Slider

SUGE KNIGHT AKABILIWA NA KESI YA MAUAJI YA RAFIKI YAKE
Entertanment

Marion “Suge” Knight alihusika katika kugonga na kukimbia alasiri ya Januari 29) hali iliyopelekea mtu mmoja kufa na mwingine kujeruhiwa katika jimbo la California. ofisi ya mwanasheria James E. Blatt, wakili wa Knight alithibitishia vyombo vya habari Kulingana na TMZ, Knight alikuwa katika mabishano na watu wawili juu ya seti ya filamu ambapo walinzi walimuamuru aondoke sasa wakati anaondoka kwa hasira aliwasha gari lake na kurudi nyuma kwa kasi na kumgonga rafiki yake yake aliekwenda nae eneo hilo Terry Carter...

Like
427
0
Friday, 30 January 2015
MALAYSIA YASITISHA SHUGHULI YA UTAFUTAJI WA NDEGE YA MH370
Global News

SERIKALI ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege ya iliyopotea ya MH370 na kuitaja kama ajali huku ikisema hapakuwa na manusura wa ajali hiyo. Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege hiyo, bado inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hiyo walifariki. Ndege hiyo bado haijulikani iliko na wala kujulikana ilikopotelea licha ya shughuli kubwa ya kimataifa kuitafuta kusini mwa bahari ya hindi. Tangazo la serikali ya Malaysia, lililotolewa leo, linatoa fursa kwa jamaa wa waathiriwa wa ajali hiyo...

Like
281
0
Thursday, 29 January 2015
RAIS KIIR AKIMBIZWA HOSPITALINI ETHIOPIA
Global News

MKUTANO wa viongozi wa kikanda ulioandaliwa kujadili mgogoro wa mwaka mmoja ulioko nchini Sudan Kusini, umecheleweshwa baada ya Rais Salva Kiir kuugua na kukimbizwa hospitalini mjini Addis Ababa, Ethiopia. Afisa mmoja wa shirika la IGAD, ambalo linafanya juhudi za kuwakutanisha viongozi wa Sudan Kusini kwa lengo la kumaliza vita, ameliambia shirika la Utangazaji la BBC, kwamba Rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani. Kabla ya kuugua, hapo jana Rais Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka...

Like
271
0
Thursday, 29 January 2015
ESCROW: KUJIUZULU KWA PROF. MUHONGO HAITOSHI
Local News

IMEELEZWA kuwa pamoja na kijiuzulu kwa Profesa Sospeter Muhongo, bado hatua hiyo haitoshi kutatua tatizo la wizi mzito wa fedha za umma kwakuwa wahusika wakuu wa uchotaji wa fedha hizo, bado hawajakamatwa na hata kuhojiwa na hivyo mjadala wa Escrow bado ungali mbichi. Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa CHADEMA Arcado Ntagazwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliojadili namna sakata la Tegeta Escrow linavyoendeshwa. Akifafanua hayo Ntagazwa amesema kuwa hatua madhubuti...

Like
265
0
Thursday, 29 January 2015
KITUKO CHA HAKI ZA BINADAMU KIMELAANI KITENDO CHA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA CUF
Local News

KITUO cha sheria na haki za binadamu kimelaani vikali kitendo cha kupigwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi –CUF, Profesa IBRAHIM LIPUMBA na kusema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar e s salaam Mkurugenzi wa Kituo hicho, HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kumekuwa na ubaguzi mkubwa hasa katika vyama vya siasa jambo linalopelekea kuvigawa vyama hivyo na kuvikosesha haki yao ya msingi. Aidha amesema kuwa kitendo cha jeshi la polisi kujichukulia sheria mkononi...

Like
232
0
Thursday, 29 January 2015
FIFA: BLATTER AREJESHA FOMU KUWANIA URAIS
Slider

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Sepp Blatter leo amerudisha fomu za kuwania kugombea urais wa shirikisho hilo kwa awamu ya tano Kupitia akaunti yake ya Twitter Blatter aliandika “Today (Thursday) is a key date in the electoral calendar. I’ve made my submission, now the electoral committee follow a process,” akimaanisha kuwa leo ni siku muhimu katika kalenda ya uchaguzi na amefanya maamuzi hayoya kurudisha fomu hivyo anaichia kazi kamati ya Uchaguzi ifanye kazi yake alisema Blatter mwenye...

Like
306
0
Thursday, 29 January 2015
AFCON: KOCHA WA IVORY COAST AMESEMA MASHINDANO YANAANZA SASA
Slider

Kocha wa Ivory Coast Herve Renard amesema mashindano ya kombe la mataifa Afrika yameanza sasa kwa timu yake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon siku ya jumatano ambapo ushindi huo uliwapeleka katika hatua ya robo fainali. Kocha alisema “kwa timu kama hii kombe la mataifa ya afrika linaanza katika robo fainali kwasababu kutolewa kabla ya kuifikia hatua hiyo ni kushindwa ” alisema kocha huyo Mfaransa ambae timu yake ameweza kupenya kwenye hatua hiyo ngumu na kuziacha timu kama...

Like
330
0
Thursday, 29 January 2015
MAHAKAMA YAMPA LUDA MAMLAKA YA MALEZI YA MTOTO WAKE
Entertanment

Ludacris amepata kile alichokuwa akikihitaji kwenye mahakama ya kusuluhisha migogoro ya kifamilia ambapo mahakama imempa mamlaka katika malezi ya mtoto wake mwenye miezi 13 Maamuzi hayo ya mahakama yamekuja mara baada ya mama wa mtoto huyo Tamika Fuller alipotoa ushahidi katika mahakama hiyo kwa kueleza kwamba Ludacriss aliikataa mimba ya mtoto huyo lakini pia alienda mbali kwa kusema alitaka mimba itolewe lakini chanzo cha habari kimeeleza kuwa jaji alipitia ripoti ya mtaalam wa kujitegemea na ushahidi ambapo mahakama imeridhia kuwa...

Like
276
0
Thursday, 29 January 2015
VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI KUJADILIWA BRUSSELS
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje kutoka Ulaya watakutana mjini Brussels kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kufuatia mashambulizi ya Mashariki mwa Ukraine. Mkutano huu wa dharula umeitishwa baada ya raia 30 kuuawa kwa makombora, mauaji yaliyotekelezwa na Waasi wanaodaiwa waliungwa mkono na Urusi na kushambulia bandari ya Mariupol Mwishoni mwa wiki iliyopita. Majeshi ya NATO yamesema mamia ya vifaru vya Urusi, Magari ya Silaha yalikua Mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi imekana kujihusisha moja kwa moja na mashambulizi hayo.  ...

Like
253
0
Thursday, 29 January 2015
JAPAN KUCHUNGUZA SAUTI INAYOHISIWA KUWA NI YA MWANDISHI ALIESHIKILIWA MATEKA NA IS
Global News

JAPAN inachunguza sauti iliyorekodiwa ambayo inawezakana ni ya mwandishi wa habari wa Japan aliyeshikiliwa mateka na wapiganaji wa Islamic state. Sauti hiyo inarudia tishio la kumuua rubani wa Jordan aliyetekwa mateka na wapiganaji hao hadi Jordan itakapomwachia huru mwanamke wa Iran aliyehusika na shambulizi la bomu. Famili ya Rubani na mpiganaji mwenye asili ya Jordan anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa hao wameendelea kuweka shinikizo kwa Serikali ya Jordan kufanya kila iwezalo kuokoa maisha yake. Jordan imeahidi kumuachia...

Like
248
0
Thursday, 29 January 2015
ACT KIMELITAKA JESHI LA POLISI LITENDE HAKI KWA VYAMA VYOTE VYA SIASA
Local News

CHAMA cha Mabadiliko na Uwazi – ACT kimelitaka jeshi la Polisi litende haki kwa vyama vyote nchini kwa kuacha uwanja huru wa kufanya siasa pamoja na kujenga amani ya kudumu kwa watanzania.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho MOHAMMED MASSAGA amesema kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kuwanyima Uhuru Wanasiasa kufanya maandamano ni kinyume cha haki ya Mtanzania ambaye anapaza sauti katika kufikisha ujumbe...

Like
287
0
Thursday, 29 January 2015