Global News

MOHAMMED MOSRI AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA
Global News

Habari za hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Mosri amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwachochoea wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood kuwaua waandamanaji wa upinzani alipokuwa madarakani mwaka...

Like
214
0
Tuesday, 21 April 2015
YEMEN: WAASI WAIKASHIFU SAUDI ARABIA
Global News

HOSPITALI kwenye mji wa bandari wa Yemen, Aden zimeripotiwa kuishiwa na bidhaa muhimu za matibabu wakati mapigano kati ya vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Shia wa Houthi yanaongezeka. Makundi ya kutoa huduma za matibabu yamelemewa na idadi ya wagonjwa wanaolazwa na yametoa wito kwa dawa zaidi na vifaa vingine vya matibau. Kiongozi wa waasi ameikashifu Saudi Arabia kwa kujaribu kuivamia na kuiteka nchi ya Yemen....

Like
250
0
Monday, 20 April 2015
SOMALIA: SHAMBULIZI LAUA WATU SABA
Global News

POLISI nchini Somalia wanasema kuwa takriban watu Saba wameuawa kwenye shambulizi lililolenga gari la Umoja wa Mataifa katika eno linalojisimamia la Puntland. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema kuwa wanne kati ya wafanyakazi wake waliuawa wakati mlipuko mkubwa ulipolipua basi kwenye mji ulio kaskazini mashariki wa Garowe. Shirika hilo linasema kuwa wale waliokufa wanatoka nchi tofauti. Kundi la wanamgamo wa Al shabaab linasema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo....

Like
195
0
Monday, 20 April 2015
POLISI LONDON WAPEKUA MSIKITI KUCHUNGUZA MAUAJI YA IMAM WA SYRIA
Global News

POLISI mjini London wamekuwa wakiupekua msikiti mmoja ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wake wa mauaji ya Imam mmoja wa zamani kutoka Syria. Abdul Hadi Arwani alipigwa risasi na kuuawa wiki moja iliopita katika makazi ya Wembley mjini London. Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa jamii ya waislamu ili kuwahakikishia kwamba upekuzi huo  ni muhimu, na kwamba msikiti huo utafunguliwa haraka iwezekanavyo. Abdul Arwani ameripotiwa kuwa mpinzani wa rais Assad wa Syria. Watu wawili wamekamatwa kuhusiana...

Like
255
0
Wednesday, 15 April 2015
KENYA YAAHIDI KUSAMEHE RAIA WAKE WALIOPOKEA MAFUNZO YA KIGAIDI WATAKAOJISALIMISHA NDANI YA SIKU KUMI ZIJAZO
Global News

SERIKALI ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo. Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani, Jenerali mstaafu Joseph Nkaissery ambae pia amewaonya wazazi wa vijana kama hao kwamba watachukuliwa hatua kali endapo hawataijulisha serikali kuhusu kujiunga kwa wanao na kundi la Al Shabaab. Serikali imewapa wale wote waliopokea mafunzo kutoka kwa Al Shabaab siku kumi kujisalimisha katika ofisi za wasimamizi wa miji ya Garissa, Mombasa au Nairobi....

Like
201
0
Wednesday, 15 April 2015
MAPIGANO YAZUKA UPYA UKRAINE
Global News

MAWAZIRI wa Mashauri ya Kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain wameelezea wasiwasi uliopo kufuatia kutokea kwa mapigano Mashariki mwa Ukrein na kikiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Februari. Baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin, Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Ujerumani FRANK-WALTER STEINMEIER amewaambia Waandishi wa Habari kuwa kati ya silaha ambazo zitaondoa ni pamoja na Vifaru. Pande hizo mbili zimeonekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa...

Like
224
0
Tuesday, 14 April 2015
KENYA YATOA MIEZI MITATU KWA UNHCR KUIFUNGA KAMBI YA DADAAB
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limepewa muda wa miezi mitatu kuifunga kambi ya wakimbizi mashariki ya Kenya na kuwarejesha kwao wakimbizi zaidi ya laki nne wa kisomali la sivyo serikali ya Kenya itawahamisha. Kauli hiyo imetolewa na Makamo wa rais wa Kenya William Ruto ambaye amesema Serikali ya Kenya inasema kambi ya Dedaab imegeuka kituo cha usajili cha wafuasi wa itikadi kali wa Al Shabab-waliowauwa zaidi ya watu 148 wiki iliyopita katika chuo kikuu cha Garissa Akihutubia...

Like
274
0
Monday, 13 April 2015
SUDAN YAINGIA KWENYE UCHAGUZI MKUU LEO
Global News

UCHAGUZI Mkuu nchini Sudan umeanza leo  huku dalili zikionesha kwamba Rais wa sasa wa nchi hiyo OMAR AL BASHIR anatarajiwa kushinda kiti hicho cha Urais. Taarifa zinasema kuwa Vyama vingi vya upinzani vimesusia uchaguzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaoendeshwa na rais OMAR AL BASHIR. Hata hivyo inaaminika kuwa Rais BASHIR alifanya kampeni kubwa akihutubia mikutano ya hadhara sehemu tofauti za taifa hilo kubwa na kwamba ndiye kiongozi pekee wa nchi aliyewekewa hati ya kukamatwa na...

Like
287
0
Monday, 13 April 2015
KIONGOZI WA DA ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA UCHAGUZI UJAO
Global News

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance, DA, amesema hatagombea katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao. Helen Zille amesema ni wakati muafaka kwake kutogombea, akisema kuwa DA watanufaika na mchango wa vijana. Atabaki kuwa waziri mkuu wa jimbo la Western Cape hadi mwaka 2019.   Zille, ni mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka...

Like
245
0
Monday, 13 April 2015
BI. HILLARY CLINTON ATARAJIWA KUTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS
Global News

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Hillary Clinton atakuwa rais bora na mwenye maono kwa nchi ya Marekani. Bi Clinton anatarajiwa kutangaza hii leo kuwa atawania uteuzi wa chama cha Democratic. Obama amesema kuwa Bi Clinton alitekeleza kwa njia nzuri majukumu yake alipohudumu kama waziri wa mashauri ya kigeni. Atatangaza azma yake ya kuwania urais kwa njia ya video ambayo itasambazwa kupitia kwa mitandao ya kijamii. Kinyume na miaka minane iliyopita Bi Clinton anatarajiwa kuangazia zaidi jinsi wapiga kura...

Like
233
0
Sunday, 12 April 2015
PALESTINA WAUNGANA NA SYRIA KUWAONDOA IS
Global News

WANANCHI wa Palestina wanasema kuwa wamekubali kushirikiana na Serikali ya Syria ili kujaribu kuwaondoa wapiganaji wa IS nje ya kambi moja ya wakimbizi viungani mwa Damascus. Tangazo kama hilo lilifanywa na Afisa mmoja wa Serikali ya Palestina huko West Bank. Wapiganaji wa IS walitekeleza shambulizi katika kambi hiyo wiki iliopita na kuweza kuiyumbisha kambi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa jeshi la Palestina....

Like
240
0
Friday, 10 April 2015