WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akihutubia kongamano la biashara baina ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Bw. Troung Tan Sang. Akizungumza kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema mbali ya mabadiliko ya...
MGOMBEA Urais wa Marekani anayeongoza katika chama cha Republican Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi. Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi. Baada ya kupata ushindi huo, Trump amesema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican ingawa Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye amepata ushindi katika jimbo dogo la...
POLISI waliopo Mashariki mwa Pakistan wamewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kupanga ndoa kati ya mvulana mwenye umri wa miaka 14 na msichana mwenye umri wa miaka 10 pekee suala ambalo ni kinyume cha sheria. Imeelezwa kwamba ndoa hiyo ilikuwa imepangwa kama njia ya kusuluhisha mzozo baina ya familia hizo mbili. Tabia ya kuendeleza ndoa za mapema pamoja na kutatua mizozo ya nyumbani kupitia ndoa, ni hatia kwa mujibu wa sheria za...
MAAFISA wa polisi nchini Brazil wamemkamata aliyekuwa rais wa nchi hiyo Luiz Inacio da Silva ikiwa ni miongoni mwa mpango wa kuchunguza ufisadi dhidi yake. Mali zote zinazohusishwa naye ikiwemo nyumba yake na taasisi ya yake ya Lula zimevamiwa na Maafisa hao ili kuzuia shughuli yoyote ya uhujumu kufanyika. Da Silva atahojiwa kuhusu madai kwamba amefaidika na mpango wa rushwa uliokuwa ukiendeshwa na kampuni...
KAMISHENI ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha makubaliano kati ya Umoja huo na Ugiriki juu ya ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Azerbaijan unaolenga kupunguza utegemezi wa nishati kwa Urusi. Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 878, litasafirisha mita bilioni 10 za ujazo za gesi kwa mwaka kutoka Azerbaijan hadi Italia kupitia Ugiriki, Albania na Bahari ya Adriatiki. Awamu ya kwanza ya gesi hiyo inatazamiwa kuwasili barani Ulaya mwaka 2020 ambapo Ugiriki itafaidika kwa mafao ya kodi kwa miaka...
MGOMBEA Urais Donald Trump ameshambuliwa na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono. Bwana Trump anayeongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz. Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si...
KOREA KASKAZINI imerusha makombora ya masafa mafupi, baharini kujibu vikwazo vipya ilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jeshi la Korea Kusini limethibitisha kushuhudia shughuli hiyo na kusema kwamba havikulenga mtu yeyote. Miongoni mwa vikwazo vipya vilivyowekwa na umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo ni pamoja na kuhakikisha mizigo yote inayoingia Korea Kaskazini kutoka nje kuanza...
IKIWA tayari mwelekeo unaonesha kuwa kinyang’anyiro cha kiti cha urais wa Marekni kitakuwa ni kati ya Bi. Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican, wazee na vigogo ndani ya chama cha Republican wamesema kuwa hawapo tayari kumruhusu Trump Agombee Urais. Wakuu hao wa chama cha Republican wamesema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais wao basi kuna uwezekano mkubwa wa chama chao kusambaratika. Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South...
UMOJA wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji unaoendelea kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia, ambako polisi wa Macedonia waliwafyatulia mabomu ya kutoa machozi mamia ya wahamiaji. Msemaji wa halmashauri kuu wa umoja huo Margaritis Schinas, amesema matukio yalioonyeshwa kwenye mpaka huo siyo njia sahihi ya kushughulikia mgogoro huo. Naye Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema matukio hayo yanaonyesha umuhimu wa mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya umoja wa Ulaya wa kujadili mgogoro wa...
IMEELEZWA kuwa aliyekuwa kiongozi wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa dola milioni 29 za kulifadhili kundi la Jihad kabla ya kuuawa mwaka 2011. Kwa mujibu wa wosia wake aliouandika ambao umeonekana leo ameihimiza familia yake kuheshimu wosia wake na kuwashauri watumie mali yake yote kuendeleza kundi la jihad. Mali yake na wasia wake ni miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa leo na maafisa usalama wa Marekani ambao pia wosia huo...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema madai yote ya kuvunja muafaka wa kusitisha mashambulizi nchini Syria yatachunguzwa. Hata hivyo Kerry amesisitiza kwamba Marekani na Urusi wameafikiana kutojadili madai hayo hadharani. Ameongeza kuwa pande hizo zimekubaliana kuhakikisha mashambulizi yanalenga ngome za wapiganaji wa Islamic State na Al-Nusra Front pekee....