Slider

18 MBARONI VURUGU ZA ILULA
Local News

SIKU moja baada ya kuibuka kwa vurugu kubwa kati ya Askari Polisi na Wananchi wa Kijiji cha Ilula Kilolo Mkoani Iringa watu 18 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na tukio hilo. Vurugu hizo zimeibuka February 24 mwaka huu baada ya mwanamke mmoja kudaiwa kuuawa na askari Mkoani Iringa wakiwa doria kwa lengo la kuwakamata watu wanaokunywa pombe kabla ya muda huo kufika. Wakati Askari watano wakiwa wamejeruhiwa kwenye tukio hilo wananchi wawili pia wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali...

Like
820
0
Thursday, 26 February 2015
SERIKALI YAWASHAURI WAFUGAJI NCHINI KUJIENDELEZA
Local News

SERIKALI imesema inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya Tume Maalum iliyoundwa na Bunge kushughulikia mgogoro kati ya Wakulima na wafugaji. Aidha, imewataka Wafugaji kuacha Mila na Desturi zilizopitwa na wakati za kufuga mifugo mingi pasipokuwa na tija, wakati maisha yao yakiendelea kuwa duni. Akizungumza Mkoani Mbeya Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA amesema kutoelewa kwa makundi hayo mawili kumesababisha uvunjifu wa amani mara kwa...

Like
259
0
Thursday, 26 February 2015
UEFA: MONACO YAILAZA ARSENAL 3-1
Slider

Matumaini ya Arsenal kufikia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza toka mwaka 2010 yanakutana na vikwazo mara baada kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Monaco katika uwanja wao wa nyumbani huko Emirates Meneja wa timu ya Arsenal ametupia lawama kwa wachezaji wake kwa kusema kuwa kiakili hawakuwa wamejiandaa kwenye mchezo huo baada ya kuruhusu magoli yaguse mlango wao kutoka kwa Geoffrey Kondogbia, Dimitar Berbatov na Yannick Ferreira Alex Oxlade aliipatia bao Arsenal lililodumu...

Like
385
0
Thursday, 26 February 2015
UINGEREZA YAWA NCHI YA KWANZA KUPITISHA SHERIA HII YA DNA
Global News

UINGEREZA imekuwa nchi ya kwanza kuidhinisha sheria itakayoruhusu uzaaji wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwanamume mmoja. Sheria hiyo ilioimarishwa imepita kikwazo chake cha mwisho baada ya kuidhinishwa na bunge la taifa hilo. Sheria hiyo sasa itadhibiti utoaji wa leseni kwa wanaotaka kutengeneza watoto hao kwa lengo la kuvilinda vizazi hivyo kutorithi magonjwa mabaya. Mtoto wa kwanza huenda akazaliwa kabla ya mwaka 2016....

Like
255
0
Wednesday, 25 February 2015
AMNESTY YATAKA KURA YA VETO ITUMIKE KUFUATIA MAUAJI YA HALAIKI
Global News

SHIRIKA la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limetoa wito kwa Wanachama watano wa kudumu wa Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kutumia kura yao ya Veto kwa maswala yahusuyo mauaji ya halaiki. Shirika hilo limesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiweka maslahi ya nchi mbele kuliko maswala ya haki za binaadam. Katika Ripoti yake ya mwaka, Amnesty International imesema mwaka 2014 ulikuwa mwaka wenye matukio mabaya kwa mamilioni ya Watu waliokuwa kwenye maeneo yenye migogoro, na kusikitishwa na...

Like
363
0
Wednesday, 25 February 2015
ESCROW: CHENGE APANDISHWA KIZIMBANI
Local News

MBUNGE wa Bariadi Magharibi kupitia chama cha Mapinduzi -CCM, Andrew Chenge amepandishwa kizimbani  kwa madai ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi,  jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo. Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungu hivyo vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni pamoja na alipokuwa  Mtumishi  mkuu wa serikali kwa  wadhifa wa mwanasheria...

Like
341
0
Wednesday, 25 February 2015
JK AANZA ZIARA ZAMBIA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo kuelekea Lusaka Zambia kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Edgar Chagwa Lungu wa Nchi hiyo. Viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi ikiwemo suala la reli ya Tanzania na Zambia Railway Authority (TAZARA), inayounganisha Tanzania na Zambia. Hivi karibuni Reli ya TAZARA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitajika kujadiliwa kwa kina na viongozi...

Like
243
0
Wednesday, 25 February 2015
VIDEO: FAHAMU KIPAJI KINGINE CHA ADEBAYOR MBALI NA KUSAKATA KABUMBU
Slider

Kama ukiulizwa orodha ya wachezaji wa mpira wa miguu barani Afrika wenye uwezo wa kucheza na mapenzi ya muziki pia basi bila shaka hutomsahau Emmanuel Adebayor. Richa ya uwezo wake wa kusakata kabumbu Adebayor pia ni dancer mzuri saana katika kulithibitisha hili tazama hii video Mchezaji huyo ambae ni raia wa Togo kwa sasa anaichezea klabu ya Tottenham Hotspur klabu ya ligi kuu ya Uingereza Mchezaji huyo pia aliwahi kuchezea Monaco, Arsenal, na Manchester City...

Like
343
0
Wednesday, 25 February 2015
AMNESTY YAKOSOA SERIKALI ULIMWENGUNI KUSHINDWA KUWALINDA RAIA
Global News

SHIRIKA la haki za binaadamu la Amnesty International limezikosoa serikali ulimwenguni kwa kushindwa kuwalinda mamilioni ya raia dhidi mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola na makundi yenye silaha. Ripoti ya kila mwaka iliyochapishwa leo na shirika hilo inaelezea hatua ambazo zimechukuliwa na ulimwengu dhidi ya migogoro nchini Nigeria na Syria kuwa ni za kutia aibu. Amnesty International inayalaumu mataifa tajiri duniani kwa kutumia nguvu na fedha nyingi kuwazuia watu kuingia kwenye mataifa hayo, kuliko kuwasaidia watu kuishi....

Like
228
0
Wednesday, 25 February 2015
NIGERIA: 30 WAUAWA KWA MASHAMBULIZI KWENYE VITUO VYA MABASI
Global News

TAKRIBANI watu 30 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika vituo vya mabasi kaskazini mwa Nigeria. Katika mashambulizi ya kwanza, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alikimbia basi lililosheheni abiria katika mji wa Potiskum, ambapo alijiripua na kuwauwa watu 16 pamoja naye. Rais Goodluck Jonathan amesema kundi la Boko Haram linahusika na mashambulizi yote mawili. Katika taarifa nyengine, majeshi ya Chad yanayoshiriki vita dhidi ya Boko Haram, yanaripotiwa kuwauwa wanamgambo 207 kwenye mji wa mpakani mwa Nigeria na...

Like
261
0
Wednesday, 25 February 2015
SIDO YAWATAKA WATANZANIA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI
Local News

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya amesema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja. Amesema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi, zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na...

Like
405
0
Wednesday, 25 February 2015