Slider

ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA MADRID OPEN
Slider

Mwingereza Andy Murray ameanza vyema kutetea taji lake katika michuano ya Madrid Open kwa ushindi wa seti 7-6 7-3 3-6 na 6-1 dhidi ya Radek Stepanek. Ilichukua muda wa saa mbili na dakika 16 kwa Murry kumshinda Stepanek raia wa Czech mwenye miaka 37. ”Sikucheza michezo mingi kipindi cha nyuma.Ilikua ngumu sana,”alisema Murray mwenye miaka 28 ambaye atakutana na Gilles Simon ama Pablo Busta katika mzunguko wa tatu siku ya Alhamisi. Mapema kwenye mchezo wa awali Muhispaniola Rafael Nadal alimshinda...

Like
243
0
Wednesday, 04 May 2016
WALIOFARIKI MKASA WA JENGO NAIROBI WAONGEZEKA
Global News

IDADI ya watu waliofariki baada ya jumba la ghorofa sita kuporomoka siku ya Ijumaa imeongezeka baada ya miili zaidi kupatikana kwenye vifusi. Maafisa wa uokoaji wamepata miili mitatu zaidi na kufikisha miili 26, ambayo ni idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha. Hata hivyo Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limeeleza kuwa Watu 93 bado hawajulikani...

Like
194
0
Wednesday, 04 May 2016
TED CRUZ AJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO MAREKANI
Local News

SENETA wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican. Cruz ametoa tangazo lake muda mfupi baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana. Katika hatua nyingine Seneta wa Vermont- Bernie Sanders amemshinda Hillary Clinton kwenye uchaguzi wa mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Democratic katika jimbo la...

Like
188
0
Wednesday, 04 May 2016
WATU LAKI NNE HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KUTOKANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA
Local News

INAKADIRIWA kuwa Watu laki nne hupoteza maisha kila mwaka Nchini kutokana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mafuriko, ukame na migogoro ya rasilimali kwa Wakulima na Wafugaji. Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Dokta Azma Simba katika Semina maalum ya Wanahabari iliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mamlaka ya hali ya hewa lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo Wanahabari kutoa elimu juu ya athari za mabadiliko ya tabia nnchi. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya...

Like
225
0
Wednesday, 04 May 2016
POLISI WA CHINA KUPIGA DORIA ITALIA
Global News

MAAFISA wanne wa polisi nchini China wamesema kuwa watashirikiana na wenzao wa Itali kupiga doria mjini Rome na Milan katika jaribio la wiki mbili zijazo. Waziri wa mambo ya nje wa Italia Angelino Alfano amesema Maafisa hao wanaozungumza Kiitaliano wanatumwa nchini Italia kwa lengo la kuwafanya watalii wa China kujisikia huru na salama wakati huu wa msimu wa juu wa utalii. Takribani watalii milioni 3 kutoka nchini China hutembelea nchi ya Italia kila mwaka....

Like
228
0
Tuesday, 03 May 2016
SYRIA: UN YASHINIKIZA URUSI KUOKOA MAKUBALIANO
Global News

MJUMBE wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura anatarajiwa kukutana na waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi kujadiliana kuhusu juhudi za kunusuru kuvunjika kwa mkataba wa amani nchin Syria. De Mistura anataka Urusi na Marekani ambazo zinaunga mkono makundi pinzani nchini humo kushirikiana ili kurejesha makubaliano waliopatana mwezi Februari. Hata hivyo Washington imeilaumu Moscow kwa kushindwa kuwazuia wanajeshi wa Syria waliopo mjini...

Like
218
0
Tuesday, 03 May 2016
NAIBU BALOZI WA UINGEREZA AISIFU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE
Local News

NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.  Pongezi hizo amezitoa leo baada ya kutembelea kambi hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini. Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na...

Like
204
0
Tuesday, 03 May 2016
WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA
Local News

MAMLAKA ya hali ya hewa Nchini-TMA-imewataka Wakulima na Wafugaji kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji katika kilimo na Ufugaji. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya hali ya hewa Nchini Dokta Ladislaus Chang’a amesema  mifugo mingi pamoja na mazao ya kilimo yamekuwa yakiharibika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa jambo ambalo  husababisha upungufu katika uzalishaji hivyo ni muhimu kwa wakulima hao kufuatilia taarifa...

Like
192
0
Tuesday, 03 May 2016
UTAFITI WA SARATANI YA MATITI WAKAMILIKA
Global News

TIMU ya kimataifa ya wanasayansi imekamilisha utafiti mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa maumbile ya saratani ya matiti, ambayo wamesema inawapa karibu picha kamili ya nini husababisha ugonjwa huo. Wanasayansi hao wanajaribu kutizama mfuatano wa jinomu kamili wa kesi zaidi ya mia tano za saratani ya matiti. Utafiti huo unaoongozwa na taasisi ya Cambridge umeweza kugundua aina tano mpya za visababishi vya ugonjwa huo ambavyo vikibadilika husababisha uvimbe katika sehemu husika ya mwili wa...

Like
276
0
Tuesday, 03 May 2016
MTOTO MCHANGA ATOLEWA KWENYE VIFUSI NAIROBI
Global News

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka siku ya Ijumaa jijini Nairobi nchini Kenya. Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha. Akizungumzia hali ya afya ya mtoto huyo, Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai amesema kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea kuimalika tangu alipofikishwa hospitalini...

Like
289
0
Tuesday, 03 May 2016
NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OCTOBA 2015
Local News

KAMATI Maalumu iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.   Akizungumza Katika kikao cha Tume baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza kazi iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.   Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume...

Like
272
0
Tuesday, 03 May 2016