Global News

WANUNUZI WA MALI KWA PESA CHAFU KUONYWA UINGEREZA
Global News

WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kulaani matumizi ya fedha chafu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinazotumiwa kununua mali nchini Uingereza. Katika hotuba anayotarajia kuitoa nchini Singapore muda mfupi ujao waziri Cameron anatarajiwa kuahidi kufichua taarifa ya kutumiwa kwa kampuni za kununua mali za kifahari na kusema kuwa Uingereza haipaswi kuwa mahali pa fedha za wizi. Zaidi ya mali laki moja za Uingereza zimesajiliwa kwa majina ya kampuni za kigeni na zaidi ya robo ya kampuni hizo zipo jijini...

Like
166
0
Tuesday, 28 July 2015
MTOTO WA GADDAFI AHUKUMIWA KUNYONGWA
Global News

MAHAKAMA moja nchini Libya imemuhukumu kuyongwa mtoto wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Gaddafi, Saif al Islam na wengine nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011. Watuhumiwa hao walikuwa wameshitakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kuzima maandamano wakati wa mapinduzi hayo. Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video ambapo hadi sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji...

Like
285
0
Tuesday, 28 July 2015
MAREKANI YATHIBITISHA KUENDELEZA MAZUNGUMZO NA UTURUKI
Global News

MAREKANI imethibitisha kuwa itaendeleza mazungumzo na Uturuki kuhusu kutoa majeshi yake yanayopambana na kikosi cha kigaidi cha Islamic State huko magharibi mwa Syria. Msemaji wa idara ya Usalama wa nchi hiyo John Kirby amesema jitihada, nguvu na umoja unapaswa kuwepo kwa kuangazia zaidi katika maeneo muhimu hususani ya mipakani. Hata hivyo Askari wa Kurdish PKK wamesema kuwa shambulio la Uturuki liko juu ya Uturuki ambayo inasimamia mapambano yake dhidi ya PKK ingawa Majeshi ya Kurdish bado yanapambana na wanamgambo wa...

Like
247
0
Tuesday, 28 July 2015
BURUNDI: KIONGOZI WA UPINZANI AHUDHURIA KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE
Global News

KIONGOZI wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa amehudhuria kikao cha kwanza cha bunge tangu kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge june 29 mwaka huu. Hatua hiyo imewashangaza watu wengi kwa kuwa awali alipinga matokeo ya uchaguzi huo pamoja na yale ya urais wiki iliopita ambapo alijipatia asilimia 20 ya kura katika uchaguzi mkuu. Hata hivyo viti 12 kati ya 30 vya muungano wake havikuwa na wabunge huku wabunge walio watiifu kwa kiongozi mwenza Charles Nditije wakisusia kikao...

Like
193
0
Tuesday, 28 July 2015
MASHAMBULIZI DHIDI YA HOUTHI YASITISHWA
Global News

MAJESHI ya muungano yakiongozwa na jeshi la Saudi Arabia yamesitisha mashambulizi yake ya angani nchini Yemen, baada ya kuanza muafaka wa amani wa kusitisha mapigano. Muafaka huo umeafikiwa kati ya majeshi hayo na wapiganaji wa Houthi chini ya Umoja wa mataifa, ili kuyaruhusu mashirika ya utoaji misaada kufikisha chakula na dawa kwa watu wanaothirika na mapigano hayo. Lakini vyanzo vya habari vinasema kumekuwa na mashambulizi makali ya roketi kusini mwa Yemen, hata kabla ya kuanza kwa muda huo wa kusitisha...

Like
179
0
Monday, 27 July 2015
HAKI ZA BINADAMU: OBAMA AIONYA ETHIOPIA
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora. Akizungumza katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika. Kwa upande wake Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia....

Like
175
0
Monday, 27 July 2015
SYRIA: BASHAR AL ASSAD AMEKIRI KUPUNGUA KWA MAJESHI YAKE
Global News

RAIS wa Syria Bashar al Assad amekiri kuwa idadi ya wanajeshi wake imepungua lakini amesisitiza kuwa bado jeshi hilo lina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa makundi ya waasi. Assad ambaye aliuhutubia umma hapo jana katika mji mkuu wa Syria, Damascus pia amesema juhudi zozote za kuvikomesha vita nchini mwake ambazo hazitazingatia suala la kupambana dhidi ya ugaidi hazitakuwa na tija yoyote. Jeshi la Syria ambalo wakati mmoja lilikadiriwa kuwa na wanajeshi laki tatu limepungua kwa asilimia 50 kutokana na...

Like
205
0
Monday, 27 July 2015
OBAMA ATUA ETHIOPIA
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya kuzitembelea baadhi ya nchi za Afrika. Imeelezwa kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza tangu aongoze Taifa la Marekani akiwa rais kuhutubia wanachama 52 wa umoja wa Afrika katika makao makuu yaliyoko Addis ababa nchini Ethiopia. Hata hivyo Mazungumzo yao yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini sudan ya kusini ambapo Rais Obama amewasili nchini Ethiopia akitokea mjini...

Like
223
0
Monday, 27 July 2015
OBAMA ATARAJIWA KUTUA KENYA LEO
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani yuko njiani kuelekea Kenya hii leo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza akiwa rais kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, alikozaliwa baba yake mzazi. Obama, ambaye ni rais wa kwanza mweusi nchini Marekani, ni mtoto wa Barack Hussein Obama Mkubwa, Mkenya aliyekutana na mama yake Obama, wakati wawili hao wakisoma nchini Marekani. Anatazamiwa pia kukutana na baadhi ya jamaa zake wa ubabani akiwa Nairobi, ingawa hategemewi kutembelea kijiji cha Kogelo inakotokea familia...

Like
227
0
Friday, 24 July 2015
EU YATANGAZA AZMA KUIWEKEA VIKWAZO BURUNDI
Global News

HUKU raia nchini Burundi wakisubiri kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi wa rais na pia kufanyika uchaguzi wa baraza la Seneti leo, Umoja wa Ulaya umetangaza azma ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo ndogo ya Afrika Mashariki. Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, amesema Umoja huo uko tayari kuwawekea vikwazo wale ambao vitendo vyao vilisababisha kutokea kwa ghasia, ukandamizaji, na uvunjwaji wa haki za binaadamu na pia kukwamisha upatikanaji wa suluhisho la kisiasa. Miongoni mwa wanaotazamiwa...

Like
177
0
Friday, 24 July 2015
MAREKANI: MTU MWENYE SILAHA AFANYA SHAMBULIO KATIKA UKUMBI WA SINEMA
Global News

POLISI katika jimbo la Louisiana nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki amewafyatulia risasi raia katika ukumbi wa sinema na kumuua mtu mmoja na wengine sita wamejeruhiwa , na mshambuliaji mwenyewe pia amejiua. Walioshuhudia wanasema kuwa walimuona mtu mmoja, mzungu wa umri wa miaka 50 au zaidi, amejitokeza kunako dakika ishirini baada ya filamu kuanza , na kisha kuanza kufyatua risasi kiholela. Tukio hilo limetokea saa chache tu baada ya Rais Barack Obama kuzungumzia tatizo la udhibiti wa...

Like
241
0
Friday, 24 July 2015