KUFUATIA malalamiko ya utendaji mbovu katika kufuata taratibu za uzabuni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo, Bodi ya dharura ya Mamlaka ya Bandari nchini-TPA imesimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo MADENI KIPANDE na kumteuwa AWADHI MASSAWE kushika nafasi hiyo hadi uchunguzi rasmi utakapokamilika. Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kikao cha bodi hiyo Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa SAMWEL SITTA amesema uamuzi huo ni muhimu katika kusaidia kuleta maendelea ya kukua kwa uchumi wa Taifa kupitia...
ITALIA imefanikiwa kuokoa Wakimbizi Elfu-2 waliokuwa wakisafiri kwa boti kutoka Libya kuelekea Ulaya. Wakimbizi hao walikuwa kwenye Meli ya Jeshi na boti za Shirika la Uokozi Baharini na pia kwenye boti za Polisi wa Mpakani. Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi ya Italia imeeleza kuwa baadhi ya waokozi wametishiwa na wanaume waliokuwa wamebeba Silaha na ambao wanaaminika kuwa ndio waliowasafirisha Wakimbizi hao. ...
POLISI mjini Damaturu, Nigeria, imesema Mshambuliaji wa Kike wa kujitoa Mhanga amejilipua katika Kituo kimoja cha Basi kilichokuwa kimejaa watu mjini humo na kusababisha vifo vya watu 16 huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa. Mji wa Damaturu ulioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram. Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo amesema amesema amesikia mlipuko uliosababisha taharuki katika eneo...
SERIKALI ya Tanzania imesema hadi ifikapo mwaka 2017, itakuwa imetimiza mpango mahususi wa kutumia umeme wa sola uitwao ‘One Solar Homes’ katika nyumba milioni moja. Akizungumza Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, LUTENGANO MWAKAHESYA, amesema mradi huo unatarajia kutoa huduma ya umeme kwa Asilimia 10 ya watu nchini na ajira 15000 zitakazohusu sola. Amebainisha kuwa mpango huo ni mfano mzuri kwa Mataifa mengine ambayo yana malengo sambamba na mradi wa Power Afrika Initiative uliotangazwa na Rais...
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa BERNARD MEMBE, ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha Tanzania imefungua Idara ya Maalum ya Upasuaji wa moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili -MNH. Hayo yamesemwa na Waziri MEMBE katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kwa niaba ya Rais JAKAYA KIKWETE ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina. Katika sherehe hizo,Jumuiya ya Wachina waishio nchini Tanzania wameungana pamoja na wageni...
Floyd Mayweather Jnr ameikana taarifa inayodai kuwa mpinzani wake Manny Pacquiao ametilia saini mkataba wa kupambana nae huko Las Vegas ifikapo tarehe mbili mwezi wa tano ila Mayweather ameeleza kwamba anamatumaini juu ya pambano hilo kufanyika. Mbabe huyo kutoka nchini Marekani ameonyesha utayari wake juu ya pambano hilo na kusisitiza kwamba bado hakuna makubaliano yoyote yakimaandishi yaliyosainiwa kuthibisha kufanyika kwa pambano hilo. Mayweather aliyasema hayo alipokuwa kwenye NBA All-Star Game katika viwanja vya Madison Square Garden siku...
Sergio Aguero na mpenzi wake Karina Tejeda mwishoni mwa wiki hii walipata nafasi yakutembelea Barcelona na kukutana na mchezaji mwenzake wa Argentina Lionel Mess akiwa na rafiki yake Antonella Roccuzzo. Mshambuliaji huyo wa klabu ya Manchester City Aguero amekuwa akihusishwa nana tetesi za kuhamia Barcelona, hata hivyo vyombo vya habari nchini Hispania vinaamini Messi anamuhitaji Aguero ajiunge na klabu hiyo ili waweze kucheza pamoja. Baadae Aguero alichukua ndege binafsi kurejea nchini Uingereza tayari kujiandaa na michezo ya Ligi kuu nchini...
MSEMAJI wa Ikulu Nchini Urusi amesema leo hii kwamba viongozi wa Urusi,Ukraine na Ujerumani wanaendelea kuwasiliana juu ya suala la mzozo wa Ukraine na kwamba anatarajia mazumgumzo hayo kwa njia ya simu yatafikiwa siku chache zijazo. Dmitry Peskov amesema serikali ya Urusi inatarajia vipengele vyote vilivyomo katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliofikiwa Minsk vitatekelezwa. Usitishaji wa mapigano katika eneo zima la mzozo unatakiwa uanze Jumapili ambapo pande zote mbili zinatakiwa zianze kuondowa silaha nzito kutoka kwenye medani ya...
KUNDI la jihad lililoko Nigeria, Boko Haram, kwa mara ya kwanza limeishambulia Chad. Wakuu nchini humo wanasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivuka ziwa Chad kwa maboti usiku na kushambulia kijiji cha Ngouboua, kilichoko kandokando ya ziwa hilo. Majeshi ya Chad yanasemekana kuwarudisha nyuma wapiganaji hao ambao wanadhibiti eneo kubwa la ziwa hilo upande wa Nigeria....
KUFUATIA agizo lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini hivi karibuni, Mheshimiwa George Simbachawene la kuitaka Mamlaka ya udhibi wa Nishati na Mafuta- EWURA kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za Umeme wa Tanesco, Mamlaka hiyo imetoa tamko la kupunguza gharama za umeme ifikapo Machi mosi mwaka huu. Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam, na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi wakati akiongeza na wandishi wa habari ambapo amesema kwa wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya Umeme itashuka...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta, Jakaya Mrisho Kikwete, amezindua rasmi sera ya elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2014 uliokwenda sambamba uzinduzi wa maabara 3 za Sayansi katika shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Kikwete amesema Elimu bora ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku pamoja na kuliletea Taifa maendeleo kwakuwa inamgusa kila mtu bila kujali jinsia. Uzinduzi huo uliofanywa na Rais Kikwete, ni...