AUSTRALIA imeonya kuwa haitawaruhusu wakimbizi wa jamii ya waislamu wa Rohingya waliowasili nchini humo kwa mashua kuishi. Waziri mkuu, wa nchi hiyo Tony Abbott, anasema kuwa ni muhimu mataifa ya magharibi kutafuta mbinu ya kuzuia ulanguzi wa watu. Anasema, njia pekee ni kuhakikisha kuwa hakuna mashua ambayo inawabeba wahamiaji hadi katika taifa lolote la magharibi....
VIONGOZI Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa. Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea msituni. Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya...
VIKOSI maalum kutoka Ufaransa vimewaua wapiganaji wanne wa kijihadi, wakiwemo viongozi wawili katika shambulizi lililofanyika eneo la kaskazini mwa Mali. Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Ufaransa mmoja wa wale waliouwawa ni Amada Ag Hama, anyeshukiwa kuhusika katika utekaji nyara na mauaji ya wanahabari wawili wa Ufaransa mwaka 2013. Ufaransa iliwatuma wanajeshi wake nchini Mali miaka miwili iliyopita wakati wanamgambo wa kiislamu walipotishia kuuteka mji mkuu, Bamako. Wanajeshi 3,000 wa kikosi cha ufaransa bado wapo katika eneo hilo...
WAZIRI MKUU wa Maysia Najib Razak amesema kuwa taifa lake litaanzisha operesheni ya kutafuta na kukomboa mashua za wahamiaji wa kabila la Rohingya katika bahari ya Andaman. Aidha amebainisha kuwa misaada ya kibinadamu kadhalika itatolewa kwa uchukuzi wa barabarani na majini. Tangazo lake limekuja baada ya maafisa kuzuia mashua za wahamiaji hao kuingia katika maji ya Malaysia, na wakati mwingine kuziondoa kwa kuzikokota kutoka maji hayo kwa majuma...
RAIS wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi . Sababu ya hatua hiyo ni mgogoro wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo ndogo ya eneo la maziwa makuu. Msemaji wa rais huyo, Willy Nyamitwe ameliambia Shirika la habari la Reuters, kwamba Rais Nkurunziza amechukua uamuzi huo baada ya kupendekezwa na tume ya uchaguzi na kufuatia pendekezo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na Jumuiya ya kimataifa kutaka uchaguzi uahirishwe. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa kitisho cha kuzuka machafuko...
RAIS wa Ukraine Petro Poroshenko amesema kuwa hamuamini kiongozi wa Urusi Vladimir Putin katika harakati za kuleta Amani Mashariki mwa Ukraine. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, Poroshenko anasema anahofia kwamba huenda kukawa na kutoku elewana kati ya mataifa hayo mawili. Hata hivyo ameielezea hali hiyo kuwa ni vita kamili kati ya nchi hizo. Vladimir Putin ...
MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa Thailand, Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa dharula mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika ukanda wao. Nchi hizo tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya wahamiaji waliokwama Baharini ambao wanahitaji chakula na maji. Wahamiaji wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar, lakini Serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo. Bado kuna hofu kuhusu usalama wa waliokwama baharini....
Rais wa Afrika kusini JACOB ZUMA amesema uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Burundi mwezi ujao unapaswa kuahirishwa hadi Amani itakaporejea nchini humo. Rais ZUMA ameyasema hayo wakati akitoa muhtasari wa matokeo ya mkutano wa eneo la kusini mwa Afrika uliofanyika nchini Angola. Mkutano huo maalum uliitishwa baada ya jaribio la mapinduzi kushindwa nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza , ambaye uamuzi wake wa kugombea kipindi cha tatu cha ...
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amemtaka Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuahirisha uchaguzi mkuu nchini mwake unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao baada ya jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa Nkurunziza kushindwa wiki iliyopita. Msemaji wa Rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema viongozi hao wawili wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki walizungumza hapo jana kwa njia ya simu. Espisu amesema viongozi wengine wa nchi za kanda hiyo ya Afrika Mashariki wana mtizamo sawa na...
HALMASHAURI ya Kimataiafa ya safari za baharini IBM imetoa ripoti yake ya hivi punde kuhusu uharamia. Halmashauri hiyo inasema kuwa uharamia sasa umeripotiwa Kusini Mashariki mwa bara Asia, huku Meli ndogo za kusafirisha mafuta zikishambuliwa baada ya kila wiki mbili. Kwenye ripoti yake ya kila baada ya miezi mitatu, IMB inasema kuwa licha ya kupungua kwa mashambulizi kote duniani miaka ya hivi majuzi, visa vya uharamia viliongezeka katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2015....
ETHIOPIA imeanza siku tatu za maombolezi ya Kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na Wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya. Bendera zitapepea nusu mlingoti wakati pia bunge la nchi hiyo litakutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya Ishirini. Msemaji wa serikali REDWAN HUSSEIN, amesema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani...