Slider

ILALA: POLISI YAWATOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA USALAMA
Local News

JESHI la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala na kuachana na taarifa za uvumi kuwa hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi sio nzuri.   Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Lucas Mkondya amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote.   Kuhusiana na malalamiko ya wananchi wa Buguruni kuhusiana na kuwepo kwa kundi la vibaka na waporaji kamanda Mkondya amesema...

Like
225
0
Thursday, 05 May 2016
DARESALAAM INATARAJIWA KUWA NA WATU MILIONI 10 IFIKAPO 2030
Local News

MKOA wa Dar es salaam unatarajiwa kuwa na watu milioni 10 ifikapo mwaka 2030 hivyo ni muhimu kuzingatia uboreshaji wa Jiji kulingana na idadi ya watu.   Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake ambapo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu serikali ilibuni mradi wa uendelezaji wa Jiji kwa ufadhili wa benki ya dunia.   Amesema kuwa ukuaji wa Jiji la Dar es salaam unakabiliwa na makazi...

Like
242
0
Thursday, 05 May 2016
KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO
Global News

MWANASIASA mashuhuri wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ametoa tangazo hilo kupitia mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadhaa vya upinzani nchini humo umeamua kumuidhinisha Bwana Katumbi kuwa mgombea wao wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi...

Like
187
0
Thursday, 05 May 2016
AFRIKA KUSINI: WABUNGE WATWANGANA BUNGENI
Global News

WABUNGE wa Bunge la Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni kwaajili ya kuwahutubia. Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani. Hata hivyo ujio wake uliwakera wabunge wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) ambao walipiga mayowe na kumtupia matusi Rais...

Like
302
0
Thursday, 05 May 2016
AJIRA KWA VIJANA BADO NI CHANGAMOTO
Local News

MKURUGENZI wa Idara ya Ajira Ameir Ali Ameir amesema tatizo la ajira nchini bado ni changamoto kubwa kwa vijana kutokana na vijana wengi kukosa sifa za kuajiriwa na baadhi yao kuchagua kazi za kuajiriwa.   Ameir ameyasema hayo katika Ukumbi wa Kidongo chekundu wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wa Kamati za Ajira za Wilaya za Mjini na Magharibi.   Amesema vijana ndio nguvu kazi katika jamii hivyo wana nafasi kubwa katika kulitumika Taifa kwa  kufanya kazi lakini mtazamo wa vijana bado...

Like
356
0
Thursday, 05 May 2016
SERIKALI YATANGAZA KUTOA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI NA MADEREVA WA KEMIKALI
Local News

SERIKALI imesema kuwa inatarajia kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123wanaosafirisha Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na matumizi yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.   Akizungumza jana Jijini Dar es salaam  wakati wa mkutano na waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na ubora wa Mifumo Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani...

Like
331
0
Thursday, 05 May 2016
CHELSEA NA TOTTENHAM WAMEPIGWA FAINI
Slider

Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kwa pamoja na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kukabiliwa na makosa matatu ya kushindwa kuwazuia wachezaji pamoja na maofisa wake wakati na baada ya mchezo wa jumatatu. Kiungo wa Spurs Mousa Dembele amekumbana na adhabu pia ya kusababisha vurugu katika mchezo huo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.FA inasema kuwa kitendo cha Dembele kumuingizia vidole machoni mchezaji wa Chelsea Diego Costa ni utovu mkubwa wa nidhamu. Hiyo ina maana ”akikutwa na hatia” kufungiwa michezo...

Like
321
0
Thursday, 05 May 2016
UMOJA WA ULAYA WAFIKIA MAKUBALIANO JUU YA WAKIMBIZI KUTOKA SYRIA
Global News

UMOJA wa Ulaya na Uturuki wamekubaliana, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya Habari juu ya namna ya kuwachagua wakimbizi wa Syria watakaohamishiwa katika nchi za Umoja huo. Gazeti la “Bild” limenukuu waraka wa siri unaoonyesha kwamba wasyria tu ndio watakaoruhusiwa kwanza kuingia katika nchi za Umoja wa ulaya ikiwa wameomba kinga kabla ya novemba 29 nchini Uturuki. Aidha taarifa zimeeleza kwamba Makubaliano ya awali yanawataka wakimbizi kutojichagulia wenyewe nchi wanayotaka wapelekwe na badala yake kukubali kupangiwa nchi za...

Like
237
0
Wednesday, 04 May 2016
RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI BAGAZA AFARIKI DUNIA
Global News

RAIS wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter imeeleza kuwa Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo baadaye aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu yake Meja Pierre Buyoya mwezi Septemba...

Like
325
0
Wednesday, 04 May 2016
VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU
Local News

JAMII imetakiwa kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta binafsi zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwani vita hiyo ni ya kila Mtanzania mwenye nia njema na vijana. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kusaidia waathirika wa Dawa za kulevya cha Pili Misana Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam Bi Pili Misana alipozungumza na Waandishi wa habari katika hafla ya kituo hicho kufikisha miaka minne tangu kuanzishwa kwake. Bi. Misana amesema tangu kuanzishwa kwa vituo...

Like
276
0
Wednesday, 04 May 2016
TEKNOLOJIA YAIWEZESHA SEKTA YA FEDHA KUPIGA HATUA
Local News

SERIKALI imesema kuwa maendeleo katika sekta ya fedha kwa kutumia teknolojia yamepiga hatua kubwa kwa  kupitia mkonge wa Taifa imekuwa rahisi kwa Watanzania kutumia na kuchochea kasi ya biashara na kujenga uchumi wa Taifa kwa ujumla. Akizungumza na E fm Jijini Dar es salaam Naibu Waziri fedha na Mipango Dokta Ashatu Kijaji amesema kuwa Watanzania wana nafasi kubwa ya kutumia teknolojia hiyo vizuri na itasaidia kuinua uchumi na kuchochoea maendeleo ya Taifa. Amebainisha kuwa Serikali imejipanga vizuri katika kudhibiti udanganyifu na...

Like
309
0
Wednesday, 04 May 2016