WATU wasiopungua sita wameuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa Homs katikati mwa Syria. Gari hiyo ililipuka katika eneo lenye makazi ya watu na maduka katika kitongoji cha Akrama, ambacho kimekuwa kikishambuliwa mara kwa mara kwa sababu kinaonekana kuwa nyumbani kwa watu wa jamii ya Alawi ambao ni wafuasi wa rais wa Syria Bashar al Assad. Gavana wa mji wa Homs Talal Barrazi amethibitisha idadi ya vifo vilivyotokea akisema wengi walikuwa wanawake na watoto. Watu...
KUMETOKEA vurugu leo wakati wa zoezi la kuwaapisha Wenyeviti watatu wa Serikali za mitaa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam. Chanzo cha vurugu hizo ni baada ya Kaimu Afisa Uchaguzi Manispaa ya Ilala Hilary Baina, kumteua Bwana Mariano Haruna kuwa ni mmoja wa wagombea ambaye amepata nafasi ya Uenyekiti eneo la Kigogo Fresh B kata ya Pugu. Kwa upande wake mgombea huyo wa Kigogo Fresh B, ambaye fanyiwa vurugu hizo, amekiri kuwa anastahiri na nimwenyekiti halali kutokana na...
KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Nchini Dubai katika Falme za Kiarabu, umefanikiwa kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri Watanzania kwenye Shirika hilo. Shirika Limekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo Maafisa wanaosimamia ajira kutoka Dubai wanatarajiwa kuja nchini Mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya kufanya usaili kwa Watanzania watakaoomba kazi kwenye Shirika hilo na kupata uteuzi wa awali. Mkurugenzi Idara...
Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Stromsgodset ya Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 16. Real Madrid hawakuweka wazi makubaliano yao na mshambuliaji huyo lakini vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa wamelipia si chini ya euro milioni tatu kumpata mchezaji huyo Anatarajiwa kuungana na klabu ya Real Madrid timu B ambayo inaongozwa na mwalimu Zinedine...
Kupitia interview aliyoifanya leo kwenye kipindi cha Genge kinachoruka kila siku ya jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana, mkali Mabeste alihusika kwenye Fresh beat leo ambapo alitambulisha wimbo wake mpya Usiwe bubu lakini pia alipata nafasi ya kuzungumzia mawili matatu yanayomuhu yeye na familia yake unaweza kuitazama interview hiyo hapa lakini pia kusikiliza na kudownload wimbo huo NEW AUDIO: Mabeste – usiwe...
MWENDESHA Mkuu wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC Fatou Bensouda ametaka kuwepo kwa juhudi mpya za kumkamata kiongozi wa kundi la waasi la Uganda la Lord’s Resistance Army LRA Joseph Kony baada ya kamanda wa ngazi ya juu wa kundi hilo Dominic Ongwen kufikishwa katika mahakama hiyo jana kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu. Bensouda amesema waathiriwa wa madhila yaliyofanywa na kundi la LRA linaloongozwa na Kony wamesubiri kwa muda mrefu kwa haki kutendeka....
MAKUNDI yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa. Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani. Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba...
SHIRIKISHO la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu limeanza kufanya uchaguzi kwa ngazi ya matawi ili kupata viongozi bora wa ngazi hiyo. Uchaguzi huo utafuatiwa na uchaguzi wa ngazi za mikoa na Taifa utakao anza march 24 mpaka april 12 mwaka huu Katibu mtendaji Mkuu wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kupitia chama cha mapinduzi ccm CHRISTOPHER NGUBIAGI amebainisha kuwa kiongozi bora ni yule anaye fuata misingi, kanuni na taratibu za kazi sambamba na...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA, kimeitisha Kikao cha Kamati kuu kitakachofanyika leo ambacho kitatoa maazimio na maamuzi ya chama kuhusu maswala mbalimbali kwa mustakabali wa wananchi kwa ujumla. Akizungumza na Wandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Afisa habari wa chama hicho Tumaini Makene, amesema kikao hicho pia kinajadili zoezi la uandikishwaji wa Daftari kudumu la wapiga kura. Hata hivyo Makene amesema swala la Elimu ya Katiba pendekezwa ikiwemo elimu ya kura ya maoni na Taarifa ya Ukawa kuelekea...
Lil wayne ameachia mixtape kufuatia kuchelewa kwa albam yake ya Carter V ambayo imesababisha ugomvi mkubwa kati yake na Birdman mmiliki wa cash money label. Mixtape hiyo inatajwa kuwa ni mixtape iliyolenga zaidi kuomba radhi mashabiki wake ambao wamekuwa wakiisubiri albam ya Carter V pia kuthibitisha hali kutokuwa shwari kati yake na uongozi wake Katika mixtape hiyo wimbo wa kwanza ni remix ya wimbo O.T. Genasis’ “CoCo,” ambapo Lil Wayne ametupia mzigo wa lawama kwa cash money kwa kuichelewesha albam...
Hii ndio kauli ya bingwa wa masumbwi duniani kutokea nchini Ufilipino Manny Pacquiao kwenye vyombo vya habari Pacquiao ametangaza rasmi kuachana kabisa na shughuri za kimuziki na kusema kwamba anaupenda muziki ila hadhani kama muziki unampenda “I love music, but I don’t think music loves me.” Pacquiao amesema hatotoa albam mpya tena . Pacquiao kwa sasa anapromote documentary lakini hadi hivi sasa amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata kupitia muziki, aidha Pacquiao ameongeza ya kuwa albam yake ya kwanza ilifikia mauzo ya...