Slider

WANAUME WAASWA KUSHIRIKI KATIKA MALEZI
Local News

WAZAZI hususani wakina baba wameaswa kushiriki katika Malezi ya Watoto ili wawajenge watoto na wakue katika fikra bora zitakazowapa amani, furaha na matumaini ya maisha yao. Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano wa Shirika linaloshughulikia Masuala ya watoto la SAVE THE CHILDREN INTERNATIONAL ELLEN OTARU OKOEDION wakati akizungumza na EFM juu ya namna Wazazi wanavyoweza kumlea mtoto katika malezi...

Like
262
0
Monday, 29 December 2014
NDEGE ILIYOPOTEA YAENDELEA KUTAFUTWA
Global News

Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo imepotea Desember 28 imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda. Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia....

Like
288
0
Monday, 29 December 2014
UPEPO MKALI NA MAWIMBI VYAKWAMISHA JUHUDI ZA UOKOAJI MELI ILIYOZAMA
Global News

IMEELEZWA KUWA Waokoaji wameendelea kupambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa abiria 300 ambao wamekwama ndani ya Ferry ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye Bahari ya Adriatic. Maofisa nchini Italia  meeleza kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea ambapo mpaka sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwenye Ferry...

Like
310
0
Monday, 29 December 2014
JAMII YATAKIWA KUKUMBUKA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NA HATARISHI
Local News

JAMII YA WATANZANIA imeaswa kuikumbuka Jamii ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi waliopo katika vituo mbalimbali nchini kwa kukaa nao ili kuwapa matumaini na kuwarejeshea furaha. Wito huo umetolewa na hivi karibuni na Mkurugenzi wa Kampuni ya Communication Media ROBERT FRANCIS wakati akizungumza na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishiwakati wa Kampeni ya Ushindi inayowakutanisha Watoto Yatima zaidi ya...

Like
436
0
Monday, 29 December 2014
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGIA MIRADI YA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuchangia miradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya Elimu. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Mradi wa Vitabu Vya Watoto Tanzania PILI DUMEI wakati akielezea mradi huo. DUMEI amebainisha kuwa Mradi huo unalenga lkuleta mabadiliko mbalimbali hasa kwa Jamii ya wanaopenda kusoma...

Like
308
0
Monday, 29 December 2014
MOUNRINHO: KUNA KAMPENI INAENDESHWA KUIANGUSHA CHELSEA LIGI KUU YA ENGLAND
Slider

Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema kuna kampeni inaendeshwa dhidi ya klabu yake ili isifanye vizuri ndani ya ligi kuu nchini England kwa kuwashawishi marefarii kutotoa maamuzi sahihi. Kocha huyo raia wan chini Ureno anayesifika kwa ubwatukaji amewashutumu makocha wenzake, watangazaji wa michezo pamoja na wachambuzi kuwa wanachangia kwa kiasi kikubwa klabu ya Chelsea kuandamwa na maamuzi ambayo siyo sahihi ndani ya uwanja. Maneno hayo ameyatoa baada ya kushuhudia mchezaji Cesc Fabregas kunyimwa penalty katika mchezo wa jana...

Like
450
0
Monday, 29 December 2014
MALI YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2015
Slider

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Mali, Cheick Omar Kone ametangaza kikosi cha awali kinachotaraji kwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwezi januari mwaka 2015 huko nchini Equatorial-Guinea. Kikosi hicho ambacho ni cha awali kabla ya kile cha mwisho kutangazwa mnamo tarehe tatu januari 2015 kimeshuhudia mshambuliaji wa klabu ya Metz, Modibo Maiga akirejea kundini baada ya kutoitwa kwa kipindi kirefu ndani ya timu hiyo. Abdou Traore na Cheick Diabate wanaokipiga katika klabu ya Bordeaux nao...

Like
382
0
Monday, 29 December 2014
INDONESIA YAFANYA KUMBUKUMBU YA MIAKA KUMI TANGU KUTOKEA KWA TSUNAMI
Global News

Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa Kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha Mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, Tsunami na kusababisha Vifo vya watu zaidi ya laki mbili. Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la Tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha...

Like
344
0
Friday, 26 December 2014
MWANAFUNZI ATIWA MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS
Global News

Polisi nchini Uturuki wamemkamata Mwanafunzi wa Sekondari mwenye umri wa 16 kwa tuhuma za kumtukana Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo amepelekwa mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana ERDOGAN na chama chake tawala cha AK kwa vitendo vya rushwa wakati wa Mkutano wa hadhara katikati ya mji wa...

Like
349
0
Friday, 26 December 2014
WANANDOA WAUAWA KIKATIRI MARA
Local News

WANANDOA wawili akiwemo mwanaume ambaye ni Mlemavu wa Macho wameawa kwa kukatwatwa mapanga na watu wasiojulikana na kisha kuchukuliwa baadhi ya viungo vyao katika kitongoji cha Mwabasabi,Wilayani Bunda Mkoani Mara. Wanandoa hao wameuawa saa mbili Usiku wakati wakitoka maeneo ya katikati ya kijiji hicho kusaga Nafaka. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara PHILIPO KALAGI amethibitisha kutokea kwa tukio...

Like
274
0
Friday, 26 December 2014
WAKAZI WA KIMARA BARUTI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MRIPUKO
Local News

WAKAZI WA KIMARA Baruti Jijini Dar  es salaam wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya Mripuko baada ya eneo wanalohifadhia taka  kujaa. Wakizungumza na EFM wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikuwa wakiweka taka hizo katika magari ya kuzolea taka lakini cha kushangaza magari hayo hayapiti hali inayowapelekea kukaa na taka hizo majumbani huku wengine wakizipeleka eneo la kilungule kwa ajili ya kutupa. Wameeleza kuwa tarari wameshatoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ili kutatua tatizo hilo lakini cha kushangaza mpaka...

Like
346
0
Friday, 26 December 2014