WATUMIAJI wa teknolojia ya interneti nchini wametakiwa kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa mbalimbali za maarifa na zenye mwelekeo wa kuleta maendeleo badala ya kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa zisizo na faida na zenye mwelekeo wa kupotosha kizazi cha sasa kimaadili. Wito huu umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, katika siku ya matumizi ya interneti duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote ambako amesema kuwa Vodacom kama kampuni ya mawasiliano siku zote itakuwa mstari wa...
WATANZANIA wametakiwa kutii sheria na kukaa pembeni ya Barabara pindi wasikiapo ving’ola vya hatari ili kurahisisha shughuli za uokoaji wa maisha ya watu na mali. Hayo yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha zima moto kanda maalum ya Dar es salaam Esward Ikonko alipokuwa Katika ajali ya moto iliyotokea leo eneo la Kariakoo na mnazi mmoja katika mtaa Jamhuri jijini Dar es salaam ambapo amesema moja ya changamoto inayosababisha magari ya zima moto kuchelewa katika eneo latukio ni msongamano wa watu....
(1) mwanzilishi wa simba B anatueleza sababu zilizo pelekea kuanzishwa kwa timu hiyo na wakina nani walikua waanzilishi. (2)Lengo la kuamua kuanzisha simba B ni nini (3)Kwa nini wachezaji wengi waliotoka simba B wapo katika klabu nyingine na hili simba wanalitazavipi. (4)Changamoto mnazokutana nazo ndani ya simba mnakabiliana nazo vipi? Je viongozi wa simba wanatoa ushirikiano katika hili. (5)Kuliwahi kutokea hali ya kutoelewana kati yenu na viongozi wa juu wa simba nahii nikutokana na ninyi kugoma kuwatumia wachezaji kutoka...
RAIS wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani inatafakari kupeleka silaha nchini Ukraine kusaidia kukabiliana na Waasi wanaoiunga mkono Urusi. Akizungumza katika Ikulu ya White House baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Markel, Obama amesema nia itakuwa kuisaidia Ukraine kuimarisha ulinzi kuliko kulishinda jeshi la Urusi. Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Angela Markel amesema haoni kama njia za kijeshi zinaweza kuumaliza mzozo huo....
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutokubali kuuza maeneo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi kwa kiasi kidogo cha fedha kwani thamani ya maeneo hayo ni kubwa. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho katika matawi ya Raha leo...
IMEELEZWA kuwa wanawake wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa ugonjwa wa Saratani kutokana na uoga wa kupima afya zao mara kwa mara. Akizindua upimaji wa Saratani Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma FATMA ALY amesema Wanawake wamekuwa wakiishi kwa hofu kuogopa kupima afya zao wakihofia kupokea majibu ambayo si mazuri. Amesema Saratani inatibika kama watawahi kabla haijazidi hivyo amewataka wajijengee tabia ya kupima afya mara kwa mara. ...
MIILI ya watu Sita wa Familia moja walioteketea kwa moto inatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Airwing jijini Dar es salaam. Hata hivyo bado chanzo cha moto huo hakijajulikana huku baadhi ya watu wakidai huenda moto huo umesababishwa na Petrol. Moto huo umetokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika Mtaa wa Kipunguni A Kipawa jijini Dar es salaam....
Imetayarishwa kwenye studio za Tomz rec. Mixing imefanywa na Mr.Thomas ...
UMOJA WA MATAIFA umesema mazungumzo yanayolenga kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Yemen yanatarajiwa kurejea leo na yatasimamiwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamal Benomar. Taarifa kutoka umoja huo imesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepokea vyema tangazo kuwa mshauri wake maalum kuhusu Yemen Benomar atayasimamia mazungumzo hayo na kuzitaka pande zinazopigana nchini humo kurejea katika meza ya mazungumzo kwa nia njema na kuwa na nia ya kuafikiana. Yemen imekumbwa na mzozo tangu Rais...
VIONGOZI wa Ukraine, Ujerumani na Ufaransa wanashinikiza kuwepo kwa mkutano wa kilele na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano wiki hii katika juhudi za hivi karibuni za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo Rais Putin ameonya kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Minsk, utafanyika tu iwapo viongozi hao watasikilizana kuhusu masuala kadhaa kabla ya Jumatano. Hii leo maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa nchi hizo nne watafanya mazungumzo kwa ajili ya maandalizi ya...
MTANDAO wa kijinsia Tanzania TGNP umefanya mafunzo ya kuelimisha Wazee wa kimila katika Mikoa ya Mara, Shinyanga, Pwani, Dar es salaam, Mbeya na Morogoro lengo likiwa ni kuwapa Ujuzi wazee hao ili waweze kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. Akizungumza na EFM Afisa mawasiliano kutoka Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP MERKIZEDECK KAROLI amesema kuwa kupitia Semina hiyo itawawezesha wazee hao kujua endapo katika maeneo wanayoishi kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutoa...