KIONGOZI wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa amehudhuria kikao cha kwanza cha bunge tangu kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge june 29 mwaka huu. Hatua hiyo imewashangaza watu wengi kwa kuwa awali alipinga matokeo ya uchaguzi huo pamoja na yale ya urais wiki iliopita ambapo alijipatia asilimia 20 ya kura katika uchaguzi mkuu. Hata hivyo viti 12 kati ya 30 vya muungano wake havikuwa na wabunge huku wabunge walio watiifu kwa kiongozi mwenza Charles Nditije wakisusia kikao...
VYAMA vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo. Maadili hayo yanayohusisha Serikali,Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC- na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu dokta Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam,...
WAZIRI Mkuu wa Australia Tony Abbot amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Waziri Mkuu Abbot ametoa pongezi hizo mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Kikwete namna nchi hizo mbili zinavyoweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii. Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa...
Kocha wa zamani nchini Nigeria,Stephen Keshi anaidai shirikisho la soka nchini humo Euro milioni 3.2 kwa kufukuzwa kazi kabla ya mkataba wake kuisha. Keshi ambaye alifukuzwa kazi mwanzoni mwa July na nafasi yake kuchukuliwa na Sunday Oliseh.Aliiandikia shirikisho la soka nchini Nigeria NFF kupitia wakili wake kwa kutoa madai ya kuchafuliwa kwa kashfa na habari zisizo na ukweli. Hata hivyo msemaji wa shirikisho hilo anasema NFF haiko kwenye nafasi ya kumlipa hivyo ana uhakika shirikisho halitaweza kulipa fedha hizo kwa...
Manchester United mnamo Jumapili walithibitisha kumnunua kipa wa Argentina Sergio Romero kwa mkataba wa miaka mitatu. Mlindalango huyo wa miaka 28 atajaza pengo lililoachwa na Victor Valdes, aliyetimuliwa Old Trafford baad aya kudaiwa kukataa kucheza na timu ya akiba ya United. “Kuchezea timu kubwa zaidi duniani kwangu ni kutimia kwa ndoto,” alisema Romero kupitia taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo. “Louis van Gaal ni meneja mzuri sana na nasubiri sana kuanza kibarua hiki mpya na cha kusisimua kwenye maisha yangu...
MAJESHI ya muungano yakiongozwa na jeshi la Saudi Arabia yamesitisha mashambulizi yake ya angani nchini Yemen, baada ya kuanza muafaka wa amani wa kusitisha mapigano. Muafaka huo umeafikiwa kati ya majeshi hayo na wapiganaji wa Houthi chini ya Umoja wa mataifa, ili kuyaruhusu mashirika ya utoaji misaada kufikisha chakula na dawa kwa watu wanaothirika na mapigano hayo. Lakini vyanzo vya habari vinasema kumekuwa na mashambulizi makali ya roketi kusini mwa Yemen, hata kabla ya kuanza kwa muda huo wa kusitisha...
RAIS wa Marekani Barack Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora. Akizungumza katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika. Kwa upande wake Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia....
UKAWA umetangaza rasmi kumkaribisha waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa kuungana na Umoja huo nakusema kuwa wapo tayari kushirikiana naye na kumpa nafasi. Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR –Mageuzi Mheshimiwa James Mbatia amesema Ukawa wanamkaribisha na yuko huru kuamua chama anachotaka kuungana nacho. Tamko hili la leo limekuja baada ya kuwepo na vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya...
Mshindi wa mashindano ya baiskeli yajulikanayo kama Tour de France ,Chris Froome ameweza kushinda kwa mara ya pili tangu aingie kwenye mchezo huo. Katika mchezo wake wa mwisho huko mjini Paris mshindi huyo Froome aliweza kufanya ushindi huo uwe rahisi kwa kumaliza chini ya muda. Mwaka huu bado Froome ni mfalme wa michuano hii kwa mwaka mwisho huko mjini Paris mshindi huyo Froome aliweza kufanya ushindi huo uwe rahisi kwa kumaliza chini ya muda .Mwaka huu bado Froome ni mfalme...
RAIS wa Syria Bashar al Assad amekiri kuwa idadi ya wanajeshi wake imepungua lakini amesisitiza kuwa bado jeshi hilo lina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa makundi ya waasi. Assad ambaye aliuhutubia umma hapo jana katika mji mkuu wa Syria, Damascus pia amesema juhudi zozote za kuvikomesha vita nchini mwake ambazo hazitazingatia suala la kupambana dhidi ya ugaidi hazitakuwa na tija yoyote. Jeshi la Syria ambalo wakati mmoja lilikadiriwa kuwa na wanajeshi laki tatu limepungua kwa asilimia 50 kutokana na...
RAIS wa Marekani Barack Obama hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya kuzitembelea baadhi ya nchi za Afrika. Imeelezwa kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza tangu aongoze Taifa la Marekani akiwa rais kuhutubia wanachama 52 wa umoja wa Afrika katika makao makuu yaliyoko Addis ababa nchini Ethiopia. Hata hivyo Mazungumzo yao yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini sudan ya kusini ambapo Rais Obama amewasili nchini Ethiopia akitokea mjini...