshimu taratibu za Republican na angepata kura za Wamarekani wengi zaidi. Mapema Marais wa zamani wa Marekani George W Bush na baba yake George Bush waliweka wazi kuwa...
AFISA mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema mashambulizi ya ndege za angani katika kambi ya wakimbizi,yanahofiwa kuwaua zaidi ya watu 30. Mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika umoja wa mataifa, Stephen O’Brien ametaka pawepo uchunguzi juu ya shambulizi hilo lililotokea katika jimbo la Idlib, karibu na mpaka wa Uturuki. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond amemtuhumu Rais wa Syria Bashar Al-Assad kwa kuonyesha dharau juu ya juhudi za kimataifa kumaliza mapigano nchini...
SERIKALI ya Uganda imepiga marufuku urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja yanayopinga uchaguzi wa rais Yoweri Museveni. Usalama katika mji mkuu wa Uganda- Kampala umeimarishwa kabla ya maandamano yalioitishwa na chama cha Forum for Democratic Change (FDC). Vyombo vya habari nchini Uganda vimetakiwa kutofanya matangazo ya moja kwa moja na wanachama wa upinzani ambao wanapinga kuchaguliwa kwa rais...
IMEBAINIKA kwamba Mwanamke amepatikana akiwa hai kwenye vifusi ikiwa ni siku sita baada ya jengo kuporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi. Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, amesema kuwa maafisa wa uokoaji bado wanajaribu kutengeneza njia ya kumtoa kwenye vifusi hivyo. Hata hivyo, mwanamke huyo amekuwa akiwasiliana na matabibu ambao wanasubiri kumpatia matibabu punde...
MWANASIASA mashuhuri wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ametoa tangazo hilo kupitia mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadhaa vya upinzani nchini humo umeamua kumuidhinisha Bwana Katumbi kuwa mgombea wao wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi...
WABUNGE wa Bunge la Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni kwaajili ya kuwahutubia. Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani. Hata hivyo ujio wake uliwakera wabunge wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) ambao walipiga mayowe na kumtupia matusi Rais...