KAMISHINA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SULEIMAN KOVA ametoa agizo kuchunguza tuhuma za askari wake wanaodaiwa kugawana fedha shilingi milioni Nane ambazo zilikuwa Mali za Akina Mama Wajasiriamali waliojiunga kwenye vikoba. KOVA ameeleza hayo jijini Dar es salaam na kusema kuwa tuhuma hizo amezesikia lakini hawezi kumhukumu mtu hivyo ametoa agizo kuwa uchunguzi ufanyike. Amebainisha kuwa endapo uchunguzi utafanyika na kubaini kuwa askari au mtu yoyote amehusika kuchukua fedha hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni...
Kwa misimu saba mfululizo Barcelona wameifikia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya wakati klabu ya Manchester City haikuwahi kufikia hatua hiyo kwenye historia yake. Katika mchezo uliochezwa hapo jana na kumalizika kwa Barcelona kuichapa Manchester City 2-1 Luis Suarez aliziona nyavu mara mbili kwenye ardhi ya Uingereza alipotokea kabla ya kusaini na klabu ya Barcelona na kuweza kuifundisha adabu Manchester City huko katika viwanja vya...
MTU mmoja Mkazi wa Dar e salaam, ambaye hujishughulisha na uokotaji wa makopo ya plastiki amenusurika kifo kutokana na kipigo cha wananchi baada ya kuvunja vioo vya nyuma vya magari mawili ya wafanyakazi wa bima ya AAR yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ofisi hizo. Kijana huyo aliyekuwa na jeraha upande wa nyuma wa kichwa chake kikivuja Damu nyingi amejitambulisha kwa jina Amir Ismail na kuiambia EFM kuwa kuna vijana sita wamemvamia na kumpora fedha zake shilingi elf 60 alizokuwa nazo. Ismail...
RAIS Vladimir Putin wa Urusi amesema haoni uwezekano wa kuzuka vita kati Ukraine na nchi yake. Rais Putin ameongeza kuwa haoni sababu ya kukutana na maafisa wa Ufaransa, Ukraine na Ujerumani kujadili suluhisho, na kuongeza kwamba hali itarejea kama kawaida taratibu. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi hizo wanakutana leo mjini Paris kujadili usitishaji mapigano mashariki mwa Ukraine....
KUNDI la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria. Tukio hilo la utekaji nyara limefanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi. Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE amewaasa wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini kusoma kwa bidii masomo yote hususani ya sayansi ili kuinua kiwango cha elimu na kuliletea Taifa maendeleo. Rais KIKWETE ametoa wito huo leo wakati akipokea rasmi vitabu milioni mbili na laki tano vya sayansi na hisabati katika shule ya sekondari ya MTAKUJA BEACH Kunduchi jijini Dar es salaam kutoka kwa serikali ya marekani kupitia shirika la msaada la-USAID- kwa lengo la...
KUNA taarifa kuwa mtu mmoja amefariki dunia baada ya kile kinachosemekana kuwa ameuawa na Askari Polisi katika kata ya Ilula, Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo lililotokea tukio hilo, polisi walikuwa kwenye msako wa vilabu vya pombe za kienyeji ambako mtu huyo ambaye jina lake bado halijajulikana inasemekana alikuwa anakunywa pombe hizo. Hata hivyo bado Efm inaendelea kulifuatilia tukio hilo, ili kujua chanzo cha tukio, na juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi mkoani Iringa zinaendelea...
Kama haukubahatika kutazama sherehe za ugawaji wa tuzo za Oscar huko Marekani basi hii inakuhusu Tuzo hizo za awamu ya 87 za Oscar zilifanyika February 22, 2015, huko Hollywood Dolby Theatre kwenye jiji la Los Angels. Katika sherehe hizo mastar wengi wa Hollywood walihudhuria akiwemo aliyekuwa mpenzi wa mchezaji nyota duniani Cristiano Ronaldo Irina Shayk. Vazi la mrembo huyu liliwaacha vinywa wazi baadhi ya wanaume waliokuwa kwenye sherehe...
Kuelekea michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 huko Qatar kikosi maalum cha shirikisho la mpira wa miguu duniani kimetoa mapendekezo ya michuano hiyo kufanyika mwezi wa kumi na moja hadi wa kumi na mbili. Maofisa hao walikutana huko Doha kujadili mapendekezo kufuatia hofu ya hali ya hewa katika msimu wa kiangazi inaweza kuwaathiri wachezaji na mashabiki. Msimu wa kiangazi huko Qatar joto huongezeka hadi kufikia nyuzi joto 40C wakati katika kipindi cha November hadi December kiwango hicho hushuka hadi...
KOREA ya Kusini na Marekani zimetangaza hivi leo kwamba zitaanza mazoezi yao ya kila mwaka ya kijeshi tarehe 2 mwezi ujao, hatua inayotazamiwa kuongeza mzozo na Korea Kaskazini.Serikali ya Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusitisha majaribio yake ya silaha za nyuklia, endapo mazoezi hayo yangefutwa mwaka huu, lakini Marekani ililikataa pendekezo hilo ikiliita “kitisho” cha kufanya jaribio la nne la nyuklia. Mazoezi hayo ya pamoja ndicho kiini cha mzozo wa mara kwa mara kwenye Rasi ya Korea, ambayo Korea Kaskazini huyachukulia...
UTURUKI imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uingereza kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State. Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa likishtua wengi. Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama...