Slider

AZMA YA ZITTO KUJIUZULU UBUNGE YAGONGA MWAMBA
Local News

AZMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ,KABWE ZITTO kupitia CHADEMA,ya kutaka kujiuzulu Ubunge imegonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa Spika wa Bunge ,ANNE MAKINDA amemzuia,kufanya hivyo. ZITTO ambaye alikuwa ameshafanya maandalizi ya kuaga Bunge March 19 ndani ya Bunge,amejikuta akigonga mwamba dakika za mwisho baada ya kuingia Bungeni na kuelezwa na mmoja wa Maofisa wa Bunge kuwa, suala lake la kutoa hotuba limeahirishwa na Spika MAKINDA, akitakiwa kwanza kuifanyia marekebisho. Kabla kuingia Bungeni,ZITTO alikuwa akibadilishana mawazo na...

Like
230
0
Friday, 20 March 2015
ANDY MURRAY ATANGAZA NDOA
Slider

Huenda mwaka wa 2015 ukawa na kumbukumbu nzuri katika maisha mcheza tennis  Andy Murray kufuatia mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake Kim Sears April mwaka huu. Mchezaji huyo raia wa Scotland amerejea katika nafasi ya nne duniani baada ya awali kuporomoka kutokana na upasuaji wa mgongo aliofanyiwa. Furaha ya mchezaji huyo inachagizwa zaidi kutokana na rekodi mpya aliyojiwekea baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya Indian Wells yanayoendelea huko California...

Like
296
0
Friday, 20 March 2015
LOUIS VAN GAAL ATANGAZA KUSTAAFU ATAKAPOMALIZA KUITUMIKIA MANCHESTER UNITED
Slider

Meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ametangaza kustaafu soka atakapomaliza kuitumikia Man U. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 63 anamkataba wa kuinoa Manchester United hadi mwaka 2007 baada ya kujiunga na klabu hiyo kwenye msimu wa kiangazi. Van Gaal ambae ni raia wa Uholanzi amesema hanampango wa kuendelea na fani hiyo kwani anahitaji kuutumia muda wake na familia yake Kocha huyu amewahi kuzinoa timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Barcelona, Bayern Munich na Ajax Akizungumza kwenye mahojiano...

Like
294
0
Friday, 20 March 2015
CHINA NA JAPAN KUFANYA MKUTANO WA KWANZA WA KIWANGO CHA JUU CHA USALAMA
Global News

CHINA na Japan wanafanya mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu wa usalama katika muda wa miaka minne. Mkutano huo unaofanyika Tokyo unajumuisha maafisa kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi ambapo mazungumzo hayo yalisitishwa mnamo mwaka 2011 kutokana na hofu kuhusu visiwa vinavyozozaniwa Mashariki mwa bahari ya China. Pande zote zimesisistiza umuhimu wa mazungumzo ya kweli kudumisha amani....

Like
288
0
Thursday, 19 March 2015
RAIS WA TUNISIA ATANGAZA VITA DHIDI YA UGAIDI
Global News

RAIS wa Tunisia, Beji Caib Essebsi, amesema nchi yake imo vitani na ugaidi baada ya wanaume waliojihami kwa bunduki kuwaua watalii wa kigeni wapatao 17 na raia wawili katika shambulio lililotokea kwenye makazi mjini Tunis. Kiongozi huyo amesema nchi yake itakabiliana vikali na alichokitaja kama makundi madogo ya kishetani. Washambuliaji hao waliwapiga risasi wageni kutoka Japan, Colombia, Australia, Italia na Uhispania kabla ya kuuawa na maafisa wa...

Like
308
0
Thursday, 19 March 2015
HALI YA MIFUMO YA VYOO DAR NI HATARI
Local News

IMEELEZWA kuwa licha ya kuwa na mazingira duni ya vyoo jijini karibia  asilimia 99 ya wakazi wa Dar es salaam  wana vyoo lakini ni asilimia 10 tu ya wakazi hao ambao vyoo vyao vimeunganishwa na mfumo wa kupitisha au kutoa maji taka. Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano uliokutanisha serikali, wadau, Taasisi na Asasi za kiraia kujadili hali halisi ya masuala ya usafi wa mazingira ya vyoo na kuangalia hali ya mtandao wa maji taka na njia...

Like
206
0
Thursday, 19 March 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUDHIBITI MATUMIZI YA SILAHA
Local News

KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kusimamia ipasavyo sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha nchini ili kuimarisha usalama wa wananchi pamoja na kukomesha matukio hatarishi yanayoleta taswira mbaya kwa Taifa. Akitoa taarifa rasmi ya kambi hiyo leo Bungeni mjini Dodoma mbunge wa Arusha Mjini mheshimiwa GODBLESS LEMA amesema kuwa ili wananchi wanufaike na sheria mbalimbali zinazopitishwa ni vyema kwa serikali kuzisimamia kwa haki na usawa pasipo kupendelea upande wowote. Awali akiwasilisha muswada wa sheria ya kudhibiti matumizi...

Like
216
0
Thursday, 19 March 2015
FDLR WATOA VITISHO KWA WAJUMBE WA MASHIRIKA YA KIRAIA
Global News

WAJUMBE wa Mashirika ya Kiraia wa vijiji vya Tama na Itala Kusini mwa tarafa ya Lubero Jimboni Kivu Kaskazini, wametishwa na kundi la Waasi wa Kihutu kutoka Rwanda-FDLR wanaoongozwa na Kanali KIZITO. Vitisho hivyo vimekuja kutokana na uchapishaji wa Ripoti ya Mashirika ya Kiraia katika Sekta hiyo. Baadhi ya Wanachama wa Vyama vya Kiraia katika Vijiji vya Tama na Itala wamesema, raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali ya maficho kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi wanaoishi...

Like
201
0
Thursday, 19 March 2015
BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA UDHIBITI WA AJIRA ZA WAGENI
Local News

BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine umeainisha vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa. Hata hivyo Bunge hilo limesisitiza Serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini uwezo kuhusu ajira wanazoomba na mienendo yao kijamii. Sheria hiyo pia inawataka Wananchi kuwepo katika ajira zote kutokana na sifa...

Like
182
0
Thursday, 19 March 2015
SUMAYE: ELIMU INAYOHITAJIKA INATOA MAJIBU KWA MATATIZO KATIKA JAMII
Local News

WAZIRI Mkuu Mstaafu,FREDERICK SUMAYE,amesema Elimu inayohitajika Kipindi hiki, inatoa majibu kwa matatizo katika jamii. SUMAYE ameeleza hayo mjini Dodoma alipokuwa akifungua Mkutano wa Mwaka wa Chama Cha Wenye Shule na Vyuo Binafsi Tanzania-TAMONGSCO. Amebnainisha kuwa Elimu lazima impe mhusika uwezo wa kumudu Mazingira ya sasa ambayo yanabadilika kwa kasi na inayomza mwanafunzi maarifa yaliyovumbuliwa na...

Like
277
0
Thursday, 19 March 2015
WANAFUNZI WATAKIWA KUEPUKA VITENDO VITAKAVYOSABABISHA KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU
Local News

WANAFUNZI wametakiwa kujiepusha na Vitendo vitakavyosababisha kupata Maambukizi ya Virus vya UKIMWI-VVU na Mimba za Utotoni,hivyo kuwafanya wakatize masomo na kutotimiza ndoto za maisha yao. Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC ya CCM,Mama SALMA KIKWETE, alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkonge mkoani Lindi. Mama SALMA KIKWETE,amesema kuna baadhi ya Wanafunzi wanajiingiza katika Mapenzi kabla ya wakati na kufanya hivyo wanakumbana na Mimba za Utotoni na UKIMWI....

Like
610
0
Thursday, 19 March 2015