Global News

MATEKA 70 WAKOMBOLEWA KWENYE MIKONO YA IS
Global News

WANAJESHI wa Marekani wakishirikiana na wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuwakomboa mateka 70 waliokuwa wakizuiliwa na wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq. Idara ya ulinzi ya Marekani imesema operesheni ya kuwakomboa mateka hao ilitekelezwa baada ya kubainika kwamba walikuwa karibu kuuawa. Lakini mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa kwenye operesheni hiyo amefariki na ndiye mwanajeshi wa kwanza kufariki tangu kuanza kwa operesheni ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya IS mwaka jana.  ...

Like
180
0
Friday, 23 October 2015
ZUMA KUKUTANA NA WADAU WA ELIMU
Global News

RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepangiwa kukutana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo leo kujadili maandamano ya wanafunzi yaliyosababishwa na kuongezwa kwa ada ya masomo. Wanafunzi wamekuwa wakiandamana wiki moja sasa, hasira nyingi zikielekezwa kwa chama tawala African National Congress (ANC). Jana, maelfu ya wanafunzi walikusanyika nje ya makao makuu ya ANC mjini Johannesburg wakitaka elimu itolewe kwa wote bila malipo...

Like
137
0
Friday, 23 October 2015
MIJADALA YA HATUA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YALALAMIKIWA
Global News

MAJADILIANO  kuhusiana  na hatua  zinazoweza  kuchukuliwa kimataifa  kupambana  na  mabadiliko  ya  tabia  nchi  yamelalamikiwa kuwa yanaendelea  kwa  kasi  ndogo  . Mazungumzo  hayo yanayofanyika  mjini  Bonn  yana lengo  la  kupata  msimamo  wa  pamoja  kabla  ya mkutano  wa  mwezi  Desemba  wa  Umoja  wa  Mataifa mjini  Paris  wakati  viongozi  wa  dunia wataamua  kuhusu makubaliano  yatakayofuatwa  kisheria na  kila  taifa duniani  kote. Kundi  la  mataifa  yanayojulikana  kama  G77, ...

Like
125
0
Thursday, 22 October 2015
RAIS ZUMA KUKUTANA NA VIONGOZI NA WANAFUNZI KUJADILI MPANGO WA KUPANDISHA ADA
Global News

RAIS  wa  Afrika  kusini  Jacob Zuma  amesema atakutana  na  viongozi  wa  wanafunzi  na  maafisa  wa vyuo  vikuu  kesho Ijumaa  kujadili  mpango  wa kupandisha  ada  ambao  umezusha  maandamano ya  wiki nzima  katika  taifa  hilo.   Wakosoaji  wanasema  ongezeko   hilo litaleta  athari  kwa wanafunzi Waafrika , ambao  tayari  ni  wachache.   Akizungumza leo, rais Zuma hajaweka wazi  juu  ya  maandamano hayo  hapo  kabla ,  na  jana  wanafunzi  walivamia  viwanja vya  bunge  mjini  Cape...

Like
138
0
Thursday, 22 October 2015
MAREKANI: JOE BIDEN ATANGAZA KUTOWANIA URAIS MWAKA UJAO
Global News

MAKAMU wa Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba hatawania urais mwaka ujao. Ni wazi sasa kuwa Bernie Sanders ndiye mpinzani mkuu wa Mama Hillary Clinton kwa uwaniaji wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, baada ya Makamu wa Rais Joe Biden kutangaza kuwa hatagombea Urais wa Marekani. Akiongea katika mji mkuu wa New York, Bwana Sanders alimpongeza Makamu wa Rais kwa kutoa huduma muhimu kwa jamii kwa muda...

Like
167
0
Thursday, 22 October 2015
MAREKANI YAISHUTUMU URUSI KWA KUMPA MAPOKEZI YA HESHIMA RAIS WA SYRIA
Global News

MAREKANI imeshutumu Urusi kwa kumpa mapokezi ya heshima Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Moscow. Afisa wa wizara ya masuala ya ndani ya Marekani amesema taifa hilo halijashangazwa na ziara hiyo, lakini wasiwasi mkubwa kwa Marekani ni Urusi kuendelea kumsaidia kivita Assad kitendo ambacho inaamini kuwa  litaipa nguvu zaidi serikali ya Assad na hivyo kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Ziara hiyo ya kiongozi wa Syria ilifanyika wiki tatu baada ya Urusi kuanza kushambulia kwa ndege ngome za...

Like
185
0
Thursday, 22 October 2015
CONGO BRAZZAVILLE: POLISI WATUMIA RISASI NA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAANDAMANAJI
Global News

POLISI nchini Congo Brazaville wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji walioitikia mwito wa upinzani wa kuendelea na siku ya pili ya maandamano ya kupinga nia ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wake wa tatu.   Waandamanaji wameweka vizuizi barabarani huku wakipigana na maafisa wa usalama.   Maeneo ya Kusini mwa jiji hilo la Brazzaville ndio lililoathirika zaidi na makabiliano hayo baina ya waandamanaji na...

Like
175
0
Wednesday, 21 October 2015
URUSI NA MAREKANI ZAAFIKIANA KUHUSU NDEGE SYRIA
Global News

URUSI na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria.   Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili.   Urusi ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State –IS, Nna  wiki iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa zimeingia eneo moja la mapigano na zilikuwa karibu sana...

Like
207
0
Wednesday, 21 October 2015
BAN KI-MOON ATARAJIWA KUANZA ZIARA MASHARIKI YA KATI
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ataliarifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo, kuhusu ziara yake ya Mashariki ya Kati, iliyolenga kutuliza ghasia zilizodumu kwa wiki kadhaa sasa.   Ban Ki-Moon alitoa ombi la kuzungumza na baraza hilo haraka kupitia njia ya video, kutokea mji wa Ramallah, uliyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Palestina.   Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya ziara ya kustukiza katika eneo hilo jana, ili kutoa onyo kwa pande mbili...

Like
164
0
Wednesday, 21 October 2015
CANADA: CHAMA CHA UPINZANI CHASHINDA UCHAGUZI MKUU
Global News

CHAMA cha upinzani nchini Canada cha Liberal kimeshinda uchaguzi mkuu na kufikisha kikomo uongozi wa karibu mwongo mmoja wa chama cha Conservative. Chama hicho kinachoegemea siasa za mrengo wa kati, chini ya uongozi wa Justin Trudeau, kilianza kampeni kikishikilia nafasi ya tatu kwa mujibu wa kura za maoni lakini sasa kimeongoza kwa kura. Trudeau, mwenye umri wa miaka 43, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu Pierre Trudeau, amesema raia wa Canada walipigia kura mabadiliko halisi ambapo pia Waziri Mkuu...

Like
133
0
Tuesday, 20 October 2015
MAANDAMANO NA MILIPUKO YATAWALA CONGO BRAZZAVILLE
Global News

Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kutaka kubadilisha katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu. Vyama vya upinzani viliitisha maandamano hayo na inasemekana kuwa wanajaribu kuingia katikati mwa jiji hilo la Brazzaville. Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kabla ya kura ya maoni itakayoamua iwapo katiba ya taifa hilo itabadilishwa au...

Like
151
0
Tuesday, 20 October 2015