Global News

BUNGE LA MAREKANI LAIDHINISHA MABADILIKO MAPANA YA SHERIA YA UPELELEZI
Global News

BUNGE la Marekani limeidhinisha mabadiliko mapana katika sheria za upelelezi zilizopitishwa baada ya mashambulio ya kigaidi yaliyotokea Septemba 11mwaka wa 2001. Mabadiliko hayo yaliuondoa mpango wenye utata wa Shirika la Usalama wa Kitaifa – NSA wa kukusanya data za mawasiliano ya simu unaowaathiri mamilioni ya Wamarekani kuchukuliwa sheria kali zaidi ya kuhifadhi rekodi hizo katika makampuni ya huduma za simu. Sheria hiyo itafufua mipango mingi ambayo baraza la Seneti liliruhusu muda wake kumalizika ambapo tayari Rais wa Marekani...

Like
237
0
Wednesday, 03 June 2015
IRAQ YASEMA HAISAIDIWI KWENYE VITA DHIDI YA IS
Global News

WAZIRI mkuu wa Iraq  HAIDER AL-ABADI amesema kuna ushahidi mdogo  wa kuwepo kwa uungwaji mkono wa kimataifa katika vita vyao dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika nchi yake. Matamshi hayo ya  ABADI yanakuja wakati wa kikao kinachotarajiwa kufanyika huko Ufaransa cha mataifa walioungana kulipiga vita kundi hilo la wapiganaji la Islamic state. Aidha Waziri HAIDER AL-ABADI  ameonya kuwa kinyume na matarajio wanamgambo hao wa kundi la IS wanaendelea kuwasajili watu wengi ili kujiunga...

Like
240
0
Tuesday, 02 June 2015
AJUZA AOKOLEWA KATIKA MELI ILIYOZAMA CHINA
Global News

WAOKOZI nchini china wanaowatafuta watu waliozama ndani ya maji kutoka kwenye meli ya abiria iliyozama katika mto Yangtze wameweza kumvuta kutoka kwenye meli hiyo mwanamke mwenye umri wa miaka 85. Mwanamke huyo ni mmoja wa watu wapatao 12 wanaofahamika kunusurika katika ajali hiyo iliyotokea baada ya meli hiyo kuzama jana usiku nchini China . Miili ya watu imekuwa ikivutwa kutoka kwenye meli hiyo ambapo zaidi ya  watu 400 walikuwa katika meli hiyo ilipopata ajali kutokana na hali mbaya ya...

Like
308
0
Tuesday, 02 June 2015
UMOJA WA MATAIFA WAITUHUMU IS NA MAKUNDI MENGINE YENYE SILAHA KWA KUWATESA NA KUWAUA WATOTO
Global News

UMOJA wa Mataifa umeishutumu IS na makundi mengine yenye silaha nchini Syria na Iraq kwa kuwatesa na kuwaua watoto. Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika kuwa wanahusika na matumizi ya kundi kubwa la watu wenye umri chini ya miaka 15 kutumiwa na makundi ya kigaidi ya Al-Nusra Front lenye uhusiano na Al-Qaeda. Kundi la Islamic State limeondoa mfumo wa elimu ya kawaida na badala yake kuanzisha shule za mtindo wa kijeshi ambazo zinawafundisha watoto itikadi kali ya kidini ikiwemo kuwafundisha...

Like
211
0
Tuesday, 02 June 2015
YEMEN: VIONGOZI WA KUNDI LA WAASI WAFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA MAREKANI
Global News

SERIKALI ya Yemen iliyo uhamishoni nchini Saudi Arabia imesema viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi wa Houthi wanafanya mazungumzo na maafisa wa Marekani nchini Oman kuendeleza juhudi za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Yemen. Muungano unaongozwa na Saudi Arabia ulianza mashambulizi ya kutokea angani mwezi Machi mwaka huu katika harakati ya kumrejesha madarakani rais wa Yemen Abd-Rabbu Mansour Hadi. Hadi alikimbia baada ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuudhibiti mji mkuu Sanaa mwezi Septemba mwaka uliopita...

Like
189
0
Monday, 01 June 2015
WANAWAKE WAANDAMANA WAKIWA WATUPU KATIKA KIJIJI KIMOJA UGANDA
Global News

WANAWAKE katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa watupu kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kipindi cha miaka 10 hadi sasa. Maandamano hayo yanekuja kufuatia mawaziri wa serikali na watafiti kuweka mpango wa kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru nchini humo. Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakazi wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa...

Like
327
0
Monday, 01 June 2015
NDAYIZEYE AMTAKA NKURUNZINZA KUTOGOMBEA KWA MUHULA WA TATU
Global News

RAIS mstaafu wa Burundi DOMITIEN NDAYIZEYE amemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo PIERRE NKURUNZINZA kutogombea kwa muhula wa tatu kwani hatua hiyo inavunja maridhiano yaliyofanyika yaliyomtaka rais huyo kukaa madarakani kwa mihula miwli. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika mashariki amesema kuwa mkataba uliosainiwa umebainisha kila makubaliano waliyoafikiana lakini hatua inayofanywa sasa na rais NKURUNZINZA umesababisha ukiukwaji wa haki za binadamu. Aidha rais huyo mstaafu amesema...

Like
229
0
Monday, 01 June 2015
CHINA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SIGARA KATIKA MAENEO YA WAZI
Global News

SERIKALI ya China imepiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing. Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote yaliyoanishwa kutohusika na kitendo cha uvutaji sigara ambapo kwa wale watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa faini. Hata hivyo tafiti zinasema kuwa  China ina jumla ya wavutaji sigara milioni 300 wakati sheria ya kusitisha uvutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa...

Like
213
0
Monday, 01 June 2015
WANAHARAKATI WALISHUTUMU JESHI LA IRAQ
Global News

WANAHARAKATI wa haki za binadamu wamelishutumu Jeshi la Iraq kwa kushindwa kuokoa maelfu ya watu kufika sehemu salama ya nchi hiyo baada ya wao kukimbia mapigano katika jimbo la Anbar . wanasema kuwa serikali inayowaongoza ina waislamu wengi wa madhehebu ya Shia inawabagua waisalamu wa madhehebu ya Suni waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Islamic State aambao nao pia ni Waislamu wa Suni. Hata hivyo kwa wale wanaojaribu kuingia mji wa Baghdad wanakutana na vikwazo vya barabarani katika mitaa...

Like
204
0
Monday, 01 June 2015
MUHAMMADU BUHARI APISHWA KUWA RAIS NIGERIA
Global News

NIGERIA leo imemwapisha bwana Muhammadu Buhari kuwa rais mpya wa nchi hiyo ambako zaidi ya nchi 30 za Afrika zinawakilishwa na viongozi katika sherehe hizo.   Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anahudhuria pia sherehe hizo wakati  Marekani inawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nchi za nje John Kerry,Uingereza na waziri  wake wa mambo ya nchi za nje Philipp Hammond na Laurent Fabius anaiwakilisha Ufaransa.   Licha ya matatizo yanayolikabili taifa hilo linalochimba mafuta kwa wingi zaidi barani Afrika,ushindi...

Like
362
0
Friday, 29 May 2015
VIONGOZI WA NCHI 17 DUNIANI KUKUTANA BANGKOK KUJADILI ONGEZEKO LA WAHAMIAJI HARAMU
Global News

VIONGOZI wa nchi 17 Ulimwenguni wanakutana mjini Bangkok nchini Thailand kutafuta mbinu bora za kukabiliana na tatizo linalozidi kuongezeka la wahamiaji haramu wanaotoka Myanmar na Bangladesh maeneo ambayo nchi zake zinaoongoza kwa kuwa na idaidi kubwa ya wahamiaji. Miezi kadhaa iliyopita maelfu ya wahamiaji haramu walitua katika pwani ya mwambao wa bahari ya Indonesia, Malaysia na Thailand. Hata hivyo wengi wa wahamiaji hao walijikuta wakizama baharini huko nchini Thailand mapema mwezi huu....

Like
180
0
Friday, 29 May 2015