Global News

NIGERIA: RAIS WA BUNGE LA SENETI ATINGA KORTINI
Global News

RAIS wa Bunge la Seneti nchini Nigeria, Bukola Saraki leo amefika kortini mjini Abuja ambako anakabiliwa na makosa 13 yanayohusu maadili. Makosa hayo ni pamoja na kuwahadaa wananchi kwa kigezo cha kutangaza mali yake pamoja na kukosa kutangaza mkopo, makosa ambayo ameyakanusha. Kesi dhidi yake inaendeshwa na jopo la mahakama kuhusu maadili na inahusu makosa anayodaiwa kuyatenda alipokuwa gavana wa jimbo la Kwara kati ya mwaka 2003 na...

Like
224
0
Tuesday, 22 September 2015
BURKINA FASO: VIONGOZI WA MAPINDUZI WAKATAA KUSALIMU AMRI
Global News

VIONGOZI wa mapinduzi nchini Burkina Faso wamekataa kutii matakwa ya kusalimu amri na kutishia kupigana vita endapo watashambuliwa. Walinzi wa rais walioongoza mapinduzi walikuwa wamepewa hadi saa nne kwa saa za Afrika kuweka chini silaha na wanajeshi ambao walifika katika mji mkuu Ouagadougou. Hayo yamejiri huku marais wa mataifa ya Afrika Magharibi chini ya muungano wa Ecowas wakikusanyika Abuja, Nigeria kwaajili ya kufahamishwa na Rais wa Senegal Macky Sall kuhusu hatua zilizopigwa katika kutatua mzozo...

Like
257
0
Tuesday, 22 September 2015
SYRIA: MAJESHI YA RAIS ASSAD YAUA RAIA 18
Global News

MASHAMBULIZI makubwa ya mabomu yaliyofanywa na vikosi tiifu kwa rais Assad yameua jumla ya raia 18 katika mji wa Kaskazini mwa Syria wa Allepo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika la haki za binadamu linalofuatilia hali nchini humo,vikosi vya serikali vimefyatua makombora  dhidi ya eneo la Al-Shaar mashariki mwa mji huo Rami Abdel Rahman kiongozi wa shirika la haki za binadamu amesema makombora yamefyatuliwa dhidi ya mkusanyiko wa watu uliokuwa katika eneo hilo na kujeruhi watu kadhaa huku wengine...

Like
221
0
Tuesday, 22 September 2015
MAREKANI: SCOTT WALKER AJIONDOA KINYANG’ANYIRO URAIS REPUBLICAN
Global News

Mgombea wa Urais wa Marekani aliyekuwa akiwania kuteuliwa kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha Republican- Scott Walker amejiondoa katika kinyang’anyiro hicho. Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Winscosin amesema amejiondoa katika kampeini hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donald Trump. Mgombea huyo ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo kiwango chake kilishuka katika kura ya maoni baada ya kufanya vibaya katika midahalo...

Like
208
0
Tuesday, 22 September 2015
BURKINA FASO: KIONGOZI WA MAPINDUZI ATOA MAPENDEKEZO KUENDELEA KUSHIKA DOLA
Global News

JENERALI aliyeongoza mapinduzi ya serikali nchini Burkina Faso wiki iliyopita ametoa mapendekezo yake ya kuendelea kuongoza taifa hilo hadi kukamilika kwa kipindi cha uchaguzi. Mapendekezo hayo yaliwasilishwa na Jenerali Gilbert Diendere kwa wapatanishi kutoka nchi za Afrika Magharibi akiwemo Rais Macky Sall wa Senegal na Rais wa Benin Yayi Boni, katika mji mkuu wa Ouagadougou. Mapinduzi hayo ya serikali yaliyotekelezwa na kikosi cha walinzi wa rais yameshutumiwa vikali, huku Burkina Faso ikiondolewa rasmi kutoka Muungano wa nchi za...

Like
259
0
Monday, 21 September 2015
MALI YA SERIKALI YA ZIMBABWE YAPIGWA MNADA
Global News

IMEBAINIKA kuwa nyumba inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe imeuzwa kwa mwekezaji mmoja wa nchini Afrika kusini kwa kiasi cha dola za kimarekani laki mbili na Elfu themanini kupitia mnada. Mnada huo umefanyika baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye mzozo uliodumu kwa kipindi cha miaka mitano kati yake na shirika la kutetea haki za Waafrika nchini Afrika Kusini. Shirika hilo liliitaka serikali ya Zimbabwe kulipa gharama ya kesi baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye kesi iliyohusu mageuzi ya umiliki wa...

Like
226
0
Monday, 21 September 2015
SHULE ZAANZA KUFUNGWA LEO KENYA
Global News

Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia leo nchini Kenya, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai walimu. Rais Kenyatta ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani ingawa tayari Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa...

Like
408
0
Monday, 21 September 2015
APPLE WAVAMIWA KIMTANDAO
Global News

KAMPUNI ya Apple ya Marekani imesema kuwa ipo katika hatua za kukabiliana na shambulio la kimitandao, lililopo kwa watumiaji wa simu za IPhone na iPad nchini China. Watalaam wa ndani ya kampuni hiyo wamesema kuwa hilo ni moja la shambulio kubwa la kimitandao kuwahi kuikumba kampuni hiyo. Msemaji wa kampuni ya Apple anasema kuwa kampuni yao imeondoa kwenye mzunguko wa soko vifaa vyote vinavyotiliwa shaka kuingiliwa na wavamizi hao wa kimitandao nchini...

Like
229
0
Monday, 21 September 2015
KENYA: SERIKALI YAAGIZA SHULE ZIFUNGWE
Global News

SERIKALI ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu ijayo huku mgomo wa walimu ukiendelea. Barua iliyotolewa na wizara ya elimu nchini humo imeagiza shule zote za umma na binafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani na kwamba watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kwa Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT zinasema kuwa tayari amepokea barua...

Like
290
0
Friday, 18 September 2015
BURKINA FASO: MAPINDUZI KUJADILIWA
Global News

MARAIS wawili wa mataifa ya Afrika Magharibi, Macky Sall wa Senegal na Thomas Boni Yayi wa Benin, wanaelekea Burkina Faso kufanya mashauriano na viongozi waliopindua serikali. Mapinduzi hayo yalitangazwa baada ya walinzi wa rais kuvamia mkutano wa baraza la mawaziri na kuwawekea kizuizi rais Michel Kafando na waziri mkuu wake Isaac Zida. Rafiki wa karibu wa kiongozi wa zamani Blaise Compaore, Jenerali Gilbert Diendere, alitangazwa kiongozi mpya jana,...

Like
214
0
Friday, 18 September 2015
CROTIA KURUHUSU WAHAMIAJI KUINGIA MAGHARIBI MWA ULAYA
Global News

WAZIRI mkuu wa Croatia amesema nchi yake haiwezi kuwazuia wahamiaji wanaotaka kuelekea upande wa magharibi mwa Ulaya. Zoran Milanovic amesema Croatia itajaribu kuwaandikisha wakimbizi wengine zaidi kadiri itakavyowezekana. Mamlaka nchini humo zinasema jumla ya wahamiaji Elfu 11 wameingia nchini humo baada ya Hungary kufunga mpaka wake uliosababisha kufungwa kwa njia ya kuelekea nchi za...

Like
219
0
Friday, 18 September 2015