Kutoka Viwanja Vya Posta Kijitonyama wakazi wa jiji la Daresalaam waliungana kwa pamoja kwenye tukio la kihistoria lililowakutanisha madereva wa bodaboda na bajajiji kutoka karibu kila kona ya jiji. Wanafamilia wa E-fm wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani Shangwe la kutosha kutoka kwa Wakzi wa Dsm Mtangazaji wa kipindi cha Genge Kicheko akiwarusha mashabiki wa E-Fm Kala Jeremiah Akiwasha moto kwenye jukwaa Viongozi kutoka jeshi la Polisi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa E-fm wakizungumza na wana E-fm kwa lengo la...
Kijana wa miaka 29 Jamie Vardy kutoka Leicister City anatarajiwa hii leo kutoa majibu iwapo atajiunga na Club ya Arsenal kabla hajaelekea kwenye michuano ya Euro za mwaka huu akiwa na timu ya taifa la Uingereza.Arsenal tayari wamefikia makubaliano na Leicester na wamemwekea mezani Vardy kitita cha fedha kwa miaka minne. Vardy bado alikuwa anatafakari kama awaache Mbweha kuelekea kwa washika Bunduki. Itakumbukwa Vardy aliisaidia sana Leicister katika kutwaa taji la Ligi kuu akifunga mabao...
Vyombo vya habari nchini Marekani, vinaripoti kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda uteuzi wa chama hicho katika eneo la Puerto Rico. Ushindi huo unaimarisha matumaini yake ya kunyakua uteuzi wa chama hicho, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi wa Novemba mwaka huu. Matokeo ya awali yanaashiria kuwa Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders. Bi Clinton sasa anahitaji chini ya wajumbe 30tu ili kushinda uteuzi...
wa aliyekuwa bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali, umewasili mjini Louisville, Kentucky, ambako atazikwa siku ya Ijumaa. Mwili wa bondia huyo wa zamani ulisafirishwa kwa msafara wa magari kutoka uwanja wa ndege wa Louisville . Mazishi yake yanatarajiwa kuwa hafla kubwa ya umma. Ali alikuwa mmoja wa wanamichezo maarufu zaidi duniani katika karne hii ya...
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limewahimiza watu wanaotoka katika sehemu zilizoathirika na virusi vya Zika kuzingatia mbinu za kujikinga endapo mtu anafanya mapenzi au kujiepusha na ngono kwa muda wa wiki nane. WHO imeongeza kwamba ni muhimu kwa wanawake kuepuka kupata ujauzito kwa miezi sita iwapo mwenzake wa ndoa amekuwa na dalili za virusi vya ugonjwa huo. Wiki iliyopita shirika hilo lilisema kuwa hakuna sababu ya kujiepusha na michezo ya Olimpiki mjini Rio mwezi...
KOREA Kaskazini imefanya jaribio lingine la makombora yake ya masafa marefu katika eneo la mashariki ya pwani yake lakini linaonekana kufeli. Wakizungumzia makombora hayo wanajeshi wa Korea Kaskazini wamesema kuwa haijulikani ni kombora gani limefeli na kwamba hiyo imejirudia baada ya makombora mengine yaliyojulikana kwa jina la ”Musudan” kufeli mnamo mwezi Aprili. Hata hivyo imeelezwa kutanda kwa wasiwasi katika eneo hilo baada ya Pyongyang kujaribu kombora la nne la Kinyukia mnamo mwezi Januari pamoja na makombora...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa mambo ya malikale na uhifadhi wa urithi asilia watafute mbinu zitakazoimarisha utunzaji wa rasilmali hizo bila kuathiri mifumo ya uchumi wa nchi zinazoendelea. Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito huo leo Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa siku nne unaojadili Uhifadhi wa Urithi wa Dunia wa Afrika kama Nyenzo ya kuleta Maendeleo Endelevu. Waziri Mkuu amesema endapo rasilmali hizo zitachambuliwa vizuri na kwa njia sahihi bila...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amewaeleza wananchi kisiwani Pemba kuwa Zanzibar hapatakuwa tena na uchaguzi hadi mwaka 2020 na kwamba kwa sasa yeye ndiye Rais aliyechaguliwa kihalali na wananchi. Dokta Shein ameyasema hayo huko Tibirinzi Chake Chake Pemba, alipokwenda kukagua Tawi la CCM lililochomwa moto katika ziara yake ya kukagua athari zilizofanywa dhidi ya Wana CCM kwa kuendelea kukiunga mkono chama hicho kiswani humo. Mbali na hayo amewataka wananchi kuyapuuza maneno ya utani na dhihaka...
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-3. Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 20 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji. Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis...
Kesi ya mashtaka ya ukiukaji wa kibinaadamu dhidi Mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Simone Gbagbo,imeanza katika mahakama ya mji mkuu wa Abidjan. Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama ‘mwanamke mkakamavu’ amewahi kuhudumia miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3. Vita hivyo viliisha baada ya mumewe, Laurent Gbagbo kukamatwa na Umoja wa Mataifa na jeshi la ufaransa kumuunga...
ALIYEKUWA rais wa Chad Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono. Habre alihusika moja kwa moja katika uhalifu huo ambao ulifanyika wakati akiwa rais wa Chad. Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji Dakar nchini Senegal, wameshangilia wakati jaji alipomaliza kusoma...