Slider

KAMPUNI YENYE MAHUSIANO NA CHINA YATUHUMIWA KUWADHILI WANAMGAMBO SUDANI KUSINI
Global News

SHIRIKA la utafiti kuhuhusu silaha ndogondogo, limesema kuwa Kampuni ya mafuta iliyo na mahusiano na China inawafadhili wanamgambo nchini Sudani kusini. Wanamgambo takriban mia saba wanaelezwa kupelekwa katika maeneo ya machimbo ya mafuta yanayomilikiwa na Kampuni hiyo ambayo Shirika la Petroli la Kenya lina hisa kubwa zaidi. Hakukuwa na majibu yoyote kuhusu utafiti uliotolewa na Kampuni ya...

Like
373
0
Friday, 30 January 2015
MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA UMEANZA LEO
Global News

MKUTANO wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika umeanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa sasa. Baadhi ya maswala yatakayopewa kipaumbele kwenye mkutano huo ni harakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, pamoja na juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Licha ya kauli mbiu ya mkutano huo wa siku mbili kuwa swala la kuwawezesha wanawake, viongozi kutoka nchi 54 wanachama wa Muungano huo watalazimika kangazia...

Like
245
0
Friday, 30 January 2015
JUMUIYA YA VIJANA CUF IMEMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU
Local News

JUMUIYA ya Vijana CUF –JUVICUF imemtaka waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe kujiuzulu kufuatia tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba,viongozi waandamizi na wanachama wake,pamoja na kutoa kauli ya uongo bungeni jana. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa JUVICUF Hamidu Bobali amesema kuwa wanasikitishwa na vitendo vilivyofanywa na jeshi la polisi na kulaani ukimya wa viongozi wa juu pamoja na upotoshaji unaofanywa na viongozi hao...

Like
299
0
Friday, 30 January 2015
SERIKALI YAANZA KUPITIA RIPOTI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI
Local News

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imeanza kupitia ripoti ya wadau wa Elimu kuhusu tafiti za watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni ili kuwawezesha watoto hao kupata elimu. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Elimu Kitengo cha Jinsia kutoka Wizara ya Elimu, Chimpaye Marandu wakati wakijadili ripoti iliyowasilishwa na Taasisi ya Policy Forum kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi. Marandu amesema kuna idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokosa Elimu kwa sababu ya kupata...

Like
351
0
Friday, 30 January 2015
CHELSEA MBIONI KUMYAKUA JUAN CUADRADO
Slider

Klabu ya Chelsea ipo kwenye hatua za mwisho kumsainisha mshambuliaji Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka 26 Juan Cuadrado ambae ni raia wa Colombia amekubaliana na dili hilo na viongozi wa ligi na klabu hivyo yupo katika hatua za mwisho za uhamiaji utakogharimu paundi milioni 26.8 kutoka kwenye klabu ya Fiorentina ya huko Italia.   Ujio wa Cuadrado’s katika klabu ya Chelsea unamaana yakuwa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 kutokea Ujerumani Andre Schurrle kwa sasa kuna uhakika wa yeye...

Like
352
0
Friday, 30 January 2015
THT KUADHIMISHA MIAKA 10
Entertanment

Baadhi ya wanamziki kutoka THT walitua katika kituo cha 93.7 EFM katika kipindi cha Genge ambacho kinatangazwa na Snahlicious pamoja na Baghdad kuanzia saa tatu asubhi mpaka saa sita mchana.  THT wanaadhimisha miaka kumi hapo kesho tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.  Maadhimisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Escape one na itashirikisha wasanii mbali mbali,wazamani na wapya kutoka katika taasisi hiyo.  Miongoni mwa wasanii watakao kuwepo kutoka THT ni pamoja na Linah, Mwasiti, Barnaba, Amini, Marlaw, Maunda Zorro, Dream na kadhalika....

Like
563
0
Friday, 30 January 2015
26 WAUAWA MISRI
Global News

MAAFISA wa Jeshi nchini Misri wamesema takriban watu 26 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic State Kaskazini mwa Misri katika eneo la Sinai Wamesema gari lililokuwa na mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini mwa Sinai katika mji wa El-Arish yakilenga hoteli ya jeshi na kuwaua wanajeshi kadhaa. Mashambulizi mengine kama hayo yalifanyika katika mji jirani wa Sheik Zuwayid na mji wa Rafah katika mpaka wa Gaza. Wakati huo huo kundi la wapiganaji la Ansar...

Like
258
0
Friday, 30 January 2015
NIGERIA YATUMIWA UJUMBE KUSIMAMIA UCHAGUZI
Global News

MWENYEKITI wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini-Zuma ameidhinisha kutuma ujumbe wa waangalizi wa umoja huo nchini Nigeria ili kusimamia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu. Taarifa kutoka Umoja wa Afrika zimesema kabla ya waangalizi 50 wa muda mfupi wa Umoja huo kwenda Nigeria, umoja huo utatuma wataalam 15 kuwa waangalizi wa muda mrefu, ambao watakuwepo nchini humo hadi tarehe 11 Machi ili kuangalia vipindi mbalimbali vya mchakato wa...

Like
316
0
Friday, 30 January 2015
VIJANA ZAIDI YA 70 WANUFAIKA NA MRADI WA KUIJIONGEZEA KIPATO
Local News

VIKUNDI saba vya vijana na wanawake vyenye wanachama 73 wamenufaika kwa kupata mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 7 kwa ajili ya kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi. Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa, DoktaLeticia Warioba wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema vijana zaidi ya 70 wamepatiwa vifaa na mbegu na wamelima zaidi ya ekari 70 katika kijiji cha Isimani ikiwa ni mradi wa kujiongezea kipato. Amesema vijana hao wamepatiwa mikopo hiyo kwa ajili ya kuanzisha shughuli...

Like
312
0
Friday, 30 January 2015
SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUSHIRIKISHA SHUGHURI ZA KILIMO NA VIWANDA ILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAO
Local News

KATIKA kupambana na umasikini nchini Serikali imeaandaa mpango wa kushirikisha shughuli za kilimo na viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima yanayouzwa nje ya nchi badala ya kuendelea kuuza mazao ghafi kwa thamani ndogo. Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo na Chakula STEVEN WASIRA alipozungumza katika Mkutano wa maswala ya Kilimo ulioandaliwa na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa-IFAD- ambapo amesema mpango huo utawawezesha wakulima wadogo kuinuka kiuchumi na kuepukana na umasikini unaowasumbua wakulima...

Like
333
0
Friday, 30 January 2015
POLISI WAPEWA KIZUNGUMKUTI KWENYE NYUMBA YA WATOTO WA P DIDY
Entertanment

Idara ya polisi katika jiji la Loss Angels walilazimika kukimbilia kwenye nyumba ya watoto wa P Didy mara baada ya kupata taarifa ya kusikika kwa milio ya bunduki na tishio la kifo. Polisi walipokea simu yenye kuelezea kuwa kuna barua imeachwa kwenye mlango wa nyumba hiyo yenye vitisho vya kutaka kuuwa watu wote kwenye nyumba hiyo ya mwanamama Kim Poster’s huko L.A Maafisa hao walifika kwenye nyumba hiyo na kukuta hakuna mtu yeyote wala barua ya vitisho. Dakika sita baada...

Like
572
0
Friday, 30 January 2015