KUPITIA mradi wa gesi wa kuongeza sifa za kuajiriwa kupitia mafunzo ya ufundi stadi, Chuo cha mafunzo na ufundi stadi –VETA, kimetoa nafasi ya mafunzo ya gesi kwa wanafunzi wa vyuo hivyo ili kuweza kuongeza wataalamu zaidi katika sekta hiyo. Akizungumza na efm, mwalimu wa taaluma ya umeme chuo cha ufundi veta Lindi, MAJOLE MWIGOLE amesema kuwa wameamua kuweka mafunzo hayo ili vijana wengi waweze kuingizwa katika sekta hiyo na kuepuka kuchukua wataalamu kutoka...
SERIKALI imelitaka Shirikala la Umeme nchini-Tanesco kuhakikisha linafuatilia mita zenye matatizo hususani za luku, ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao na kuwafungia mita zinazofanya kazi. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage wakati akijibu swali la mheshimiwa Diana Chilolo, Mbunge wa Viti Maalum, katika kipindi cha maswali na majibu. Katika swali lake Mheshimiwa Chilolo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mita mpya ambazo...
TAKRIBAN watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta mji mkuu wa Ghana –Accra. Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makazi. Taarifa zinasema kuwa mafuriko huenda yalisababisha moto ambao ulitokea jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa...
CHINA imeitaja Marekani kuwa imekosa kuwajibika kwa kudai kuwa wadukuzi wa china ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi ya serikali ya Marekani. Wizara ya mambo ya nje ya china imesema ni vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi wowote wa kisayansi haitasaidia. Shirika la ujasusi la –FBI- nchini Marekani linachunguza namna wadukuzi wa komputa walivyoweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne...
IMEELEZWA kuwa migogoro ya Ardhi hapa Nchini inasababishwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji wasiokuwa na uelewa mpana kuhusu maswala ya sheria na utaratibu wa ugawaji ardhi. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwemwekiti wa Jukwaa la Ardhi Tanzania Docta STEPHEN MUNGA amesema kuwa suala la migogoro ya ardhi limekuwa ni changamoto kubwa katika jamii hususani ya wakulima na wafugaji ambao wamekuwa na madai ya mara kwa mara katika maeneo yao. MUNGA ameongeza kuwa...
WIZARA ya Maji imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 455, milioni 900 laki 9 na elfu 81 kwaajili ya kuboresha utekelezaji wa miradi ya maji katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2016. Akiwasilisha makadilio ya matumizi ya wizara, waziri wa wizara hiyo Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia kurahisisha ukamilishaji wa miradi hiyo ambapo kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 17 zitatumika kwaajili ya mishahara. Kwa upande wake kamati ya kudumu ya bunge...
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili. Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi. Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki. Sterling amekataa ombi la kitita cha...
SERIKALI ya marekani imekumbwa na udukuzi mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa. Ofisi ya Utumishi ya nchini hiyo inasema karibu ya watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo. Taarifa zote za udakuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika lakini Afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa....
SEREKALI imetakiwa kuangalia upya sheria ya mtoto ya mwaka 1971 kwani imebainika kuwa ni chanzo kimojawapo kinachoruhusu uwepo wa ndoa na mimba za utotoni. Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na shirika la intiative for youth –INFOY– mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya ya Arusha HASSANI OMARY amesema kuwa ni wajibu wa serekali kuangalia upya sherika hiyo kwani imekuwa ikiwaathiri watoto wengi hapa nchini. Amesema kuwa sheria hii imekuwa ikiruhusu watoto hata wenye umri chini ya miaka 18 kuolewa iwapo...
IMEELEZWA kuwa rais mpya ajaye nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja na Amani kwani Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili. Kauli hiyo imetolewa na rais Jakaya Kikwete jijini Stockholm – Sweden ambapo alikuwa akiongea na watanzania waishio Sweden mara baada ya kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku 3, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Juni, mwaka huu. Watanzania mbalimbali walioko nchini Sweden kwa ajili ya shughuli za kikazi,...
WANAJESHI watano wa Ukraine wameuawa katika mapigano karibu na mji unaoshikiliwa na serikali wa Maryinka, ambako waasi wanaoipendelea Urusi wakijaribu kusonga mbele. Msemaji wa Ikulu mjini Kiev Yuri Biryukov, amesema kuwa katika ukurasa wake wa Faceboock, kwamba raia 39 wa Ukraine wamejeruhiwa katika mapigano hayo. wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema kwamba waasi wanaotaka kujitenga, wakitumia vifaru na mizinga walijaribu kuviteka vituo vya serikali karibu na Maryinka, mashariki mwa mji unaoshikiliwa na waasi wa Donetsk, ikiwa ni...