Slider

TANGAZO KUTOKA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA ILALA
Slider

Chama cha mpira wa miguu wilaya ya ilala IDYOUTH kinawatangazia kutawakuwa na michezo miwili ya nusu fainali ya under 17 siku ya jumapili katika uwanja wa chuo cha magereza kati ya Lil boyz vs Vumbua vipaji na Colon vs Manyota ya ilala Mgeni rasmi anatrajiwa kuwa Ruvu kiwanga imetolewa na afisa habari wa chama Musa...

Like
435
0
Thursday, 19 February 2015
LIBYA YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA SILAHA KULINDA USALAMA WAKE
Global News

SERIKALI ya Libya inayotambuliwa Kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya Usalama nchini humo. Akihutubia Kikao cha dharura cha Baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya,MOHAMMED AL-DAIRI amesema hatua hiyo itaisaidia Serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya Wapiganaji. Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Libya ameungwa mkono na Waziri wa Mambo ya nje wa...

Like
199
0
Thursday, 19 February 2015
BARACK OBAMA: HATUPO KWENYE VITA DHIDI WAISLAMU BALI MAGAIDI WANAOUCHAFUA UISLAMU
Global News

RAIS BARACK OBAMA ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu. Bwana OBAMA amesema ni sharti dunia ikabiliane na Itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya dini . Rais huyo wa Marekani ameeleza hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina...

Like
235
0
Thursday, 19 February 2015
NAMTUMBO: WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAKANDARASI WA MIRADI YA BARABARA
Local News

WANANCHI wa Wilaya ya Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma wametakiwa kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo hadi Tunduru  kwa kuacha tabia ya kuwaibia mafuta na vifaa kwa lengo la kuleta ufanisi wa kazi hizo. Hayo yamesemwa na Meneja Wakala wa Barabbara mkoani Ruvuma –TANROADS ABRAHAM KISIMBO wakati alipokuwa akizungumzia kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Barabara hizo unaoendelea kwa kasi tofauti na miaka miwili iliyopita. Kabla ya Serikali haijakatisha mkataba na...

Like
343
0
Thursday, 19 February 2015
SUMATRA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MAJINI KUKATIA LESENI VYOMBO VYAO
Local News

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini-SUMATRA imewataka wamiliki wote wa Vyombo vya Majini kuhakikisha wanakatia Leseni vyombo vyao ili kuweza kufanya kazi kwa lengo la kupunguza vifo vya Majini. Rai hiyo imetolewa na Afisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoani Tanga WALUKANI LUHAMBA katika kikao cha maofisa na Mamlaka zinazojishughulisha na ukaguzi wa vyombo vya majini mkoani humo. Amesema vyombo vingi vya majini vimekuwa vikifanya kazi bila ya kufuata taratibu kitu ambacho ni hatari kwa maisha ya wasafiri...

Like
334
0
Thursday, 19 February 2015
VIDEO: TAZAMA TRAILER YA WIMBO MPYA WA JAGUAR
Entertanment

Mkali kutokea Kenya hutmaker wa ngoma ya Kigeugeu, Kioo na nyingine kibao hivi karibuni anatarajia kuachia mzigo mpya unaokwenda kwa jina la huu mwaka. Jaguar mapema hapo jana alishea kipande cha video ya wimbo huo iliyofanywa chini ya kampuni ya Godfather   Video dropping soon… watch the full trailler here http://youtu.be/MDxn7c9iqPI #huumwaka A post shared by Hon. Jaguar (@jaguarkenya) on Feb 18, 2015 at 12:33am...

Like
912
0
Thursday, 19 February 2015
FA YAMUONYA VAN GAAL
Slider

  Meneja wa timu ya Manchester United Louis van Gaal amepewa onyo na shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza kufuatia kauli alizozitoa kuzungumzia matokeo ya mechi kati ya timu yake na Cambridge United kwenye ligi ya Uingereza ambapo mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya bila kufungana mwezi uliopita. Van Gaal alielekezea lawama zake kwenye Nyanja zote za mechi hiyo kwamba zilikuwa ni dhidi ya timu yake na kuwalaumu waamuzi wa mchezo pia. FA imetoa onyo hilo mara baada ya...

Like
261
0
Thursday, 19 February 2015
UGIRIKI YAPIGANIA KUREGEZWA KAMBA KATIKA MVUTANO WA MADENI
Global News

IMEELEZWA kuwa kuna dalili za kulegezwa kamba katika mvutano wa madeni kati ya Ugiriki na nchi za kanda ya Euro. Kwa mujibu wa duru za serikali mjini Athens,Waziri wa Fedha wa Ugiriki YANNIS VAROUFAKIS amepanga muda wa mpango wa misaada urefushwe. Muda huo ulikuwa umalizike mwishoni mwa mwezi...

Like
227
0
Wednesday, 18 February 2015
UKRAINE: BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAHIMIZA MAKUBALIANO YA KUWEKA SILAHA CHINI YAHESHIMIWE
Global News

KUFUATIA mapigano makali katika mji wa Mashariki ya Ukraine,baraza la usalama la Umoja wa mataifa limehimiza makubaliano ya kuweka chini silaha yaheshimiwe haraka. Muswada wa azimio uliowasilishwa na Urusi umezitaka pande zote zinazohasimiana zitekeleze makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita mjini Minsk. Tayari Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wameliangalia azimio hilo kuwa ni ushindi kwa sababu kwa mara ya kwanza mataifa yote 15 Wachama wa Baraza la Usalama wameyatambua matokeo ya mkutano wa Kilele wa...

Like
210
0
Wednesday, 18 February 2015
DAWASCO YABAINI WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI DAR
Local News

LICHA ya jitihada zinazoendelea kufanywa ili kuzuia uhujumu wa Miundombinu ya Majisafi na Wizi wa Maji,hujuma nyingine kubwa ni ya chuma chakavu za Majitaka. Hujuma hiyo imebainika baada ya DAWASCO kukamata mifuniko ya Majitaka katika kiwanda cha Nondo cha Iron and Steel cha jijini Dar es salaam. Vyuma hivyo chakavu ni mifuniko ya Chemba za Majitaka za DAWASCO, zimebainika baada ya uchunguzi wa kina na taarifa kutoka kwa Wasamaria wema kuhusu upatikanaji wa mifuniko hiyo kiwandani...

Like
608
0
Wednesday, 18 February 2015
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI LINDI NA MTWARA
Local News

WAZIRI wa Nishati na Madini,mheshimiwa  GEORGE SIMBACHAWENE amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo ameahidi huduma za umeme na Maji kwa wananchi mbalimbali. Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Mtambo wa kuchakata gesi, Waziri SIMBACHAWENE amemwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi KAPUULYA MUSOMBA kutoa huduma ya Maji Safi kwa Wananchi wanaozunguka maeneo...

Like
1075
0
Wednesday, 18 February 2015