Slider

CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YA MAGOLI LIGI YA MABINGWA
Slider

 Ronaldo avunja rekodi ya magoli kwenye ligi ya mabingwa ambapo mshambuliaji huyo alishinda mabao mawili kwenye mechi ya jana na kufikisha idadi ya magoli 78. Klabu ya real Madrid hapo jana ilipokea kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Schalke kwenye uwanja wa nyumbani. Aidha Cristiano Ronaldo ambae ni mchezaji wa kimataifa kutoka Ureno ameapa kutozungumza chochote kwenye hadhara hadi mwisho wa msimu wa ligi hiyo   10 BORA WANAOONGOZA IDADI YA MAGOLI BARANI ULAYA PAMOJA NA UEFA SUPER CUP  ...

Like
428
0
Wednesday, 11 March 2015
VENEZUELA YAMUONDOA BALOZI WAKE WASHINGTON KUFUATIA VIKWAZO DHIDI YA MAAFISA WAKE
Global News

Venezuela imesema imemuita balozi wake mjini Washington MAXIMILIEN SANCHEZ arejee nyumbani baada ya vikwazo vya Marekani dhidi ya maafisa wake. Rais wa Venezuela NICOLAS MADURO ameikosoa vikali Marekani kwa kuwawekea vikwazo maafisa wa Venezuela wanaoshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu, akisema ataliomba bunge limpe mamlaka zaidi kupambana na kitisho cha...

Like
249
0
Tuesday, 10 March 2015
ANGELA MERKEL AITAKA JAPAN KUTAFUTA UFUMBUZI WA TUHUMA ZA WANAJESHI KUJIHUSIHA NA UTUMWA WA NGONO
Global News

KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL ameitaka Japan kuutafutia ufumbuzi mzozo unaohusiana na mfumo wa nchi hiyo wa utumwa wa ngono wakati wa vita. Akikamilisha ziara yake nchini Japan ,MERKEL amekutana na KATSUYA OKADA, Mkuu wa Chama cha Upinzani cha Democratic na kusema, Japan inatakiwa kuendelea mbele na juhudi za maridhiano na Korea Kusini. Kwa mujibu wa takwimu rasmi wanahistoria wanasema hadi Wanawake 200,000 wengi kutoka Korea, China, Indonesia, Ufilipino na Taiwan, waliwatumikia wanajeshi wa Japan katika madanguro ya...

Like
515
0
Tuesday, 10 March 2015
ASILIMIA 1.03 YA WATANZANIA HUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UGONJWA WA FIGO
Local News

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Figo-NESOT pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya na Magonjwa ya Figo, imeeleza kuwa Ugonjwa wa Figo wa Mstuko  na Ugonjwa Sugu wa Figo ni tatizo mojawapo kwenye kundi la magonjwa yasiyoambukiza ambayo mchango wake katika kuongeza athari za Kiafya na Vifo Ulimwenguni unaongezeka siku hadi siku. Akizungumza na Waandishi wa Habari  jijini Dar es salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo, Dokta JACKLINE SHOO amesema Tanzania ni nchi...

Like
262
0
Tuesday, 10 March 2015
CHADEMA YAMVUA RASMI UANACHAMA ZITTO KABWE
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Leo kimemvua Rasmi Uanachama aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa ZITTO KABWE kwa madai ya kushindwa kutekeleza Masharti ya Katiba ya chama hicho.   Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Mheshimiwa TUNDU LISU amesema kuwa, mnamo mwaka jana Mheshimiwa ZITTO alifungua Mashitaka katika Mahakama Kuu akizuia vyombo vya Chama kukaa kujadili na kufanya maamuzi yanayohusu yeye kuendelea kuwa Mwanachama wa Chama hicho. Amesema kuwa katika kipindi...

Like
326
0
Tuesday, 10 March 2015
NICK CANNON: MARIAH CAREY ANAUZA NYUMBA BILA KUNISHIRIKISHA
Entertanment

Nick Cannon adai aliekuwa mkewe Mariah Carey hakumuhusisha na jambo lolote kwenye mjadala wa kuuza nyumba. Nick ameeleza kuwa meneja wao anaehusika na mambo yote ya kibiashara ndie alikuwa kinara wa kuongoza hatua zote muhimu katika uuzwaji wa nyumba hiyo ya kifahali na kumuweka kizani kwa asilimia mia moja kwa kutomfahamisha chochote kwa mujibu wa Nick. Kwa mujibu wa chombo cha kusimamia sheria Cannon amesema hakuidhinisha jumba hilo la kifahari kuuzwa kwa dola milioni 9 za kimarekani, nyumba ambayo Nick...

Like
304
0
Tuesday, 10 March 2015
ROY KEANE: VAN GAAL APEWE MUDA KUKIJENGA KIKOSI IMARA
Slider

Aliekuwa Captain wa Manchester United Roy Keane ameesema ni janga kubwa kwa klabu hiyo kushindwa kumaliza hatua ya nne bora ila anaamini kuwa meneja wa sasa wa timu hiyo Louis van Gaal anahitaji muda wa takribani miaka miwili ama mitatu kukijenga kikosi hicho. Ndoto za klabu hiyo kwenye michuano ya FA zilifutika hapo jana baada kupokea kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Arsenal katika robo fainali za michuano hiyo Keane ameeleza kuwa si jambo la kushangaza...

Like
272
0
Tuesday, 10 March 2015
MAREKANI YATANGAZA KUTUMIA WANAJESHI 3000 KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIJESHI YA NATO
Global News

MAREKANI imetangaza kutuma wanajeshi 3,000 kwenye mataifa ya Baltic kushiriki mazoezi ya Kijeshi na Washirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Tangazo lililotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani,limesema mazoezi hayo yatazijumuisha Estonia, Latvia na Lithuania, na yatakuwa ya miezi...

Like
293
0
Tuesday, 10 March 2015
UKRAINE: WAASI WAONYESHA DHAMIRA YA KUSITISHA MAPIGANO
Global News

RAIS PETRO POROSHENKO wa Ukraine amesema kwamba waasi wanaotaka kujitenga Mashariki mwa nchi yake wameondoa kiwango kikubwa cha silaha nzito kutoka mstari wa mbele wa mapambano, hali inayoashiria kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. Akizungumza na Televisheni ya Taifa ya Ukraine Bwana POROSHENKO Amesema kuwa kila upande, kati ya Wanajeshi wa Serikali na Waasi, umeondoa silaha kwenye uwanja wa...

Like
209
0
Tuesday, 10 March 2015
BABATI: HAMASHAURI YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 39 KWA VIJANA NA VIKUNDI 5 VYA WANAWAKE
Local News

HALMASHAURI ya WIlaya ya Babati Mkoani Manyara,imekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 39 kwa kikundi cha Kuweka na Kukopa cha Vijana SACCOSS na vikundi vitano vya Wanawake 150. Akikabidhi hundi hizo Katika Kijiji cha Ayasanda,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo NICODEMUS TARIMO,amesema fedha hizo zinatokana na Asilimia 10 ya Mapato ya Halmashauri kwa ajili kuwawezesha Vijana na...

Like
247
0
Tuesday, 10 March 2015
CCM YARIDHISHWA NA JK KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA
Local News

CHAMA cha Mapinduzi-CCM kimeonyesha kuridhishwa na harakati za Mwenyekiti wake Rais JAKAYA KIKWETE,Katika kutekeleza Ilani yao juu ya ushirikishwaji wa Wanawake katika Uamuzi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, ABDULRAHMAN KINANA katika Ziara yake ya kuangalia Utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita katika Kijiji cha Mageleko. KINANA amesema amezunguka sehemu kubwa ya mkoa huo na kukuta nafasi nyingi za juu zikishiliwa na Wanawake hali inayoonyesha kuwa Utekelezwaji wa Ilani ya CCM umeafanikiwa kwa kiasi...

Like
242
0
Tuesday, 10 March 2015