BALOZI wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akipiga kelele kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao. Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi. Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa...
JAMII nchini imetakiwa kushirikiana na Serikali katika kudhibiti tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kuanzia ngazi ya Familia kwakuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji wa kata ya Temeke Elias Wawa amesema kuwa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya linaanzia katika ngazi ya familia hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuzungumza na vijana wao ili kuondokana na tatizo hilo . Aidha amewataka wazazi kutowakatisha tama...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 38 huku wengine 82 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia jana tarehe 4 Machi, mwaka huu. Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mwakata iliyoko katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, hivyo kuathiri watu 3,500. Katika Kata Mwakata iliyoathiriwa zaidi, kaya 350 zimeathiriwa...
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 44 amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 75 jela nchini Kenya Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya watoto ya Nakuru baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki mapenzi na mototo wake mwenye umri wa miaka 12 na kumuambukiza virusi vya...
MEYA wa mji wa Ferguson, jimboni Missouri, ametangaza hatua zitakazochukuliwa kufuatia ripoti iliyoonyesha ushahidi dhidi ya polisi wa mjini humo kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi. Meya JAMES KNOWLES amesema mwajiriwa mmoja toka Idara ya Polisi amefukuzwa kazi na wengine wawili wamelazimishwa kwenda likizo baada ya kushutumiwa kutuma barua pepe yenye ujumbe wa kibaguzi. KNOWLES amewaambia Waandishi wa Habari kuwa Idara itaongeza namba ya Maafisa wasio wazungu na kujikita...
MVUTANO kati ya Serikali ya Kenya na vyombo vya habari kuhusu kuhamia mfumo wa Digitali kutoka Analogia ambao umesababisha Vituo vinne vikubwa vya Televisheni nchini humo kutorusha matangazo hivi sasa umeisha. Vituo hivyo mfumo wake wa Analogia ulizimwa,vitaanza kurusha matangazo yake tena. Makubaliano hayo yamefikiwa March 03 mwaka huu kati ya Serikali na Vituo hivyo vikubwa vya Televisheni nchini Kenya NTV, QTV, KTN na Citizen TV ambavyo vimekubaliwa kurusha matangazo yao jijini Nairobi chini ya Mtandao wa Africa Digital Networks...
BAADHI ya Wajawazito katika Kata ya Tinde,Halmashauri ya Wilaya Shinyanga wamewalalamikia wahudumu wa Kituo cha Afya Cha Tinde, kuwadai fidia na kuzuia kadi za Kliniki. Wahudumu hao baada ya kuwapima wajawazito ,hudai shilingi 2000 kwa kila Mjamzito.Wakizungumza na Efm kituoni hapo,baadhi ya wajawazito wamesema tabia hiyo ni ya siku nyingi na imekuwa ni kero...
SERIKALI ya China imetoa Zaidi ya Shilingi Milioni 265 kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi ya Maji mkoani Tabora. Akiwasilisha taarifa yake katika kikao cha Kamati ya Bunge jijini Dar es salaam,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi MBOGO FUTAKAMA amesema pesa hizo zimetolewa kwa ajili Mkoa wa Tabora ambao una matatizo ya upatikanaji wa Maji. Ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika katika miradi mbalimbali katika mkoa huo na Wilaya zake ili kuboresha Miundombinu na hatimaye kupatikana kwa...
Klabu ya Arsenal hapo jana imefanikiwa kujinususru na balaa la kuondolewa kwenye michuano ya Champions ligi kwa ushindi wa magoli mawili ndani ya dakika tano kwenye mchezo kati yao na QPR huko katika viwanja vya Loftus Road siku ya jana ambapo mechi hiyo ilimalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa 2-1 Kocha wa timu ya Arsenal alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupoteza mchezo kati yao na Monaco baada ya kupokea kichapo lakini kwa ushindi huo wa jana unaiweka klabu...
WATU wawili raia wa Australia waliopatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevywa wamehamishwa kutoka jela mjini Bali nchini Indonesia leo na kupelekwa katika kisiwa kimoja nchini humo ambako watauwawa kwa kupigwa risasi. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Australia, hatua hiyo ya adhabu ya kifo kwa Myuran Sukumaran na Andrew Chan imeongeza wasiwasi wa kidiplomasia, huku kukiwa na maombi ya msamaha kwa watu ...
RAIS Barack Obama wa Marekani, ametupilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la Marekani. Rais Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza silaha za Nuclear. Waziri Mkuu Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari . ...