Slider

SAMSUNG “YASITISHA UTENGENEZAJI WA GALAXY NOTE 7”
Slider

Kampuni kubwa ya kutengeza simu aina ya smartphone Samsung,imeroptiwa kusitisha utengezaji wa simu aina ya Galaxy Note 7 kufuatia madai kwamba simu mpya zilizotengezwa kuchyukua mahala pa zile zilizo na matatizo ya betri pia zina matatizo. Vyombo vya habari vya Reuters na kile cha Yonhap kutoka Korea kusini vimewanukuu baadhi ya maafisa ambao hawakutajwa majina wakisema kuwa kampuni hiyo imesitisha kwa muda utengezaji wa simu hizo. Samsung imeambia BBC inaimarisha utengezaji wa simu hizo ili kuhakikisha ubora na usalama wake....

Like
348
0
Monday, 10 October 2016
CHINA YASHINDA TUZO YA KUTAMBUA MVINYO DUNIANI
Slider

Kundi moja la wataalam nchini China limeshinda tuzo la shindano la kuonja mvinyo nchini Ufaransa. Watalaam hao walitambua mivinyo waliopewa huku wakiwa wamefunikwa uso,wakibainisha asili, aina ya zabibu zilizotumika na mwaka mivinyo hiyo iliotengezwa. Waandalizi wa shindano hilo waliwataja wataalam hao wa China kuwa mabingwa katika ulimwengu wa mvinyo. Waliyashinda mataifa mengine 20,ikiwemo washindi wa awali Ubelgiji na Uhispania. Huku mapato yakiongezeka nchini China,taifa hilo linaongoza katika utengezaji na utumiaji wa mvinyo...

Like
346
0
Monday, 10 October 2016
SAMSUNG NOTE 7 YASHIKA MOTO KWENYE NDEGE
Slider

Simu ya kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, imeshika moto kwenye ndege nchini Marekani. Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa na abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines. Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake, iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa Jumatano. Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu...

Like
247
0
Thursday, 06 October 2016
ASWEKWA LUPANGO KWA KUMNYONGA MKEWE
Slider

Mkazi wa Kijiji cha Igate, Kata ya Nzera wilayani Geita anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga mkewe Dotto Frederick (25) baada ya kuibuka ugomvi kati yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kuwa mauaji hayo yalitokea nyumbani kwa mtuhumiwa.   Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Oktoba Mosi eneo la Machimboni Kijiji cha Muranda Kata ya Buseresere wilayani hapa baada ya kuishi mafichoni kwa siku 15. Kamanda Mwabulambo amesema mtuhumiwa huyo alimnyonga mkewe kwa kutumia kipande cha nguo...

Like
213
0
Thursday, 06 October 2016
YANGA YATOA MUHTASARI WA MKATABA
Slider

1.    Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji” kwa muhtasari wa maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano Mkuu wa Young Africans Sports Club uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016 ulitambua kuwa Young Africans Sports Club (anayejulikana hapa kama “YANGA”): 1.1    KWA KUWA, Timu ya Soka ya Mmiliki ni kongwe na yenye mafanikio kuliko timu ya soka nyingine...

Like
279
0
Thursday, 06 October 2016
BODI YA WADHAMINI CUF KUMFUNGULIA KESI LIPUMBA NA MSAJILI
Slider

Bodi ya wadhamini CUF imefungua maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama 12 waliosimamishwa uanachama wa chama hicho. Katika maombi hayo bodi hiyo inaomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya Msajili, Lipumba na wenzake, ili mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili asifanye kazi nje ya mipaka ya mamlaka yake kisheria. Jana wajumbe wanne wa bodi hiyo waliibuka na kuunga mkono msimamo wa msajili wa vyama vya...

Like
224
0
Wednesday, 05 October 2016
TYSON FURY AKIRI KUTUMIA COCAINE
Slider

Bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury amesema amekuwa akitumia Cocaine ili kumsaidia kukubiliana na matatizo ya kiakili. Bondia huyo wa Uingereza amesema kuwa amekuwa akiugua ugonjwa wa kiakili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei. Nimekuwa nje nikilewa ,Jumatatu hadi Ijumaa hadi Jumapili na kutumia Cocaine,Fury aliambia jarida la Rolling Stones. Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya Fury kudai katika mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu,kabla kukana madai hayo saa tatu baadaye akisema alikuwa akifanya...

Like
187
0
Wednesday, 05 October 2016
NIGERIA KUUZA NDEGE ZA RAIS KUPUNGUZA UBADHIRIFU
Slider

Nigeria imetangaza kwamba itauza ndege mbili zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo kama njia ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za umma. Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari, Garba Shehu, amesema ndege hizo mbili kati ya 10 zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo zitauzwa kama sehemu ya kupunguza ‘ubadhirifu’ wa serikalini. Serikali imeweka tangazo magazetini kwamba inauza ndege hizo, moja aina ya Falcon 7X na nyingine Hawker 4000. Bw Shehu amesema Rais Buhari ndiye aliyeidhinisha matangazo hayo. Ameongeza kwamba baadhi ya...

Like
186
0
Wednesday, 05 October 2016
DUTERTE ASEMA OBAMA ANAWEZA ‘KWEND JEHANAMU’
Slider

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejelea tena shutuma zake dhidi ya Rais Obama na viongozi wengine wa nchi za Magharibi wanaopinga mpango wake wa kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya. Kiongozi huyo amesema Bw Obama anaweza “kwenda jehanamu”. Umoja wa Ulaya, ambao pia umemkosoa Bw Duterte, unaweza “kuchagua kwenda eneo la kutakasia dhambi ndogo, kwa sababu jehanamu kumejaa”, amesema. Watu karibu 3,000 wameuawa tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mwezi Juni. Watu wanaoshukiwa kulangua mihadarati au kuwa...

Like
259
0
Wednesday, 05 October 2016
WACHINA WAZINDUA VYOO VILIVYOJENGWA KWA VIOO
Slider

China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani. Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo. Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani. Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi. Vyombo vya habari...

Like
295
0
Monday, 03 October 2016
UCHAGUZI DRC WAAHIRISHWA KWA MIAKA MIWILI
Slider

aarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinasema kuwa tume huru ya Uchaguzi nchini humo, imetangaza kuwa uchaguzi mkuu sasa utaandaliwa Novemba mwaka wa 2018 na wala sio mwaka huu kama ilivyotarajiwa. Viongozi kadha wa upinzani walioshiriki katika mazungumzo ya amani ya kitaifa wameafikiana na uamuzi huo, lakini kuna wale wanaoupinga wakisema ni njama ya Rais Joseph kabila kusalia...

Like
269
0
Monday, 03 October 2016