Global News

ICC: NTAGANDA AKANUSHA MASHTAKA YA UHALIFU WA KIVITA
Global News

ALIYEKUWA kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, amekanusha mashtaka aliyokuwa yakimkabili ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadam, baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kimataifa ya jinai, ICC, iliyoko mjini the Haque leo. Ntaganda anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya raia mia nane na kuwabaka watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini kama watumwa wa ngono. Mashtaka yote yanahusiana na wakati alipokuwa akiongoza mapigano katika eneo la Ituri Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo...

Like
240
0
Wednesday, 02 September 2015
BUDAPEST: SAFARI ZA TRENI KWA WAHAMIAJI ZASITISHWA
Global News

KITUO kikuu cha reli cha kimataifa mjini Budapest leo kimeamuru kuondolewa kwa mamia ya wahamiaji wanaojaribu kupanda treni kuelekea Austria na Ujerumani. Tangazo la kipaza sauti lililotolewa hadharani limesema hakuna treni zitakazoondoka au kuwasili katika kituo hicho cha Keleti hadi hapo itakapotolewa taarifa zaidi na kwamba kila mtu alitakiwa aondoke katika kituo hicho. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP tangazo hilo linakuja baada ya wahamiaji 500 wanaume,  wanawake na watoto kujaribu kupanda treni ya mwisho kuelekea...

Like
195
0
Tuesday, 01 September 2015
ALSHABAAB YASHAMBULIA KAMBI YA AMISOM
Global News

KUNDI la wapiganaji wa Kiislamu la Al – Shabaab limeshambulia kambi ya kikosi cha walinda usalama wa muungano wa Afrika AMISOM na Kujeruhi watu wengi katika shambulio hilo. Al-Shabaab wamejisifia kuwa mmoja wa walipuajI wake wa kujitolea ameliendesha gari liliolkuwa na bomu ndani ya kambi ya Janale umbali wa kilomita 90 kutoka mji mkuu Mogadishu kisha wapiganaji wake wengine wakashambulia kwa risasi. Kwa mujibu wa Al shabaab, wanajeshi hamsini wa AMISOM wameuawa japo ripoti hizo hazijathibitishwa kutoka upande wa AMISOM....

Like
219
0
Tuesday, 01 September 2015
BOKO HARAM YADAIWA KUENEA LAGOS
Global News

MAAFISA wa Serikali nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, wanajaribu kupanua shughuli zao kutoka maeneo ya Kaskazini, yenye idadi kubwa ya Waislamu, hadi mji mkuu wa Lagos na maeneo mengine. Wakati huo huo idara ya ujasusi nchini humo imesema kuwa imewakamata takriban makamanda 20 wa kundi hilo la Boko Haram. Aidha idara hiyo imesema kuwa wapiganaji wengine wamekamatwa katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa nchi hiyo yakiwemo ya Kano, Gombe , Central Plateau, pamoja na...

Like
270
0
Monday, 31 August 2015
NJAA YAIKABILI SOMALIA
Global News

UMOJA wa Mataifa umeelezea viwago vya utapiamlo na hali ya usalama wa chakula nchini Somalia na kusema kuwa idadi ya watu ambao wanakabiliwa na ukosefu wa chakula imeongezeka kwa karibu asilimia 20 katika muda wa miezi sita iliyopita. Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa mvua na mzozo unaoendelea. Karibu theluthi moja na watu nchini Somalia wanahitaji msaada wa kibinadamu huku Watu robo milioni wameaga dunia nchini Somalia wakati njaa ilipoikumba nchi hiyo miaka minne iliyopita....

Like
213
0
Monday, 31 August 2015
MZOZO WAIBUKA KATI YA HUNGARY, UFARANSA
Global News

MZOZO wa kidiplomasia umeibuka kati ya Hungary na Ufaransa juu ya uamuzi wa Hungary kuweka ukuta katika mpaka wake na Serbia ili kuzuia kuingia wahamiaji haramu. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema kuwa ujenzi wa ukuta huo  ni ukiukaji wa maadili ya nchi za ulaya. Hata hivyo mwenzaeke kutoka upande wa Hungary Peter Szijjarto ameelezea kushangazwa kwake na madai hayo nakusema kuwa bara la Ulaya linastahili kushirikiana kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu badala ya kuelekezeana...

Like
174
0
Monday, 31 August 2015
IS WALIPUA MADHABAHU SYRIA
Global News

WAPIGANAJI wa dola ya kiislamu IS, wanadaiwa kulipua sehemu ya madhabahu ya kidini katika mji wa Syria wa Palmyra. Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Syria limesema kuwa wanamgambo hao wametumia mabomu kulipua hekalu hilo la kiroma ya Bel. Islamic State waliuteka mji wa Palmyra mwezi Mei na kuzua hofu ya kushambuliwa madhabahu hayo....

Like
239
0
Monday, 31 August 2015
UN KUCHUNGUZA MASHAMBULIZI YA KEMIKALI SYRIA
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba anapanga kuchunguza mashambulizi ya kemikali nchini Syria. Ban Ki – Moon ameuelezea mpango wake wa kuwabaini wahusika wa mashambulizi hayo, katika barua yenye kurasa saba. Hatua hiyo imetangazwa baada ya baraza hilo la usalama kuidhinisha azimio kuhusu Syria, mwanzoni mwa mwezi...

Like
212
0
Friday, 28 August 2015
ZAIDI YA WAHAMIAJI 200 WAANGAMIA LIBYA
Global News

ZAIDI ya watu mia mbili wanahofiwa kufariki baada ya boti mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama katika eneo la Zurawa pwani ya Libya. Mamia ya wahamiaji wengine wameokolewa na wanamaji wa Libya usiku wa kuamkia leo. Kwa zaidi ya mwaka mmoja Libya haijakuwa na serikali thabiti na sehemu kubwa ya nchi hiyo inathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu, na walanguzi wa watu wanatumia nafasi hiyo kusafirisha watu kimagendo hadi...

Like
220
0
Friday, 28 August 2015
NASA: TOKYO NA SINGAPORE MIONGONI MWA MAENEO YANAYOHOFIWA KUZAMA BAHARINI
Global News

UTAFITI mpya uliyofanywa na shirika la utafiti wa safari za anga la Marekani NASA, unaonyesha kuwa kuongezeka kwa kina cha maji baharini kwa zaidi ya mita moja katika kipindi cha miaka 100 hadi 200 ijayo hakuzuwiliki. Kuongezeka huko kunatishia kuyazamisha maeneo na miji mikubwa duniani iliyoko chini ya usawa wa kina cha bahari kama Tokyo na Singapore. Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha utafiti cha NASA Michael Freilich, zaidi ya watu milioni 150, wengi wao kutoka bara la Asia,...

Like
215
0
Friday, 28 August 2015
NIGERIA:MATUMAINI YA KUWAPATA WANAFUNZI WALIOTEKWA NA BOKO HARAM YAZIDI KUFIFIA
Global News

LEO zimetimia siku 500 tangu wanafunzi zaidi ya 200 wa kike walipotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram kutoka mji cha Chibok kaskazini-mashariki mwa Nigeria, huku matumaini ya kupatikana kwa wanafunzi hao yakizidi kufifia.   Kumbukumbu hiyo inafanyika wakati hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya katika eneo hilo, ambako Boko Haram wamezidisha mashambulizi tangu kuingia madarakani kwa rais Muhammadu Buhari, ambapo wameuwa zaidi ya watu 1,000 katika miezi mitatu.   Wapiganaji hao walivamia shule ya serikali mjini Chibok...

Like
250
0
Thursday, 27 August 2015