NDEGE inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei. Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa. Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung. Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo. Chanzo cha ajali...
CHAMA CHA WAFUGAJI Tanzania-CCWT kimetoa tamko la kutotambua mkutano uliofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa GEORGE SIMON kuanzisha chama kingine cha wafugaji kwa madai ya kutofuata sheria na Katiba zilizounda chama hicho. Tamko hilo limekuja kufuatia Mkutano Mkuu wa Wanachama wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma January 24 na 25 mwaka huu. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa- CCWT ALLY LUMIYE amesema kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho alikumbwa na tuhuma za...
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI amesema Serikali itahakikisha inapambana na watu wote wanaoendesha vitendo vya dhuluma, matapeli na wanaonyang’anya viwanja, majengo, mashamba na ardhi za wanyonge. Waziri LUKUVI ametangaza azma hiyo wakati akijibu baadhi ya hoja za Wabunge waliochangia Taarifa ya Kamati ya Bunge, ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni mjini Dodoma. Amebainisha kuwa anatambua kwamba hasa maeneo ya mijini kuna dhuluma nyingi zinafanyika ambapo Masikini,...
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema takribani watu Milioni Tisa wanakufa kila mwaka kutokana na kuugua ugonjwa wa Saratani. Kauli hiyo imetolewa na Waziri huyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa February 04 kila mwaka Duniani kote. Ametaja kauli Mbiu ya mwaka huu kuwa ni UDHIBITI WA SARATANI UPO NDANI YA UWEZO WETU. Amebainisha kuwa pamoja na idadi ya watu wanaokufa na ugonjwa...
Klabu ya Liverpool imepanga kutembelea nchini Australia baadae mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kampeni ya klabu hiyo kwa mwaka 2015 hadi 2016 iliripoti klabu hiyo ya ligi ya Uingereza siku ya jumanne Liverpool kwa mara ya mwisho ilifanya safari katika Nchi ya Australia takribani miaka miwili iliyopita Klabu hiyo ikiwa nchini humo itacheza na klabu ya Brisbane Roar katika uwanja wa Queensland’s Suncorp tarehe 17 ya mwezi wa saba mwaka huu na baadae watacheza na klabu ya...
KENETH anaelezea ubora wa klabu za zamani na utofauti wa klabu za sasa. Nini kifanyike ili timu yetu ya taifa iweze kufanya vizuri Nitakribani miaka 26 sasa imepita tangu kikosi cha timu ya taifa taifa stars kushiriki katika michuano ya mataifa Africa na kwa nini haikuweza kushiriki kwa mara nyingine. Nini kikwazo katika mchezo wa soka tanzania MOHAMED MWAMEJA Ilikuaje ukahusishwa katika sakata la usajili dhidi ya keny mkapa AFRICAN SPORTS Mara baada ya klabu ya AFRICAN SPORT kupata nafasi...
WAZIRI MKUU mpya wa Ugiriki Alexis Tsipras anaendelea na ziara ya mataifa ya Ulaya tangu aingie madaraka wiki moja iliyopita, katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono mpango wa kutaka suala la kuiokoa nchi yake na mzigo wa madeni lijadiliwe upya. Anakwenda Italia leo kwa mazungumzo na waziri mkuu Matteo Renzi. Jana waziri mkuu huyo aliondoa uwezekano wa kufanyakazi pamoja na kundi la pande tatu la wakopeshaji wa ...
UMOJA wa Ulaya umesema leo kuwa mahakama nchini Misri imekiuka majukumu yake ya kimataifa kuhusu haki za binadamu kwa kuwahukumu watu 183 adhabu ya kifo jana kwa kuwauwa polisi 13. Idara ya mambo ya kigeni ya Umoja wa Ulaya imesema katika taarifa yake kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya Misri kuwahukumu washitakiwa 183 adhabu ya kifo kufuatia kesi ya jumla ni ukiukaji wa majukumu ya Misri ya haki za binadamu. Hukumu iliyotolewa ...
SERIKALI imeshauriwa kuweka mikakati bora itakayowezesha kuanzishwa kwa mfuko wa kujitegemea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kuboresha tume ya kupambana na kudhibiti Ukimwi –TACAIDS- ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo na kuliletea Taifa maendeleo. Akitoa taarifa za utekelezaji wa kamati ya masuala ya Ukimwi leo Bungeni mjini Dodoma mwenyekiti wa Kamati hiyo LEDIANA MNG’ONG’O amesema kuwa endapo mfuko huo utaanzishwa utaisaidia nchi kwa kiasi kikubwa katika kupambana na ugonjwa huo pasipo...
UMOJA wa Nchi Huru za Afrika –AU, umetoa heshima pekee kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kumuenzi kwa kuamua kuwa moja ya majengo yake muhimu katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, litapewa jina la Mwalimu Julius Nyerere. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anapewa heshima hiyo kubwa kwa mchango wake katika ukombozi wa Bara la Afrika na kuliondoa Bara hilo katika ukoloni. Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama (Peace and Security Council)...
LEO ni mwezi mmoja tangu wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia miji ya Baga na Doron Baga kaskazini mashariki mwa Nigeria. Idadi kamili ya watu waliokufa haijulikani lakini inadaiwa kuwa ni kati ya watu mia moja na hamsini hadi elfu mbili. Wakati wapiganaji wa Boko Haram wakivamia kutoka upande wa magharibi wa Baga, kundi la vijana waliodhamiria kupambana na kundi hilo walijaribu kuulinda mji wao. ...