Slider

MAELFU YA WAHAMIAJI WAWASILI UGIRIKI
Global News

MAELFU ya wahamiaji wanaendelea kuwasili Ugiriki, huku serikali ikijiandaa kwa mazungumzo ya kujadili mbinu za kukabiliana na wahamiaji wengi wanaofika katika fukwe za taifa hilo. Meli mbili zilizobeba zaidi ya watu 4,200 zilisafiri hadi bandari ya Piraeus, usiku baada ya kuondoka kisiwa cha Lesbos. Mamia ya watu, wengi kutoka Mashariki ya Kati, bado wamekwama nje ya kituo cha reli nchini Hungary, baada ya polisi kuwazuia kusafiri kuingia EU....

Like
207
0
Wednesday, 02 September 2015
ICC: NTAGANDA AKANUSHA MASHTAKA YA UHALIFU WA KIVITA
Global News

ALIYEKUWA kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, amekanusha mashtaka aliyokuwa yakimkabili ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadam, baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kimataifa ya jinai, ICC, iliyoko mjini the Haque leo. Ntaganda anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya raia mia nane na kuwabaka watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini kama watumwa wa ngono. Mashtaka yote yanahusiana na wakati alipokuwa akiongoza mapigano katika eneo la Ituri Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo...

Like
231
0
Wednesday, 02 September 2015
CCM YATANGAZA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI
Local News

MGOMBEA  mwenza  wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi.   Ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilani ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kukipa ridhaa tena Chama Cha...

Like
225
0
Wednesday, 02 September 2015
DK SHEIN AZINDUA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR
Local News

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein amezindua Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwataka wananchi wasiogope mabadiliko katika maendeleo huku akiitaka Kamisheni ya utalii kuutangaza huku akiwashawishi wageni kuutembelea mnara huo.   Katika hotuba yake kwa wananchi mara baada ya kuuzindua mnara huo Dokta Shein amesema kuwa  ni vyema  taasisi zinazoshughulika na mambo ya utalii zikafahamu kwamba hivi sasa zina kazi kubwa ya kuhakikisha mnara huo wenye mita...

Like
295
0
Wednesday, 02 September 2015
BUDAPEST: SAFARI ZA TRENI KWA WAHAMIAJI ZASITISHWA
Global News

KITUO kikuu cha reli cha kimataifa mjini Budapest leo kimeamuru kuondolewa kwa mamia ya wahamiaji wanaojaribu kupanda treni kuelekea Austria na Ujerumani. Tangazo la kipaza sauti lililotolewa hadharani limesema hakuna treni zitakazoondoka au kuwasili katika kituo hicho cha Keleti hadi hapo itakapotolewa taarifa zaidi na kwamba kila mtu alitakiwa aondoke katika kituo hicho. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP tangazo hilo linakuja baada ya wahamiaji 500 wanaume,  wanawake na watoto kujaribu kupanda treni ya mwisho kuelekea...

Like
179
0
Tuesday, 01 September 2015
ALSHABAAB YASHAMBULIA KAMBI YA AMISOM
Global News

KUNDI la wapiganaji wa Kiislamu la Al – Shabaab limeshambulia kambi ya kikosi cha walinda usalama wa muungano wa Afrika AMISOM na Kujeruhi watu wengi katika shambulio hilo. Al-Shabaab wamejisifia kuwa mmoja wa walipuajI wake wa kujitolea ameliendesha gari liliolkuwa na bomu ndani ya kambi ya Janale umbali wa kilomita 90 kutoka mji mkuu Mogadishu kisha wapiganaji wake wengine wakashambulia kwa risasi. Kwa mujibu wa Al shabaab, wanajeshi hamsini wa AMISOM wameuawa japo ripoti hizo hazijathibitishwa kutoka upande wa AMISOM....

Like
198
0
Tuesday, 01 September 2015
WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA TAARIFA YA HALI YA HEWA
Local News

WATANZANIA wametakiwa kufuatilia na kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA– ili kuepukana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali hewa.   Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo dokta Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya siku moja juu ya Elnino na kusema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huweza kuleta athari mbaya kwa jamii.   Dokta Kijazi amesema kuwa Elnino husababishwa na ongezeko la joto katika bahari ya Pasifiki...

Like
175
0
Tuesday, 01 September 2015
DK SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA
Local News

ALIYEKUWA katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo –CHADEMA- Dokta WILBROAD SLAA ametangaza rasmi kuachana na siasa isipokuwa ataendelea kuwa mtumishi wa kawaida kwa watanzania.   Dokta Slaa ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya azma yake ya kujihusisha na masuala ya kisiasa nchini kwa kipindi cha maisha yake.   Aidha katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema kuwa hata kama hatojihusisha na siasa na chama chochote cha siasa atahakikisha...

Like
250
0
Tuesday, 01 September 2015
JONJO SHELVEY AITWA KIKOSINI UINGEREZA
Slider

Jonjo Shelvey ana kila sababu ya kuikumbuka siku ya Jumapili, kwani baada ya kusaidia Swansea City kulaza Manchester United 2-1 Ligi ya Premia, alitajwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachocheza mechi za kufuzu kwa Euro 2016 dhidi ya San Marino na Uswizi. Kiungo huyo wa kati alichezea taifa mechi yake ya pekee dhidi ya San Marino miaka miwili iliyopita. Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw, aliyechezea taifa mara ya mwisho ushindi wa 3-1 dhidi ya Scotland Novemba 2014, pia...

Like
256
0
Tuesday, 01 September 2015
BOKO HARAM YADAIWA KUENEA LAGOS
Global News

MAAFISA wa Serikali nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, wanajaribu kupanua shughuli zao kutoka maeneo ya Kaskazini, yenye idadi kubwa ya Waislamu, hadi mji mkuu wa Lagos na maeneo mengine. Wakati huo huo idara ya ujasusi nchini humo imesema kuwa imewakamata takriban makamanda 20 wa kundi hilo la Boko Haram. Aidha idara hiyo imesema kuwa wapiganaji wengine wamekamatwa katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa nchi hiyo yakiwemo ya Kano, Gombe , Central Plateau, pamoja na...

Like
261
0
Monday, 31 August 2015
NJAA YAIKABILI SOMALIA
Global News

UMOJA wa Mataifa umeelezea viwago vya utapiamlo na hali ya usalama wa chakula nchini Somalia na kusema kuwa idadi ya watu ambao wanakabiliwa na ukosefu wa chakula imeongezeka kwa karibu asilimia 20 katika muda wa miezi sita iliyopita. Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa mvua na mzozo unaoendelea. Karibu theluthi moja na watu nchini Somalia wanahitaji msaada wa kibinadamu huku Watu robo milioni wameaga dunia nchini Somalia wakati njaa ilipoikumba nchi hiyo miaka minne iliyopita....

Like
204
0
Monday, 31 August 2015