93.7 EFM yajinyakulia ushindi baada ya kuwafunga kibaha veterans mabao mawili kwa moja, katika mchezo uliochezwa jumamosi ya juzi katika uwanja wa Tamco kibaha. Mechi hiyo ni baadhi ya mechi zinazoendelea baina ya EFM na timu mbalimbali za wasikilizaji wake, Kupitia kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar . Burudani haikuishia hapo, baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani ya kibaha kontena. Ilikuwa ni bandika bandua ya ngoma kali kutoka kwa Rdj’s wa 93.7 EFM na shamra shamra kutoka...
Muziki mnene bar kwa bar KIBAHA KONTENA burudani imefunguliwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Kibaha Veterans Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa TAMCO ulimzlizika kwa E-fm kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1. Kibaha Veterans ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Efm lakini goli hilo halikudumu kwani E-fm walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia mpira wa adhabu na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi kipindi cha kwanza kumalizika Katika kipindi cha pili E-fm walirudi kwa...
WANAJESHI hamsimi wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) wameagizwa kurejea nyumbani. Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendakazi. Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa Congo. Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini...
MAHAKAMA nchini Kenya imesimamisha mgomo wa walimu uliodumu kwa wiki nne na kuwaagiza walimu kurudi kazini mara moja. Jaji Nelson Abuodha wa mahakama ya kiviwanda na masuala ya wafanyakazi amesimamisha mgomo huo kwa miezi mitatu na kuwataka walimu na serikali kuunda kamati ya kutafuta suluhu katika muda wa mwezi mmoja. Aidha, ameiagiza Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kutowaadhibu walimu na kuwalipa mishahara yao kikamilifu, pamoja na...
KATIKA Kuhakikisha suala zima la uzazi salama linazingatiwa nchini ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto ,Muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania umeanzisha programu endelevu ya kushirikisha wananchi katika kupaza sauti zao kuhusu matatizo mbalimbali ya afya yanayowakumba kipindi cha uzazi na jinsi gani serikali na Asasi mbalimbali zisizo za Kiserikali zinaweza kutatua changamoto hizo. Mratibu Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania ROSE MLAY amewaambia wandishi wa habari leo, kuwa Taasisi imekuwa...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni mjini New York, ambapo wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Uganda, yanayohusu Jumuia ya Afrika Mashariki ambako Tanzania na Uganda ni wanachama . Miongoni mwa mambo ambayo viongozi hao wamezungumzia ni maendeleo ya uchimbaji mafuta katika Uganda na faida za mafuta hayo kwa Tanzania na kwa nchi zote wanachama wa...
KIONGOZI wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewaambia wanasiasa nchini Marekani kwamba wanapaswa kuwaangalia wahamiaji kama watu na sio idadi ya watu. Katika hotuba yake ya dakika 50 , kiongozi huyo wa kanisa amegusia mzozo wa wakimbizi katika bara la Ulaya wakati akielezea kuhusu madhila ya mamilioni ya wahamiaji kutoka America ya kusini ambao wanafasiri kuelekea kaskazini kutafuta maisha bora. Papa Francis ametoa wito wa ...
MFALME Salman wa Saudi Arabia ametoa agizo la kupitiwa upya kwa masuala ya hija baada ya watu zaidi mia saba kufariki kutokana na msongamano nje ya msikiti wa Macca. Watu wengine mia nane walijeruhiwa katika tukio hilo ambapo inaelezwa kuwa vifo hivyo ni vingi kutokea katika hija kwa takriban miaka ishirini na tano iliyopita. Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za mwisho katika ibada za hija.na huo ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati...
MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu. Taarifa kutoka ofisi za Bunge ambazo zilithibitisha kifo hicho zimeeleza kuwa Bunge na Serikali watasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki. Mheshimiwa Kombani amefariki dunia jana huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka...
BAKWATA imethibitisha kutokea kwa vifo vya Watanzania watano miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya waliofariki huko Minna Saudi Arabia wakati mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat , ambako kulikuwa na msongamano mkubwa uliopelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abu Bakari Zuberi Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla na Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania...
RAIS wa serikali ya mpito ya Burkina Faso aliyekuwa amepinduliwa wiki iliyopita na wanajeshi waasi, Michel Kafando, amesema kwamba sasa amerejea rasmi madarakani. Kauli hiyo ya Kafando inakuja masaa machache baada ya wanajeshi waliofanya mapinduzi hao na wale wanaoitii serikali kusaini makubaliano ya kujiepusha na ghasia katika mji mkuu...