Global News

UMOJA WA ULAYA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI
Global News

UMOJA wa Ulaya umesema utaanza kukabiliana na wafanyibiashara wanaowasafirisha wahamiaji kinyume na sheria katika bahari ya Mediterania. Taarifa kutoka Umoja huo zinaeleza kuwa upo uwezekano wa kuanzisha operesheni ambayo itaruhusu majeshi ya nchi wanachama kuingia, kufanya upekuzi na kuzuia boti ambazo zinashukiwa kuhusika katika biashara haramu ya kuwasafirisha wahamiaji kuanzia oktoba saba mwaka huu. Hata hivyo viongozi wa dunia waliopo katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wamezihimiza nchi za Umoja wa Ulaya kuwakaribisha wahamiaji na...

Like
144
0
Tuesday, 29 September 2015
WAFUNGWA WATOROKA GEREZANI AFRIKA YA KATI
Global News

MAMIA ya wafungwa katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha. Hali hiyo imekuja baada ya dereva wa gari ndogo muumini wa dini ya kiislamu kuuawa na kusababisha kuibuka kwa mapigano siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu. Wafuasi wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina Anti-Balaka walishambulia gereza siku ya jumatatu na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na...

Like
239
0
Tuesday, 29 September 2015
17 WAZAMA BAHARINI SYRIA
Global News

KIASI cha raia 17 wa Syria wamezama katika bahari ya Aegean baada ya kuondoka Uturuki wakielekea Ugiriki. Takriban wahamiaji wengine 20 kutoka Syria wameokolewa na maafisa wa Uturuki baada ya boti yao kuzama na Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti hapo jana kuwa miongoni mwa waliokufa maji ni watoto watano. Boti hiyo ilikuwa imewabeba wahamiaji 37 na kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kushughulikia wahamiaji IOM, zaidi ya wahamiaji laki 350,000 wengi wao kutoka Syria wameingia Ugiriki mwaka huu...

Like
228
0
Monday, 28 September 2015
WALINDA AMANI WA AFRIKA KUSINI KUADHIBIWA
Global News

WANAJESHI hamsimi wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) wameagizwa kurejea nyumbani. Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendakazi. Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa Congo. Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini...

Like
206
0
Friday, 25 September 2015
KENYA: MAHAKAMA YASIMAMISHA MGOMO WA WAALIMU
Global News

MAHAKAMA nchini Kenya imesimamisha mgomo wa walimu uliodumu kwa wiki nne na kuwaagiza walimu kurudi kazini mara moja.   Jaji Nelson Abuodha wa mahakama ya kiviwanda na masuala ya wafanyakazi amesimamisha mgomo huo kwa miezi mitatu na kuwataka walimu na serikali kuunda kamati ya kutafuta suluhu katika muda wa mwezi mmoja.   Aidha, ameiagiza Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kutowaadhibu walimu na kuwalipa mishahara yao kikamilifu, pamoja na...

Like
227
0
Friday, 25 September 2015
PAPA FRANCIS ATOA WITO KUONDOLEWA KWA ADHABU YA KIFO
Global News

KIONGOZI  wa  kanisa  Katoliki  Duniani, Papa  Francis  amewaambia wanasiasa  nchini  Marekani  kwamba  wanapaswa kuwaangalia  wahamiaji  kama  watu na  sio  idadi  ya watu.   Katika  hotuba  yake  ya  dakika  50 , kiongozi  huyo  wa kanisa  amegusia  mzozo  wa  wakimbizi  katika  bara  la Ulaya  wakati  akielezea  kuhusu  madhila  ya  mamilioni  ya wahamiaji  kutoka  America  ya  kusini  ambao  wanafasiri kuelekea  kaskazini  kutafuta maisha  bora.   Papa  Francis  ametoa wito  wa ...

Like
151
0
Friday, 25 September 2015
MAAFA MECCA: MFALME AAGIZA KUPITIWA UPYA MASUALA YA HIJA
Global News

MFALME Salman wa Saudi Arabia ametoa agizo la kupitiwa upya kwa masuala ya hija baada ya watu zaidi mia saba kufariki kutokana na msongamano nje ya msikiti wa Macca. Watu wengine mia nane walijeruhiwa katika tukio hilo ambapo inaelezwa kuwa vifo hivyo ni vingi kutokea katika hija kwa takriban miaka ishirini na tano iliyopita. Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za mwisho katika ibada za hija.na  huo ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati...

Like
201
0
Friday, 25 September 2015
RAIS WA BURKINA FASO AREJEA MADARAKANI
Global News

RAIS wa serikali ya mpito ya Burkina Faso aliyekuwa amepinduliwa wiki iliyopita na wanajeshi waasi, Michel Kafando, amesema kwamba sasa amerejea rasmi madarakani. Kauli hiyo ya Kafando inakuja masaa machache baada ya wanajeshi waliofanya mapinduzi hao na wale wanaoitii serikali kusaini makubaliano ya kujiepusha na ghasia katika mji mkuu...

Like
277
0
Wednesday, 23 September 2015
MAHUJAJI KUKUSANYIKA LEO KATIKA MLIMA ARAFA
Global News

MAHUJAJI kutoka duniani kote wameanza kukusanyika leo hii katika mlima wa Arafat nchini Saudi Arabia kwa kisimamo cha siku nzima ambacho ndio kilele cha ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka. Takriban mahujaji milioni 2 wanakusanyika bega kwa bega kwa siku nzima na Wengi wameonekana wakiwa wamenyanyua mikono yao juu huku wakimuomba msamaha Mwenyezi Mungu kwa makosa yao na ya jamaa zao. Siku kama ya leo miaka 1,400 iliyopita, Mtume Muhammad alitoa khutba yake ya mwisho katika mlima huwo wakati wa...

Like
418
0
Wednesday, 23 September 2015
PAPA AWASILI MAREKANI
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani kuanza ziara ambako pia atahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuzungumza katika kikao cha Congress ya Marekani, ambacho kinajumuisha Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti. Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 alipokelewa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Andrews karibu na Washington DC. Awali, katika ziara yake ya siku tatu...

Like
162
0
Wednesday, 23 September 2015
BURKINA FASO: KIONGOZI WA MAPINDUZI ATARAJIWA KUKABIDHI MADARAKA LEO
Global News

KIONGOZI wa mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere hii leo anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa rais aliyempindua, Michel Kafando baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa kikanda. Makubaliano yamepatikana kati ya jenerali huyo na jeshi la nchi yake usiku wa leo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wawakilishi wa pande hizo mbili. Makubaliano hayo yamejengwa juu ya vipengele vitano, ambavyo vinajumuisha kile kinachowataka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais kilichojaribu kufanya mapinduzi –...

Like
164
0
Wednesday, 23 September 2015