Uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa chuo cha Oxford umeonysha kuwa asilimia 10 ya watoto walioambukizwa virusi vya HIV hawapati ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutopata matibabu. Utafiti uliofanyiwa watoto 170 walio na virusi vya HIV nchini Sudan Kusini ulionyesha kuwa kinga yao ya mwili ililingana na ya nyani waliokuwa na virusi hivyo. Wataalamu wanasema kuwa ugunduzi huo ni ishara ya kwanza ya watu wanoishi na virusi vya HIV, ambao utasababisha kupatikana na tiba kwa wagonjwa wote walio na virusi hivyo....
Mahakama ya juu zaidi nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upinzani ya kupinga kutolewa sarafu mpya ya noti sawa na sarafu ya dola ya marekani, wakati nchi hiyo inapokabiliwa na hali mbaya ya uchumi tangu iache kutumia sarafu yake mwaka 2009. Mahakama ya katiba ilitoa uamuzi kuwa kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa chama cha Zimbabwe People First ,Joice Mujuru ukiitaja kuwa uvumi. “Mnadai kuwa noti hizo zitatolewa kinyume cha sheria lakini serikali imesema kuwa itafanya hivyo kuambatana na sheria,...
“Natayarisha Supu ya Mawe”, kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope kuelekea mchezo utakawakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga. Timu zote mbili zipo kambini kwa sasa kujiandaa na mchezo huo unasubiri kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka huku ukitajwa kuwa na mvuto wa kipekee, Simba imeweka kambi Morogoro, huku Yanga wakiweka kambi...
Yanga yapeleka barua TFF ikiwa na lengo la kukata rufaa kupinga klabu ya Stand United kumtumia mchezaji Frank Igobela kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa Yanga kupokea kichapo cha 1-0 kutoka Stand United, katika barua hiyo Yanga imeeleza kuwa Frank Igobela ni mchezaji halali wa Polisi ya...
Mwigizaji maarufu kutoka Marekani Brad Pitt amesikitishwa na mkewe Angelina Jolie kudai talaka na kusema watoto wasihusishwe na suala hilo. Pitt amesema amegadhabishwa na suala hilo lakini amesema kitu muhimu kwa hivi sasa ni maslahi ya watoto wake, kwa mujibu wa gazeti la Marekani la People. Jolie mwenye umri wa miaka 41 aliwasilisha ombi la kutaka talaka kutoka kwa Pitt mwenye umri wa miaka 52, kutokana na “sababu zisizoepukika” siku ya Jumatatu Wakili wa Jolie, Robert Offer, alisema Jolie alichukua...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa Hasa Mlawa. Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo inasema pamoja kutengua uteuzi wa Profesa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo. Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa...
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amelalamikia hali kwamba mshukiwa anayedaiwa kutekeleza shambulio New York Ahmad Khan Rahami alitibiwa baada ya kujeruhiwa wakati wa ufyatulianaji risasi na maafisa wa polisi Jumatatu. Aidha, amekerwa na hali kwamba mshukiwa huyo bado atapewa wakili na serikali. Mshukiwa huyo mzaliwa wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 28 amefunguliwa mashtaka matano ya kujaribu kutekeleza mauaji. Bw Trump akihutubu Fort Myers, Florida amesema hiyo si “hali nzuri” na inaashiria...
TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu. Hayo yamebainishwa Jana Jijini Dar es salaam na Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini–TCRA, Mhandisi James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasilino ulioandaliwa na shirika la kimataifa la mawasilino -ITU kwa kushirikiana na TCRA pamoja na benki kuu ya tanzania, ambao umeshirikisha washiriki 156 kutoka nchi mbalimbali duniani, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma za fedha kupitia...
Mchungaji wa kanisa moja la watu weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha Donald Trump akihutubu alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton. Mchungaji Faith Green Timmons alimkatisha BwTrump alipomshutumu mgombea huyo wa chama cha Democratic kuhusu mikataba ya kibiashara duniani. “Bw Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru kwa juhudi ambazo tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa,” amesema pasta huyo wa kanisa la Bethel United Methodist. “Aha, hilo ni jambo njema,” amemjibu mgombea huyo wa chama...
Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou. Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C. Alianza kwa kufunga bao la mapema. Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili. Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao...
Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton atarejelea kampeni zake mnamo Alhamisi, msemaji wake amesema. Mwanasiasa huyo alikuwa amepumzika kwa siku kadha ili kupata nafuu baada ya kuugua kichomi. Bi Clinton alizidiwa na nusura azirai alipokuwa anahudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 15 tangu kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi la 9/11 ambapo watu karibu 3,000 waliuawa. Aligunduliwa kuwa anaugua kichomi, ugonjwa wa mapafu ambao pia hujulikana kama nimonia, siku ya Ijumaa. Kumezuka mjadala mkali kuhusu afya yake...