ZAIDI ya watu 130 wamefariki dunia baada ya maporomoko ya matope kukiangamiza kijiji kimoja, kando ya mji mkuu wa Guatemala. Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka za nchi hiyo ya Amerika ya Kati, ikiwa ni siku ya tatu tangu janga hilo kutokea, zinasema idadi mpya ya waliopatikana wamekufa imefikia 131, huku wengine 300 wakiwa hawajuilikani walipo. Maporomoko yenye matope mazito yalikifunika kijiji cha El Cambray katika manispaa ya Santa Cantarina Pinula, na kuharibu nyumba 125, usiku wa...
DONALD TRUMP amesema atawafukuza wakimbizi kutoka Syria walioko nchini Marekani iwapo atakuwa rais. Bilionea huyo, ambaye kwa sasa anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican amesema katika mkutano wa kisiasa kuwa akishinda watarudi kwao. Matamshi hayo ni tofauti na aliyoyatoa mapema mwezi huu akihojiwa na Fox News aliposema Marekani inafaa kuwapokea wakimbizi...
MAAFISA wa Afghanistan wanasema kuwa wamedhibiti maeneo muhimu ya mji wa kaskazini wa Kunduz kutoka kwa wapiganaji wa Taliban. Oparesheni iliotekelezwa usiku kucha imesababisha kuchukuliwa kwa maeneo muhimu ya serikali mbali na kusababisha uharibifu mkubwa kwa wapiganaji. Lakini wapiganaji wa Taliban wanasisitiza kuwa wanashikilia maeneo makubwa ya mji...
SERIKALI ya Afrika Kusini imesema italipa fidia kwa familia za wafanyakazi wa mgodini waliouawa wakati wa kuzuka kwa mgogoro wa Marikana mwaka 2012. Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ameeleza kuwa taarifa za kina kuhusu malipo zitatolewa na jopo huru linaloongozwa na jaji. Kwa upande wa familia, wakili wao ameripotiwa kuunga mkono tangazo hilo la...
BENDERA ya Palestina imepeperushwa kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Bendera hiyo ilipandishwa kwenye mlingoti kwenye sherehe iliyohudhuriwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw Abbas amesema ni jambo lisiloeleweka kwamba hadi sasa suala la Palestina kuwa taifa bado...
MSHUKIWA wa kundi la wapiganaji wa kiislamu, anayetuhumiwa kuharibu makavazi ya kihistoria nchini Mali, anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC wakati wowote kuanzia sasa. Anatuhumiwa kuteleza uhalifu wa kivita. Ahmad Al Faqi Al Mahdi, alikabidhiwa kwa mamlaka kuu nchini Niger siku ya Jumamosi ambapo inasemekana aliamrisha au kutekeleza uharibifu katika makavazi ya kale huko...
KIKOSI maalum cha shirika la kujihami la muungano wa mataifa ya Magharibi NATO, kinasemekana kufika mji wa Kunduz nchini Afghanistan. Nia hasa ni kujaribu kuutwaa tena mji huo, ambao kwa sasa uko chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa...
UMOJA wa Afrika umesema mahakama maalumu itaundwa kwa ajili ya kuwashitaki washukiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sudani kusini ambapo imekumbwa na mzozo mkubwa tangu mwaka 2013. Hatua hii inalenga kuunga mkono hatua ya Afrika kushughulikia migogoro yao wenyewe. Uundwaji wa mahakama ni sehemu ya makubaliano ya Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi, Riek Machar yaliyotiwa saini baada ya kuwepo shinikizo kutoka kwa viongozi wa...
WAUZAJI wa mboga mboga na matunda waliopo karibu na soko la Mjini Babati Mkoani Manyara, ambao wanauza bidhaa zao chini wametoa ombi kwa halmashauri ya mji huo kumalizia ujenzi wa soko jipya ili waweze kuhamishia bidhaa zao hapo. Wakizungumza wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye soko jipya, wafanyabiashara hao wamedai wanakuwa na wakati mgumu kwani soko la sasa ni dogo na halitoshelezi mahitaji. Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela, amemweleza kiongozi wa mbio za...
IDADI ya watu waliouwawa katika shambulio la anga kwenye sherehe ya harusi nchini Yemen imefikia watu 131, na kuaminika kuwa shambulio hilo ni baya kuwahi kutokea katika vita nchini Yemen. Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unafanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya waasi nchini Yemen umekanusha kuhusika na shambulio hilo huku msemaji wa muungano huo amesema wanamgambo wa eneo hilo huenda wameshambulia kwa makombora. makombora hayo yaliyorushwa jana...
NCHI ya Urusi imesema kuwa inatafakari uwezekano wake wa kuifuata Marekani ili kuwashambulia kwa ndege wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS). Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ameyasema hayo baada ya kukutana na Rais wa Marekani Barack Obama kwenye maongezi ya nje ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN). Hata hivyo hotuba zilizotolewa na viongozi hao katika mkutano huo, ziliashiria mgawanyiko kuhusu jinsi ya kumaliza vita nchini Syria ambapo Urusi ilisema itakua “kosa kubwa” kutofanya kazi...