KIONGOZI wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini Equador ambako alilakiwa na maelfu ya watu waliojitokeza barabarani jana jioni. Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kutoa hotuba 22 wakati wa ziara yake ya siku nane ambayo pia itamfikisha Bolivia na Paraguay. Mataifa hayo matatu ni miongoni mwa mataifa maskini kabisa katika bara la Amerika ya Kusini na Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 mzaliwa wa Argentina, amesema ataangazia mahitaji ya watoto, wazee, wagonjwa na...
KITUO cha Sheria na Haki za binadamu nchini –LHRC– kimeiomba Serikali kutoa elimu ya uraia katika mchakato wa katiba mpya kwa viongozi wa kimila wa mkoa wa Manyara ili waifikishe kwa jamii inayowazunguka. Mwanasheria wa kituo hicho Lengai Merinyo ameyasema hayo wakati akizungumza na jamii ya wafugaji wa kata ya Partimbo wilayani Kiteto juu ya elimu ya uraia kwa mpiga kura kuhusu katiba pendekezwa. Merinyo amesema ili kuwezesha jamii ya mkoa wa Manyara kunufaika na kuuelewa mchakato wa katiba mpya...
SERIKALI imeahidi kushirikiana vyema na sekta binafsi katika masuala ya kuinua utalii wa nchi kwa lengo la kuhakikisha Taifa linaingiza mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo. Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa MAHMOUD MGIMWA wakati akijibu swali la mbunge wa Ilala mheshimiwa Mussa Zungu aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya suala hilo. Mheshimiwa Mgimwa amesema kuwa ingawa sekta ya utalii imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi lakini serikali ipo tayari kuhakikisha...
Na Omary Katanga. Hakuna ubishi kwamba nchi yeyote duniani yenye dhamira ya kweli ya kuwa na maendeleo katika michezo, serikali ni lazima iweke nguvu yake ya fedha kwa asilimia 50 hadi 80 kusaidia mpango huo. Lakini inashangaza kuona katika nchi yetu shirikisho la mpira wa miguu TFF linalia kila kukicha kutokana na kukabiliwa na ukata wa fedha,hali inayocheleweshwa maendeleo ya sekta ya mpira wa miguu ambayo TFF inadhamana kubwa ya kusimamia. Awamu ya rais Leodiga Tenga alipokuwa TFF alianzisha wimbo...
Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amesema timu yake imepigana kufa na kupona na kucheza vizuri licha ya kutolewa na wenyeji Uganda (The Cranes) katika kinyang’anyiro cha kugombea tiketi ya kufuzu kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda. Stars imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo Jumamosi. Stars ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali...
“Argentina haikustahili kushindwa dhidi ya Chile katika mchezo wa fainali za michuano ya Copa America kutokana na timu zote kucheza sawa katika viwango” alisema kocha Gerardo Martino Chile imejishindia taji lake kubwa la kwanza kwakuitandika Argentina kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 120. katika mchezo wa uliochezwa kwa kiwango cha juu na timu hizo lakini kwa mtazamo wake anaona Argentina walistahili kutwaa taji hilo alisema Martino wakati akizungumza na vyombo vya habari...
MRENGO wa vijana kutoka chama tawala cha Afrika Kusini-ANC– Youth League umesema unapanga kufanya sherehe ya tohara ya kitamaduni kwenye milima maalum iliyopo nchini humo. Shirika la Turathi la Umoja wa Mataifa-UNESCO– limetangaza eneo hilo la “Table Mountains” kuwa turathi kwa sababu kuna mimea ya kipekee zaidi ya aina elfu tano. Taarifa ya vijana hao wa –ANC– katika jimbo la Western Cape imesema hakuna ardhi ya kufanyiwa tohara ya utamaduni ingawa bado haijabainika ikiwa watapata idhini ya kuendesha...
WATU 29 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu nchini Sudan Kusini huku wengine elfu moja wakiwa katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo. Takriban visa 484 vya ugonjwa huo ikiwemo vifo 29 ambavyo sita kati yake ni vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano idadi iliyoripotiwa mwishoni mwa mwezi Juni kutoka ofisi ya mratibu wa masuala ya kibinaadamu katika umoja wa kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo watoto elfu tano walio chini ya umri wa miaka mitano...
MKUU wa Mkoa wa Manyara dokta JOEL BENDERA amewataka raia wa nchi za kigeni wa mkoa huo kutojitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani atakayebainika atamchukulia hatua kali za kisheria. Mkoa huo unatarajia kufanya zoezi hilo la uandikishaji wa kutumia vifaa vya kielekrtoniki –BVR– kwa mwezi mmoja ambapo wapiga kura takribani laki saba na elfu hamsini wanatajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la mkoa wa Manyara. Dokta Bendera ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa...
WABUNGE wameishauri serikali kuweka muda rasmi wa kufanya uchunguzi wa makosa mbalimbali ili kuokoa ucheleweshwaji wa kutoa hukumu kwa watuhumiwa kulingana na makosa. Akichangia maoni yake leo bungeni mjini Dodoma mbunge wa Singida Mashariki mheshimiwa TUNDU LISSU amesema kuwa ni muhimu kwa serikali kuweka kipengele hicho ili kutatua changamoto za ucheleweshwaji wa kesi kutokana na uchunguzi mbovu. Naye mbunge wa ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA amewataka wabunge wa chama tawala kutotumia wingi wao katika kupitisha hoja bila kusikiliza upande wa...
Rapa The Game ambae hapo nyuma aliwahi kuwa member wa kundi la G-Unit amesema kuwa richa ya yeye kutokuwepo kwenye kundi hilo kwa sasa lakini bado anatumia mafanikio anayoyapata kifedha kutokana na kazi za kundi hilo. Akiongea wakati wa hafla ya awali kabla ya tuzo za BET kufanyika amesema “Nina dola milioni 30n mfukoni bado natumia mkwanja kutoka G-Unit richa ya kutosikika kwenye redio “. The Game amekuwa na mahusiano mabaya na boss wa kundi hilo 50 Cent nah ii...