Slider

HOFU YA KUZUKA KWA EBOLA DRC YATANDA
Global News

JUMLA ya watu wanne wamefariki dunia wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mbali na kutokea kwa taarifa za mgonjwa huyo wa Ebola Mamlaka za Afya nchini humo zimesema kuwa bado zinachunguza uwezekano wa kutokea zaidi kwa mlipuko wa ugonjwa huo. Waziri wa Afya Felix Kabange amesema wafanyakazi wa afya wamepelekwa katika kijiji cha Masambio kilichoko kilomita 270 kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo wawindaji sita...

Like
225
0
Friday, 03 July 2015
BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA
Global News

IMEELEZWA kwamba jumla ya Watu 150 wameuawa baada ya kundi la Boko Haram kuvamia na kufanya mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi ya  Nigeria. Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa mashambulizi hayo zinasema kuwa watu tisini na saba wameuawa katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad kutokana na mashambulizi hayo. Hata hivyo baadhi ya Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wamesema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wamewaua wanaume, wanawake na...

Like
192
0
Friday, 03 July 2015
MATUMIZI MABAYA YA ARDHI NI TISHIO KWA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI ZA JAMII
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora yamekuwa tishio kwa maeneo yanayozunguka hifadhi za jamii. Nyalandu ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano kati ya  Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori –WMAs– uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa. Aidha amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya hifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za...

Like
526
0
Friday, 03 July 2015
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA SHUGHULI ZA UBORESHAJI MIUNDOMBINU
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea na shughuli za uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaletea manufaa zaidi wananchi. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi dokta JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa ubungo mheshimiwa John Mnyika aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya suala hilo. Mheshimiwa Magufuli amesema kuwa kwa kiasi kikubwa serikali imekamilisha uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali na kwamba ipo tayari kuendelea na utekelezaji wa mikakati hiyo...

Like
206
0
Friday, 03 July 2015
MOURINHO: NAHESHIMU MAAMUZI  YA CECH PIA NATAMBUA MCHANGO WAKE
Slider

Mlinda mlango kutoka jamhuri ya Czech, Petr Cech’s ambae uhamisho wake umekamilika kutoka kwa mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea kwenda kukipiga katika klabu ya Arsenal uhamisho wake umeungwa mkono na meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho. Cech amekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha klabu ya Chelsea katika kipindi cha miaka 10 na baadae kuipoteza nafasi hiyo kwa mbeligiji Thibaut Courtois katika msimu uliopita na kujiunga rasmi na Arsenal hapo jumatatu. Mourinho ameeleza kuwa alipendelea kuona nyota huyo...

Like
215
0
Friday, 03 July 2015
STARS IPO KAMILI KUKIPIGA NA CRANES
Slider

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeondoka nchini mwao kuelekea Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya jumamosi. Kikosi cha Taifa Stars kimeaondoka kikiwa na wachezaji 20,na viongozi 7 wa bechi la ufundi,Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo. Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana...

Like
247
0
Friday, 03 July 2015
UHURU KENYATTA ACHAGULIWA KAMA RAIS BORA BARANI AFRIKA MWAKA HUU
Global News

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amechaguliwa na muungano wa wanafunzi wa Vyuo vikuu barani Afrika- AASU kama rais bora barani Afrika mwaka huu. Muungano huo unasema kuwa maelfu ya wanafunzi kutoka kote barani walishiriki katika kura hiyo. Kenyatta alichaguliwa kwa uwezo wake wa kujenga makubaliano kitaifa na kimataifa, juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa ufumbuzi katika maswala yanayowaathiri wakenya. Rais wa Rwanda Paul Kagame alishinda tuzo kama hiyo mwaka...

Like
168
0
Thursday, 02 July 2015
SERIKALI YAOMBWA KUCHUNGUZA WANAOJINUFAISHA NA HARAMBEE ZA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI
Local News

SERIKALI kupitia vyombo vya ulinzi na Usalama vimeombwa kuchunguza  Asasi, Taasisi, Mashirika na watu binafsi wanaotumia mwamvuli wa matatizo ya watu wenye ulemavu wa ngozi kujinufaisha kwa kufanya harambee mbalimbali. Katibu wa Chama cha Maalbino Wilaya ya Temeke Gaston Mcheka ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kile alichodai kuchoshwa na tabia ya baadhi ya watu kukusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia albino na badala yake kutokomea pasipo walengwa...

Like
195
0
Thursday, 02 July 2015
JAMII YAOMBWA KUWA NA MAZOEA YA KUPIMA AFYA
Local News

JAMII imeombwa kuwa na mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara  hususani kwa Watoto ilikuweza kutambua matatizo au magonjwa ya moyo mapema kwakuwa idadi inonesha katika watoto milioni moja na laki saba waliozaliwa mwaka 2014 asilimia 1 mpaka 2 ya watoto hao sawa na watotoelf 13 na mia 6 wanamagonjwa ya moyo mbalimbali. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam wakati wakutiliana saini mkataba wa makubaliano maalum kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi binafsi ya misaada ya...

Like
253
0
Thursday, 02 July 2015
SPIKA AHAIRISHA BUNGE KUFUATIA KUTOELEWANA BAADHI YA WABUNGE
Local News

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa ANNE MAKINDA amelazimika kuahirisha kikao cha bunge kabla ya wakati kufuatia Muongozo ulioombwa na mbunge wa Ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA juu ya kubadili mfumo wa uwasilishwaji na upitishwaji wa miswada ambayo bado haijawasilishwa hali iliyosababisha kutoelewana kwa wabunge wa chama tawala na wabunge wa vyama vya upinzani. Hali hiyo imekuja baada ya wabunge wa vyama vya upinzani kuonesha hali ya kuonewa kwa madai kuwa hawapewi nafasi ya kutosha katika kujadili...

Like
259
0
Thursday, 02 July 2015
KURA YA MAONI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA KIUCHUMI UGIRIKI
Global News

WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amesisitiza kura ya maoni aliyoitisha  siku ya Jumapili wiki hii itaamua hatma ya mgogoro wa kiuchumi unaoikumba nchi yake. Mawaziri wa fedha wa kanda inayotumia sarafu ya euro waliokutana hapo jana wamesema hawatafanya mkutano mwingine wa kuzingatia maombi yoyote mapya ya kuipa nchi hiyo mkopo wa uokozi hadi kura hiyo ya maoni itakapofanyika. Tsipras amesema kura ya kupinga masharti magumu ya wakopeshaji wa Ugiriki haimaniishi nchi hiyo inajiondoa kutoka Umoja wa Ulaya bali ni...

Like
201
0
Thursday, 02 July 2015